Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 4/1 uku. 3
  • Mlo wa Jioni wa Bwana Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mlo wa Jioni wa Bwana Ni Nini?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Mlo wa Jioni wa Bwana Una Maana Kubwa Kwako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Kuadhimisha Kifo cha Mwanamume Mkuu Zaidi Aliyepata Kuwa Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Mlo wa Mwisho wa Jioni wa Yesu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Tukio ambalo hupaswi kukosa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 4/1 uku. 3

Mlo wa Jioni wa Bwana Ni Nini?

MANENO haya, “mlo wa jioni wa Bwana,” yanakukumbusha nini? Watu wengi watafikiria mchoro unaovutia sana wa mchoraji Leonardo da Vinci (1452-1519) huko Milan, Italia. Bila shaka, kwa karne nyingi, wasanii, waandishi, na wanamuziki wamevutiwa sana na Mlo wa Jioni wa Bwana.

Lakini, Mlo wa Jioni wa Bwana ni nini, nao una maana gani kwa watu wanaoishi katika karne ya 21? Ensaiklopedia na kamusi mbalimbali huonyesha kwamba Mlo wa Jioni wa Bwana, ambao pia huitwa Chakula cha Bwana, ni mlo ambao Yesu Kristo na mitume wake walikula jioni kabla ya kifo chake cha kidhabihu. Kwa kawaida unaitwa Mlo wa Jioni wa Bwana kwa kuwa huo ndio uliokuwa mlo wake wa jioni wa mwisho pamoja na wafuasi wake waaminifu. Na kwa kuwa ulianzishwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe, jina Mlo wa Jioni wa Bwana linafaa.

Kwa karne nyingi wengi wamejitolea kufa kwa ajili ya mambo wanayoona kuwa yanafaa. Baadhi ya vifo hivyo viliwafaidi watu fulani kwa muda. Ingawa huenda watu fulani wakasifu vifo hivyo, haviwezi kulinganishwa na kifo cha Yesu Kristo ambacho ni chenye maana kubwa. Isitoshe, hakuna kifo katika historia ya wanadamu yenye matatizo kinachoweza kufaidi watu ulimwenguni pote kama cha Yesu. Kwa nini?

Ili kujibu swali hilo na kukusaidia uelewe Mlo wa Jioni wa Bwana una maana gani kwako, tunakuomba usome makala inayofuata.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki