Msomi Aipa Hati ya Biblia Tarehe Mpya
Kulingana na Carsten Peter Thiede, mtaalamu Mjerumani wa elimu ya hati za mafunjo, kuna ithibati yenye nguvu kwamba vipande vitatu vya mafunjo ya Gospeli ya Mathayo (viitwavyo Mafunjo ya Magdalen) viliandikwa katika karne ya kwanza.
Baada ya kuvilinganisha vipande (vyenye sehemu za Mathayo sura ya 26) na barua nyingine ya kale ya kibiashara iliyopatikana Misri, Thiede aliona kwamba ile hati ya kutoka Misri yafanana sana na “hati ya mafunjo ya Magdalen—kwa kuonekana kwa ujumla na kwa umbo na muundo wa herufi mojamoja.” Thiede na Matthew D’Ancona mtungaji-mwenzi wa kitabu chao Eyewitness to Jesus—Amazing New Manuscript Evidence About the Origin of the Gospels wafikia mkataa wa kwamba ufanani kati ya hati hizo mbili huonyesha kwamba ziliandikwa karibu wakati mmoja. Lini? Hati hiyo ya kibiashara imepewa tarehe ya “‘Katika mwaka wa 12 wa Bwana Nero, Epeiph 30’—ambayo, kulingana na kalenda yetu ni Julai 24, 66 [W.K.].”
“Ikiwa utaratibu huu wa kuweka tarehe ni sahihi, basi ni wa maana sana,” aeleza Profesa Philip W. Comfort, kwenye makala iliyochapishwa katika Tyndale Bulletin, “kwa kuwa yakadiria tarehe ya hati ya Gospeli ya Mathayo kuwa katika karne ileile ambayo gospeli hiyo iliandikwa.” Waweza pia kuyafanya Mafunjo ya Magdalen kuwa vipande vya Gospeli vya zamani zaidi vilivyopo.
[Picha katika ukurasa wa 29]
Mafunjo ya Magdalen ambayo yameonyeshwa katika ukubwa halisi
[Hisani]
By permission of the President and Fellows of Magdalen College, Oxford