Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w04 7/1 uku. 3
  • Je, Tumlaumu Mungu kwa Matatizo Yetu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Tumlaumu Mungu kwa Matatizo Yetu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Tulimjaribu Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Katika Ujeremani Uliofuata baada ya Vita Vijana Wamsifu Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Mungu Anakujali Kwelikweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Waambie Unawapenda
    Masimulizi ya Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
w04 7/1 uku. 3

Je, Tumlaumu Mungu kwa Matatizo Yetu?

WAKATI binti ya Marion, aliye mtu mzima, alipopata jeraha baya la ubongo, Marion alifanya jinsi ambavyo wengi wetu tungefanya.a Alimwomba Mungu amsaidie. “Sikumbuki wakati mwingine wowote ambapo nimewahi kuhisi nikiwa mpweke hivyo na bila msaada,” asema Marion. Baadaye, hali ya binti yake ilizorota, naye Marion akaanza kuwa na shaka kumhusu Mungu. “Kwa nini jambo hilo lilitukia?” akauliza. Hangeweza kuelewa kwa nini Mungu mwenye upendo na mwenye kujali angeweza kumwacha.

Ni jambo la kawaida kabisa kuhisi jinsi Marion alivyohisi.Watu wengi duniani wamehisi kwamba Mungu amewaacha wakati wa uhitaji. “Bado sijui ‘kwa nini MUNGU huruhusu mambo mabaya yatokee,’” asema Lisa baada ya mjukuu wake kuuawa. “Bado sijapoteza imani kabisa katika Mungu, lakini imepungua.” Pia, mwanamke mmoja alisema hivi baada ya mtoto wake mchanga wa kiume kuhusika katika msiba fulani wa kipumbavu: “Mungu hakunifariji kwa yaliyotokea. Hakunionyesha kama ananijali au kunihurumia.” Aliongeza kusema: “Sitamsamehe Mungu kamwe.”

Wengine hujawa na uchungu kumwelekea Mungu wanapotazama ulimwengu wanamoishi. Wao huona nchi zilizolemewa na umaskini na njaa, wakimbizi wa vita wasio na tumaini, watoto wengi waliopoteza wazazi kwa sababu ya UKIMWI, na mamilioni ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa mengine. Kwa sababu ya misiba hiyo na mingineyo, wengi humlaumu Mungu kwa kuwa inaonekana kama hajali.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba si Mungu anayesababisha matatizo yanayowapata wanadamu. Kwa kweli, kuna sababu zifaazo za kuamini kwamba hivi karibuni Mungu atabatilisha madhara yote ambayo yamewapata wanadamu. Tunakualika usome makala inayofuata na uone kwamba Mungu anatujali kwelikweli.

[Maelezo ya Chini]

a Majina yamebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki