Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 7/15 uku. 3
  • Waweza Kuwalindaje Watoto Wako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Waweza Kuwalindaje Watoto Wako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wanahitaji Mengi Zaidi ya Riziki
  • Unataka Watoto Wako Wawe na Wakati Ujao wa Aina Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2003
  • Vijana na Dawa za Kulevya
    Amkeni!—2003
  • Jinsi Ambavyo Dawa za Kulevya Haramu Huathiri Maisha Yako
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 7/15 uku. 3

Waweza Kuwalindaje Watoto Wako?

BAADA ya kusomea shule jirani kwa miaka kadhaa, Wernera alianza masomo ya juu pamoja na vijana wengine wapatao 3,000 katika São Paulo, Brazili. Kwa mara ya kwanza, aliona wanafunzi wenzake wakiuza na kutumia dawa za kulevya. Kwa vile alikuwa na umbo dogo, upesi alidhulumiwa kwa kuteswa na wanafunzi wa zamani.

Eva pia, dadake Werner, alikuwa na matatizo. Akitaka kufanya vema zaidi, alisoma kwa bidii sana hata akachoka kimwili na kihisia-moyo na kuvurugika akili. Kama ilivyo na wabalehe wengine, Werner na Eva walihitaji ulinzi wa kimwili na wa kihisia-moyo pia. Watoto wako wanahitaji msaada wa namna gani? Unaweza kuwatayarishaje kwa ajili ya maisha ya wakati watakapokuwa watu wazima? Kwa kweli, unataka watoto wako wawe na wakati ujao wa aina gani?

Wanahitaji Mengi Zaidi ya Riziki

Ebu fikiria kwa dakika ule ugumu ambao wazazi hukabili katika kuwalinda watoto wao leo. Katika nchi nyingi, idadi ya watoto wanaoishi mitaani inaongezeka kwa sababu ya kushuka kwa kiwango cha maisha ya familia na kuongezeka kwa umaskini. Kutumia watoto kufanya kazi ni tokeo la kushindwa kuwalinda wachanga dhidi ya kutumiwa ili kujifaidi. Matumizi mabaya ya dawa za kulevya pia huharibu wachanga wengi. Kwa mfano, tineja fulani kutoka Brazili alipokuwa mraibu wa dawa za kulevya, amani ilitoweka nyumbani mwake. Mbali na mkazo wa kihisia-moyo uliowapata wazazi wake, walipambana pia na kugharimia kupona kwake, nao wachuuzi wa mihadarati wasio na huruma walikuja nyumbani kwao kudai malipo.

Hata hivyo, licha ya mikazo ya maisha, wazazi wengi huendelea na pambano la kuwaandalia watoto wao chakula, mavazi, na makao na pia ulinzi dhidi ya jeuri, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, na matatizo mengine. Kufanya hivyo ni jitihada nzuri, lakini je, kunatosha? Namna gani ulinzi dhidi ya madhara ya kihisia-moyo na ya kiroho? Wengi hung’amua kwamba kulea watoto kwa mafanikio hutia ndani kupambana na magumu yahusishayo tafrija na marafiki ambao watoto wao huchagua. Hata hivyo, wazazi wanaweza kuepukaje kuwa ama wenye kuwalinda kupita kiasi ama kuwa waendekevu mno? Unaalikwa kuchunguza majibu yapatikanayo katika makala inayofuata.

[Maelezo ya Chini]

a Majina yamebadilishwa katika makala hii.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki