Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 6/15 uku. 3
  • Aliyeko Mkuu Zaidi Hana Kifani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aliyeko Mkuu Zaidi Hana Kifani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Habari Zinazolingana
  • Ule “Utatu Uliobarikiwa”—je! Umo Katika Biblia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Utatu Hufafanuliwaje?
    Je, Uamini Utatu?
  • Mungu ni Nani?
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Sehemu ya 1—Je! Yesu na Wanafunzi Wake Walifundisha Fundisho la Utatu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 6/15 uku. 3

Aliyeko Mkuu Zaidi Hana Kifani

ALIYEKO MKUU ZAIDI. Je! wewe unasadiki kuwako kwake? Ijapokuwa kutoka pole-pole katika makanisa kunakoenea sana katika nchi nyingi, mamilioni wangali wanasadiki katika Aliye mwenye nguvu zote, mwenye ukarimu ambaye kwaye wao wanaweza kumgeukia, hasa wanapokuwa katika taabu.

Kwa mfano, katika Afrika kuna makanisa mengi ya mahali mahali, ya kimapokeo yanayotofautiana sana moja na jingine na yanayoabudu miungu yenye majina mengi. Hata hivyo, watu wengi wanasadiki sana kuwapo kwa Aliyeko Mkuu Zaidi ambaye “hana kifani” na “msimamizi pekee wa ulimwengu wote.”

Kama ilivyosimuliwa katika kitabu cha Dakt. Peter Becker Tribe to Township, mzee Msotho mhubiri wa kawaida wa Afrika Kusini alisema: “Baba yangu mzee pamoja na baba yake . . . walijua juu ya Mungu, Molimo, muda mrefu kabla ya kuja kwa wamisionari, yule Mungu ambaye ndiye Aliyeko Mkuu Zaidi aliyeviumba vitu vyote . . . Je! ni kitu kwamba sisi [Wabasuto] tunamwita Mungu, Molimo, Wazulu, Nkulunkulu, Waxhosa, Thixo . . . ?”

Bila shaka, wingi wa majina unavuruga. Labda wewe utakubali kwamba Mungu wa ulimwengu wote mzima amepasa awe yule yule kwa watu wote na lazima awe na jina la ulimwengu wote mzima. Mkusanyo ulioongozwa na roho wa maandishi ya kale, Biblia, inaheshimiwa duniani pote. Inatangaza: “Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.” (Zaburi 83:18) Kwa hiyo, kulingana na Biblia, Aliyeko Mkuu Zaidi asiye na kifani ana jina lake mwenyewe lisilo na kifani.

Kama inavyofunuliwa na Biblia, ni wa aina gani huyo Aliyeko ambaye ni Mungu mmoja? “Njia zake zote ni haki”; “Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli”; “mwingi wa rehema, mwenye huruma”; “si Mungu wa machafuko, bali wa amani”; “Mungu ni upendo.”—Kumbukumbu 32:4; Kutoka 34:6; Yakobo 5:11; 1 Wakorintho 4:33; 1 Yohana 4:8.

Biblia pia inafunua kwamba Yehova peke yake Ndiye anayepaswa kuabudiwa. Ndiyo, akiwa asiye na kifani, kwa haki yeye anadai ibada ya pekee. (Kutoka 20:5) Yesu Kristo alisema: “Msujudie Bwana [Yehova, NW] Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.”—Mathayo 4:10.

Hata hivyo, Waafrika walio wengi zaidi, huku wakidai kusadiki kuwako kwa Aliyeko Mkuu Zaidi, wanaabudu miungu mingi. Je! jambo hilo halingeonekana kwako kuwa linadokeza mvurugo fulani kuhusu Mungu ni nani au yeye ukoje? Lakini hata katika sehemu nyingi za Jumuiya ya Wakristo, mtu wa Mungu aliye wazi, mwenye utukufu anaharibiwa kwa kumfikiria yeye kuwa Mungu mwenye nafsi tatu. Huenda ikawa umesikia juu ya jambo hili kuwa Utatu Mtakatifu, fundisho ambalo ni fumbo na gumu kuelewa. Kwa mfano, kijitabu The Blessed Trinity kinasema: “Fundisho la Utatu Uliobarikiwa . . . ni fumbo . . . Haliwezi kuthibitishwa kwa kutoa sababu . . . Haliwezi hata kuthibitishwa kuwa linawezekana.”a (Italiki ni zao.) Kijitabu hicho kinaongezea: “Kwa sababu hii, uthibitisho wa fumbo unatia ndani kuonyesha kwamba umo katika ufunuo, katika Maandiko Matakatifu.”

Lakini je! Maandiko Matakatifu kweli kweli yanafundisha fundisho hili? Je! Aliyeko Mkuu Zaidi ni watu watatu katika Mungu mmoja?

[Maelezo ya Chini]

a Kilichochapishwa na Catholic Truth Society ya London.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki