Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 4/1 uku. 19
  • Lile “Koti Takatifu la Trier”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Lile “Koti Takatifu la Trier”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Wao Huenda Kuitazama Hiyo Kanzu?
  • “Shika Upindo wa Nguo ya Mtu Aliye Myahudi”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
  • Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye Thamani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Dumisheni Muungano Katika Siku Hizi za Mwisho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Umoja wa Kikristo Unamletea Mungu Utukufu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 4/1 uku. 19

Lile “Koti Takatifu la Trier”

TRIER, likiwa na historia ndefu inayorudi nyuma miaka 2,000, ndilo jiji la zamani zaidi katika Ujerumani.a Kwa karne nyingi Trier limepata kuwa na uhusiano wenye nguvu pamoja na Kanisa Katoliki. Katika mwaka wa 1996 kanisa kuu katika Trier lilionyesha salio ambalo ladhaniwa kwamba ni la kale kama jiji lenyewe. Linaitwa Koti Takatifu la Trier.

Hilo koti lina urefu wa meta 1.57 na upana wa meta 1.09 na mikono yake ni nusu ya urefu walo. Limetengenezwa kwa pamba na, kulingana na Hans-Joachim Kann katika kitabu chake Wallfahrtsführer Trier und Umgebung (Mwongozo wa Safari ya Trier na Mazingira), labda lilivaliwa likiwa vazi la nje. Makadirio mengine huonyesha hilo vazi la asili—sehemu yalo kubwa ikiwa imeshonwa upya na kuimarishwa kwa vitambaa vingine kwa karne nyingi ni—la tangu karne ya pili au hata ya kwanza W.K. Ikiwa ni sahihi, hilo lingelifanya kuwa salio la kikale la vazi, kitambaa chenye kupendeza kwenye jumba la kuhifadhi vitu vya kale.

Hata hivyo, wengine husisitiza kwamba vazi hilo sio salio la kale tu bali pia ni takatifu—kwa hiyo laitwa Koti Takatifu. Hiyo ni kwa sababu lilikuwa bila mshono, kama lile vazi la ndani lililovaliwa na Yesu Kristo. (Yohana 19:23, 24) Wengine hudai kwamba “Hilo Koti Takatifu” kwa hakika lilikuwa la Mesiya.

Hakuna uhakika wa jinsi koti hilo lilivyofika huko Trier. Kitabu kimoja cha marejezo chaeleza kwamba “lililetwa jijini humo na malkia Helena, mama ya Konstantino Mkubwa.” Kann aeleza kwamba ripoti ya kwanza yenye kutegemeka ya kuwapo kwa hilo vazi katika Trier ni kutoka mwaka wa 1196.

Hilo koti, ambalo limewekwa katika kanisa kuu, limewekwa lionekane na watu pindi tofautitofauti tangu karne ya 16. Mathalani, liliwekwa mwaka wa 1655, muda mfupi baada ya Vita ya Miaka Thelathini, iliyokuwa yenye gharama kubwa sana kwa Trier. Mauzo ya vitu vya ukumbusho wa safari yametokeza mapato mengi pindi kwa pindi.

Kumekuwa na safari tatu za “Koti Takatifu” karne hii—katika miaka ya 1933, 1959, na 1996. Katika mwaka wa 1933 hiyo safari ilitangazwa siku ileile Hitler aliwekwa rasmi kuwa chansela wa Utawala wa Ujerumani. Kann aonyesha kwamba sadfa hiyo ya matukio hayo mawili kwenye tarehe ileile yakazia hali zilizozunguka safari hiyo. Askari wa Kinazi wakiwa na mavazi rasmi walifanya gwaride la heshima nje ya kanisa kuu kwa ajili ya hao wasafiri. Watu milioni mbili na nusu walitazama hiyo kanzu mwaka huo.

Herbert, mkazi wa Trier kwa miaka mingi, alilinganisha idadi ya wasafiri katika mwaka wa 1959 na 1996. “Katika mwaka wa 1959 barabara zilijaa umati, kukiwa na vibanda vyenye kuuza vitu vya kumbukumbu kwenye karibu kila kona barabarani. Mwaka huu hiyo sherehe ni tulivu zaidi.” Kwa kweli, ni watu 700,000 tu waliotazama hiyo kanzu katika mwaka wa 1996, idadi inayopungua kwa milioni moja ile ya mwaka 1959.

Kwa Nini Wao Huenda Kuitazama Hiyo Kanzu?

Kanisa hutia mkazo kwamba hiyo kanzu haipasi kuonwa kana kwamba ni kitu cha kupewa heshima. Hiyo kanzu isiyo na mshono yaonwa kuwa ufafanisho wa muungano wa kanisa. Gazeti la habari la Frankfurter Allgemeine Zeitung yaripoti kwamba alipokuwa akitangaza hiyo safari, Askofu Spital alisema hivi: “Hali isiyo ya kawaida ulimwenguni mwetu hutusai sisi Wakristo kuwa na majibu yasiyo ya kawaida. Lazima tupinge chuki, unyama, na jeuri inayozidi kuongezeka.” Huyo askofu alieleza kwamba kuitazama hiyo kanzu kungemkumbusha mtu juu ya muungano.

Lakini kwa nini yeyote ahitaji “Koti Takatifu” ili kukumbushwa juu ya muungano wa kanisa? Namna gani kama hiyo kanzu ingepatwa na madhara au ichanguke au ifichuliwe kuwa bandia? Je, muungano wa kanisa ungekuwa hatarini? Namna gani watu ambao hawawezi kusafiri hadi Trier? Je, wamepungukiwa katika kukazia uangalifu muungano wowote kanisani?

Maandiko Matakatifu hayataji Wakristo wa mapema wakihitaji vitu ili kuwakumbusha juu ya uhitaji wa muungano wa Kikristo. Kwa kweli, mtume Paulo aliwatia moyo Wakristo kwa maneno haya: “Kwa maana tunatembea kwa imani, si kwa kuona.” (2 Wakorintho 5:7) Hivyo muungano ambao Wakristo wa kweli hufurahia hufafanuliwa kuwa “umoja katika imani.”—Waefeso 4:11-13.

[Maelezo ya Chini]

a Ona Amkeni! la Aprili 22, 1980, kurasa 21-23, la Kiingereza.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki