Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 7/15 uku. 31
  • Wafundishe Tangu Utoto Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wafundishe Tangu Utoto Sana
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 7/15 uku. 31

Wafundishe Tangu Utoto Sana

UTAFITI wa kisasa huonyesha kwamba “vijusu vina maitikio ya kisaikolojia kuelekea sauti mbalimbali.” Watafiti wa Chuo Kikuu cha Carolina Kaskazini “waligundua kwamba baada ya mama mbalimbali kuwasomea watoto wao walio kwenye tumbo la uzazi, watoto waliotoka kuzaliwa waliitikia wakati vifungu hivyo vya maneno viliposomwa tena,” lasema Winnipeg Free Press. Wanawake wasomapo kwa sauti kubwa wakiwa waja-wazito, huenda hilo likachangia sana kukazia kikiki katika mtoto kanuni nzuri za kiadili. Biblia husema kwamba Timotheo ‘aliyajua maandishi matakatifu tangu utoto sana.’ (2 Timotheo 3:14, 15, NW) Ni wazi kwamba mama yake na nyanya yake waling’amua thamani ya kumzoeza tangu utoto sana, mazoezi ambayo yaelekea yalitia ndani kusoma kwa sauti.

Kusoma ndiko “ustadi wa maisha wenye uvutano zaidi tulio nao katika jamii yetu leo,” asema mtungaji Jim Trelease. Stadi za lugha na msamiati huongezwa kwa kusoma kwa sauti.

Ni jambo lenye hekima kuanza kusoma kwa sauti angalau mara tu uanzapo kuzungumza na kitoto chako kichanga. Hata ingawa mwanzoni mtoto wako ambaye bado hajazaliwa au aliyetoka kuzaliwa hataelewa yale unayosema, manufaa za muda mrefu ziwezazo kupatikana zafanya usomaji huo ustahili. Mithali 22:6 yasema: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”

Ni nini uwezacho kusoma ambacho ni chenye kutumika na pia chenye manufaa? Msomee mtoto wako Biblia kwa sauti kila siku. Pia soma vichapo vingine vyenye mafaa, kama Kumsikiliza Mwalimu Mkuu, Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi, na makala katika magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni!

Ni kweli kwamba, kujitoa mwenyewe kwa njia hii huhusisha wakati, lakini ni wakati utumiwao vizuri. Ni njia halisi ya kuonyesha kwamba unamjali na kumpenda mtoto wako.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki