Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 6/15 kur. 22-26
  • Kutoa Ushahidi Katika Ufaransa Bara Lenye Unamna-namna

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoa Ushahidi Katika Ufaransa Bara Lenye Unamna-namna
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • ALSACE
  • BRITTANY
  • MILIMA ALPS
  • BONDE LOIRE
  • CORSICA
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 6/15 kur. 22-26

Kutoa Ushahidi Katika Ufaransa Bara Lenye Unamna-namna

UFARANSA ni nchi yenye unamna-namna mwingi. Milima yenye adhama, vilima vyenye kuteremka-teremka, magenge ya miamba yenye kupigwa na dhoruba, fuo za bahari zenye mchanga na ujoto, nyanja wazi za nafaka, mashamba madogo yaliyozungushiwa nyua, mashamba makubwa ya mizabibu, ardhi za mifugo, misitu ya misunobari na miti yenye kupukusa majani, vitongoji, vijiji, miji, majiji makubwa ya ki-siku-hizi—Ufaransa ni changanyiko la yote hayo, na zaidi.

Ingawa sehemu kubwa ya eneo la mashambani imedumu ikiwa na uvutio wayo, tamasha ya kijamii ya Ufaransa imepatwa na mabadiliko ya haraka sana katika miaka ya majuzi. “Jamii ya Kifaransa haipiti katika kipindi cha mashaka makubwa,” yasema chapa ya 1989 ya Francoscopie, “bali inapita katika msukosuko wa kweli kweli. Miundo ya kijamii, viwango vya maadili, viwango vya utamaduni, na mitazamo inapatwa na mabadiliko ya kina kirefu kwa mwendo wenye kuongezeka.”

Mabadiliko makubwa hayo yameathiri pia sehemu ya kidini. Ingawa Ukatoliki ungali ndiyo dini ya walio wengi sana, sasa imekuwa pokeo hasa kuliko kuwa dini yenye uvutano wowote halisi juu ya maisha ya washiriki walio wengi. Ubaridi wa watu unaoongezeka kuelekea viwango vya kiroho umekomesha ukuzi wa makanisa.

Kwa utofautiano kabisa, utendaji wa Mashahidi wa Yehova katika Ufaransa umesonga mbele kwa haraka sana katika miaka michache iliyopita. Kuanzia Alsace kaskazini-mashariki hadi Brittany katika Bahari Kuu ya Atlantiki, kuanzia ile milima mirefu ya Alps hadi lile Bonde Loire lenye kushuka chini, hata katika kisiwa Mediterania cha Corsica, Mashahidi wakabili hali tofauti na kukutana na watu wenye malezi tofauti. Acheni tufunge safari ya utalii wa picha tuone jinsi ilivyo kuhubiri habari njema za Ufalme katika Ufaransa, lile bara lenye unamna-namna.—Mathayo 24:14.

ALSACE

Kwa kupakana na Ujeremani, Alsace ni mkoa ujulikanao sana kwa mashamba yao ya mzabibu na vijiji vya kuvutia vilivyojaa maua. Strasbourg, mji mkuu wao, imekuwa ngome ya Kiprotestanti tangu ule Mrekebisho wa Kidini, na Waalsatia kwa ujumla wana staha ifaayo kwa Biblia. Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakihubiri habari njema za Ufalme katika jimbo hilo tangu mapema katika karne hii. Leo, kazi hiyo imesimamishwa imara, kama ionyeshwavyo na jambo lililoonwa la kijana mmoja jina lake Sylvie, aliyetumia kwa faida fursa ya kuhubiri shuleni.

Katika mazungumzo pamoja na wanadarasa kadhaa, Sylvie alitokeza kusudi la maisha na matazamio ya wakati ujao. Mvulana mmoja alipendezwa kadiri iliyotosha kumwacha Sylvie na Shahidi mwingine wamtembelee nyumbani. “Ingawa kijana huyu Mkatoliki alikuwa amekuwa mvulana mwenye kutumika katika altare, alikuwa na maswali mengi yaliyokuwa hayajajibiwa kamwe,” akasema Sylvie. “Tuliitumia Biblia kujibu baadhi ya hayo, naye akakubali funzo la Biblia lenye ukawaida.” Kijana huyo mwanamume alibatizwa mwaka mmoja kufuata hapo na baada ya kustahili akaingia huduma ya wakati wote akiwa painia wa kawaida. Sylvie pia amekwisha chukua pendeleo hilo la utumishi.

BRITTANY

Brittany ni mkoa mmoja imara wa mapokeo ya Kikatoliki, nao unachomoza nje kuingia katika Bara Kuu ya Atlantiki. Hata hivyo, kupitia jitihada za udumifu za Mashahidi, idadi yenye kuongezeka ya watu katika eneo hilo wanaukubali ujumbe wa Ufalme. Hiki hapa ni kielelezo cha linalotukia katika jimbo hilo la kaskazini-magharibi mwa Ufaransa.

“Mume na mke vijana walihamia nyumba ya orofa iliyo juu yetu,” aripoti Shahidi mmoja wa huko. “Wakati fulani baadaye, nilimkuta mwanamke huyo kijana ngazini, akiwa amemshika mwanaye ndani ya mikono yake. Nilipojua kwamba jina la mwana huyo ni Yonathani, nikauliza mwanamke huyo kama alijua asili ya jina hilo. ‘Nafikiri latoka katika Biblia, lakini hilo tu ndilo nijualo,’ akajibu. Alisikiliza maelezo niliyotoa, naye akataja kwamba wote wawili yeye na mume wake walitatanishwa na Biblia. Ingawa tulikuwa na maongezi zaidi, hakuna jambo lolote thabiti lililositawi wakati huo.

“Kitambo fulani baadaye, mume na mke hao waliniomba ushauri juu ya matatizo fulani. Nilitumia Biblia kujibu, nao wakashangazwa na habari ilizozitoa. Niliwaalika tena wajifunze Biblia. Kesho yake yule mwanamke kijana alikubali. Majuma machache baadaye, mume wake alijiunga katika funzo. Sasa wote wawili ni Mashahidi waliobatizwa.”

MILIMA ALPS

Milima Alps yajulikana sana kwa mandhari ya kutazamisha. Watu huenda huko wakastaajabie vilele vyayo vyenye adhama, hasa Mont Blanc, mwinuko ulio mrefu zaidi katika Ulaya Magharibi. Katika jimbo hilo pia, idadi ya wahubiri wa Ufalme wamtukuzao Muumba inaongezeka. Watu wa umri wote na kutoka namna zote za maisha wanajiunga na idadi zao, kama vile usimulizi unaofuata uonyeshavyo.

Vijana wanne katika eneo hilo walikuwa na vioja vyenye kukumbukwa sana. Waliiba magari na bidhaa nyinginezo, wakalewa mara nyingi, wakatumia na kuchuuza dawa za kulevya, na kuhusika katika umalaya na kuwasiliana na roho. Walikuwa bila kazi ya kuajiriwa na katika matata ya mara nyingi pamoja na polisi, na wote walikuwa wamekuwa gerezani. Hata hivyo, wote wanne walikuwa wamesikia juu ya ukweli katika utoto wao kwa sababu familia zao zilikuwa zimejifunza pamoja na Mashahidi wa Yehova mara kwa mara.

Baada ya miaka kadhaa ya maisha ya fujo, mmoja wa vijana hao alifanya badiliko la moyo na kuamua kumtumikia Yehova. Hiyo ilisababisha mfululizo wa miitikio. Siku moja polisi walikuwa wakiendesha uchunguzi wao wa kikawaida, nao wakamwomba mmoja wa vijana hao afungue mfuko wake. Kwa kutarajia kupata dawa za kulevya au bidhaa za kuibwa, walishangaa kupata Biblia na vijitabu fulani tu. Kijana huyo mwanamume aliitumia Biblia kueleza kilicholeta mabadiliko katika maisha yake. Kwa kutatizwa kuamini hilo, mmoja wa polisi hao akauliza: “Wamaanisha kwamba wewe umeacha kuvuta sigareti, kunywa, au kutumia dawa za kulevya?” Mwishowe polisi hao walikubali elezo hilo na kumwacha aende zake bila lolote la ziada. Leo wanaume vijana hao wamebatizwa, wote wanatumikia katika kundi wakiwa watumishi wa huduma, na watatu kati yao ni mapainia wa kawaida.

BONDE LOIRE

Bonde Loire huitwa bustani ya Ufaransa. Hutandaa kuanzia Orléans, kilometa 110 kusini mwa Paris, hadi kwenye kinywa cha Mto Loire katika Pwani ya Atlantiki. Jimbo hili lajulikana kwa kastili zalo nyingi, ambazo hapo kwanza zilikuwa makao na malalo ya uwindaji ya wanaufalme. Kuna makundi ya Mashahidi wa Yehova katika miji yote mikubwa katika eneo hilo.

Wakati wa mapumziko ya shule siku moja, Emma mdogo, msichana mwenye urafiki na shauku wa miaka sita, alirudi darasani kumsalimu mwalimu wake. Kwa kushtuka kumwona mwalimu wake akivuta sigareti, alibubujika machozi akakimbia. Mwalimu alimfuata na kuuliza analilia nini, lakini Emma hakutaka kusema lolote. Mwalimu aliposisitiza, Emma alilia kwikwi akajibu: “Ni kwa sababu wewe unavuta sigareti. Utakuwa mgonjwa ufe!”

Kesho yake mwalimu aliita mama ya Emma kueleza jinsi alivyoguswa moyo na itikio la binti yake. Hivyo basi mama akaeleza msimamo wa Mashahidi kuhusu tumbako. Ndipo mwalimu huyo akaeleza usiri wa kwamba familia yao ilikuwa tayari imemwomba aache kuvuta sigareti lakini haikufanikiwa. Hata hivyo, safari hii aliguswa na itikio la moyo mweupe la Emma hivi kwamba akaacha kuvuta sigareti katika muda wa siku mbili tu.

CORSICA

Kisiwa cha Corsica, ingawa huitwa “kisiwa kilichotiwa manukato,” chajulikana pia kwa roho ya ugumu wa moyo ya wakaaji wacho, ambayo mara nyingi hutokeza mizozano ya umwagaji damu. Kwa miaka mingi Mashahidi walionwa kuwa dini “kutoka Bara.” Hata hivyo, nguvu za ukweli wa Biblia zinabadili mioyo ya watu wengi hapa.

Shahidi mmoja aliyebatizwa karibuni alisimulia kwamba wakati mmoja alirudi kutoka likizo akagundua kwamba vifaa vyote vyenye kubebeka vya shamba lake vilikuwa vimeibwa kutoka shirika lake. “Kwa kumtumaini Yehova,” yeye akatoa usiri wake, “niliweza kuitikia kwa njia iliyo tofauti na jinsi ningaliitikia zamani.” Alipokuwa akiongea na jirani zake, aliitaja hasara yake kwa utulivu.

“Baadaye, majirani fulani walipatwa na matatizo. Niliacha kazi yangu niende kuwasaidia. Siku chache baadaye, nilipokea simu kutoka kwa mmoja wao akiniomba niende upesi iwezekanavyo. Nikifikiri alikuwa matatani tena, nikaenda moja kwa moja. Alinialika niketi na kuniuliza hivi: ‘Wajua kwa nini nimekuomba uje? Ni kuhusu vifaa vyako. Ni mimi niliyeviiba. Lakini nilipoona mtazamo wako wenye fadhili na urafiki, nilijiambia, “Siwezi kumtenda yeye hivyo!” Na baada ya wewe kutusaidia, sikuweza kamwe kulala usiku.’” Ukristo wa kweli wenye kuzoewa kimatendo uliongoza kwenye tokeo zuri.

Mwishoni mwa vita ya ulimwengu ya pili, wakati kazi ya kutolea Ufalme ushahidi ilipofunguka tena katika Ufaransa, kulikuwa na Mashahidi 1,700 tu katika nchi nzima. Kazi ya kufikia idadi nzima ya watu kwa ujumbe wa Ufalme ilionekana kama jambo lisilowezekana. Hata hivyo, muda wa miaka iliyopita, Yehova amebariki watu wake katika Ufaransa kwa vifaa vyenye kuhitajiwa—mashine za uchapaji, Majumba ya Ufalme, Majumba ya Kusanyiko, na kadhalika—na roho yenye nia ya kuitimiza kazi. Leo, kukiwa na wahubiri watendaji zaidi ya 117,000, ujumbe wa kwamba Ufalme wa Yehova ulio mikononi mwa Kristo ndilo tumaini la pekee kwa jamii ya kibinadamu unahubiriwa kotekote katika hili bara lenye unamna-namna.

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 23]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

UFARANSA

BRITTANY

BONDE LOIRE

MILIMA ALPS

ALSACE

BAHARI KUUYA ATLANTIKI

BAHARIMEDITERANIA

MLANGO-BAHARI WA UINGEREZA

CORSICA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki