Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 6/1 uku. 3
  • Je, Neno “Mkristo” Linapoteza Maana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Neno “Mkristo” Linapoteza Maana?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mwelekeo wa Kupendelea Mabadiliko
  • Uchunguzi Muhimu Zaidi Unaoweza Kufanya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Ukristo wa Kisasa Ni wa Kweli Kiasi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Je, Ukristo Umeshindwa?
    Amkeni!—2007
  • Kanisa La Kweli na Msingi Wake
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 6/1 uku. 3

Je, Neno “Mkristo” Linapoteza Maana?

INAMAANISHA nini kuwa Mkristo? Ungejibuje? Bila kufuata mpango maalumu watu katika nchi mbalimbali waliulizwa swali hilo, na yafuatayo ni baadhi ya majibu waliyotoa:

“Kumfuata Yesu na kumwiga.”

“Kuwa mtu mwema na kuwapa watu wengine vitu.”

“Kumkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi.”

“Kuhudhuria Misa, kusali ukitumia Rozari na kula mkate na kunywa divai.”

“Siamini kama ni lazima uende kanisani ndipo uwe Mkristo.”

Hata kamusi hutoa mafafanuzi mengi yenye kutatanisha. Kamusi moja hata ina mafafanuzi kumi ya neno “Mkristo,” na baadhi ya mafafanuzi hayo ni, “kuamini au kuwa mfuasi wa dini ya Yesu Kristo” na, “mtu mwenye adabu au mwenye kukubalika.” Si ajabu kwamba wengi hushindwa kufafanua kinachomaanishwa na kuwa Mkristo.

Mwelekeo wa Kupendelea Mabadiliko

Leo, miongoni mwa watu wanaodai kuwa Wakristo—hata miongoni mwa waumini wa dini moja—unaweza kupata maoni tofauti-tofauti kuhusu mambo kama kupuliziwa kwa Biblia na Mungu, nadharia ya mageuzi, kujiingiza kwa kanisa katika siasa, na kujulisha wengine imani yako. Masuala ya kiadili juu ya mambo kama utoaji-mimba, ugoni-jinsia-moja, na wanaume na wanawake kuishi pamoja bila kuoana, mara nyingi hutokeza mijadala mikali. Hakuna shaka kwamba wengi wanapendelea mabadiliko.

Kwa mfano, hivi majuzi baraza moja la hukumu la kanisa moja la Kiprotestanti lilipiga kura kuunga mkono haki ya kanisa ya “kuchagua mtu anayejulikana wazi kuwa mgoni-jinsia-moja awe mzee kwenye kamati inayoongoza kanisa hilo,” laripoti jarida la Christian Century. Wanatheolojia fulani hata wametoa maoni kwamba imani katika Yesu si muhimu kwa wokovu. Wanaamini kwamba Wayahudi, Waislamu, na wengineo “wanaweza pia kuingia mbinguni [kama vile tu Wakristo],” yasema ripoti moja katika gazeti la The New York Times.

Ukiweza, ebu wazia Mfuasi wa Maksi akitetea ubepari au mtetezi wa demokrasia akiendeleza utawala wa mabavu au mtetezi wa mazingira akiunga mkono ukataji-miti. “Mtu huyo kwa kweli si Mfuasi wa Maksi wala mtetezi wa demokrasia wala mtetezi wa mazingira,” unasema—na inaweza kuwa unasema kweli. Lakini unapochunguza maoni mbalimbali ya watu wanaodai kuwa Wakristo leo, unaona itikadi zinazotofautiana sana na ambazo mara nyingi hupinga mafundisho ya Mwanzilishi wa Ukristo, Yesu Kristo. Maoni hayo yanaonyesha nini kuhusu aina yao ya Ukristo?—1 Wakorintho 1:10.

Tamaa ya kubadili mafundisho ya Kikristo ili yapatane na maoni ya watu wa kizazi fulani ni ya zamani sana, kama tutakavyoona. Mungu na Yesu Kristo wanayaonaje mabadiliko hayo? Je, makanisa yanayounga mkono mafundisho ambayo hayakuanzishwa na Kristo yanaweza kwa kufaa kujiita ya Kikristo? Maswali hayo yatajibiwa katika makala ifuatayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki