Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 4/15 kur. 3-4
  • Je! Mwongozo wa Kibinadamu Umeshindwa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Mwongozo wa Kibinadamu Umeshindwa?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Wafungwa wa Umaskini
    Amkeni!—1998
  • Waweza Kupata Wapi Mwongozo Wenye Kutumainika?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Jitihada za Kumaliza Umaskini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Majibu ya Maswali ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 4/15 kur. 3-4

Je! Mwongozo wa Kibinadamu Umeshindwa?

NI NANI aliyeumba vitu vyote? Ikiwa jibu lako ni “Mungu,” basi wakubaliana na mamilioni ya watu waaminio katika Mungu wa Biblia, aliye Muumba.

Bado, wengi waaminio katika Mungu huona vigumu kukubali kwamba yeye huhusika sana katika kusuluhisha matatizo ya wanadamu. Je! ni jambo liwezekanalo kufikiri kwamba Mungu ana programu itakayoiletea jamii ya kibinadamu kitulizo? Wengi hawaoni uthibitisho wowote ufaao kuonyesha kwamba hilo lawezekana.

Kwa muda wa maelfu ya miaka, wanadamu wamejaribu njia nyingi za kujisaidia katika kutafuta-tafuta masuluhisho, bila msaada wa Mungu. Lakini je, wanadamu wamepata masuluhisho? Au, je, matatizo yanakuwa mabaya na magumu zaidi kusuluhisha? Je! mwanadamu anashughulikiaje yale matatizo muhimu yaliyomo ulimwenguni leo?

Mstadi mmoja aeleza jambo hilo hivi: “Tangu ule Mvuvumko wa Viwanda, nchi zilizositawi zimenyonya kupita kiasi nyenzo za asili za ulimwengu kwa njia za uundaji na matumizi yasiyo ya kuhifadhi, zikisababisha uharibifu wa mazingira tufeni pote, kwa hasara ya nchi zinazositawi.

Mwanadamu aendelea kuiharibu dunia. Gazeti la habari la Argentina liitwalo Clarín lilieleza hivi: “Katika nusu ya pili ya karne hii, uchoyo wa kiuchumi, utovu wa uangalifu, na uzembe ulisababisha misiba mikubwa ambayo iliua wanadamu na pia kushusha hali ya mazingira, mara nyingi kufikia hatua zisizopimika.”

Sasa umaskini wa kupita kiasi waonekana kuwa jambo la kudumu katika jamii ya ki-siku-hizi. Hata zile nchi ziitwazo eti nchi tajiri za ulimwengu zinalemewa na umaskini mwingi sana. Kulingana na The Globe and Mail la Toronto, Kanada, inakadiriwa kwamba “theluthi moja ya Wakanada wote watapatwa na umaskini wakati fulani wanapokuwa na umri ufaao wa kufanya kazi.” Gazeti hilo la habari laongeza kwamba “mvunjiko wa familia ni mojayapo sababu kuu za umaskini, na mwelekeo huo umeongezeka katika miaka ya karibuni.”

Matumizi mabaya ya madawa ni ishara nyingine ya kuzorota kwa jamii. Wanadamu waweza kufanya nini kuhusu hilo? Kwa wazi ni machache sana kwa ujumla. Mamilioni ya watu waendelea kupatwa na mshuko wa hali ya kimwili, ya kiakili, na ya kiadili likiwa tokeo la moja kwa moja la kutumia kwao vibaya madawa ya kutuliza maumivu. Na tatizo hilo linaenea vyepesi sana.

Yaonekana wanasayansi wanashindwa katika vita dhidi ya magonjwa. Ni kweli, tekinolojia ya ki-siku-hizi imeshinda mapigano mengi. Bado, baadhi ya taratibu za kisayansi nazo zimechangia kule kutokea kwa aina mpya za vijiumbe-maradhi vya hatari vinavyokinza madawa.

Serikali za kibinadamu haziwezi kuzuia ule mweneo mkubwa wa kuvunjwa kwa haki za kibinadamu. Kwa kielelezo, zijapokuwa zile ahadi na sheria zilizofanyizwa ili kuzuia utumwa, inakadiriwa kwamba kotekote ulimwenguni watu zaidi ya milioni mia moja wanalazimishwa kufanya kazi chini ya hali zilizo kama za utumwa wa mwisho.

Lakini kwa nini mwongozo wa kibinadamu umeshindwa? Fikiria mambo haya. Mwongozo wa kibinadamu watoka kwa watu—watu walio na mipaka mikubwa. Wameona maisha kwa muda mfupi kwa kulinganishwa na kwa kawaida huzuiwa na tamaduni au mazingira fulani-fulani. Ujuzi wao una mipaka pia. Mwongozo wowote watoao huonyesha mipaka hiyo. Kama vile mtume Paulo alivyosema, “wote wamefanya dhambi, na [h]upungukiwa na utukufu wa Mungu.”—Warumi 3:23.

Kwa kweli mengi ya matatizo na magumu ambayo sehemu kubwa zaidi ya jamii ya kibinadamu inapatwa nayo ni tokeo ama la moja kwa moja ama lisilo la moja kwa moja la kupuuza mwongozo wa Mungu. Lakini mwongozo huo waweza kupatikana wapi? Mungu hutuandaliaje mwelekezo leo? Makala ifuatayo itazungumzia majibu hayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki