Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w10 11/1 uku. 4
  • Wapende Watu, Bali Si Pesa na Mali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wapende Watu, Bali Si Pesa na Mali
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Pesa
    Amkeni!—2014
  • Je, Pesa Ndio Chanzo cha Uovu Wote?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Unaweza Kudumishaje Maoni Yaliyosawazika Kuhusu Pesa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Kuridhika na Kuwa Mkarimu
    Amkeni!—2018
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
w10 11/1 uku. 4

Njia ya 1

Wapende Watu, Bali Si Pesa na Mali

BIBLIA INAFUNDISHA NINI? “Kupenda pesa ni chanzo cha mambo mabaya ya namna zote.”—1 Timotheo 6:10.

KWA NINI INAWEZA KUWA VIGUMU? Matangazo ya biashara yanatuchochea kutoridhika na vitu tulivyo navyo. Wanaotoa matangazo hayo wanataka tufanye kazi kwa muda mrefu ili tupate pesa za kununulia vitu vya kisasa zaidi, vizuri zaidi, na vikubwa zaidi. Pesa ni kishawishi, na ni rahisi sana kuanza kuzipenda. Hata hivyo, Biblia inaonya kwamba mtu anayependa pesa hatatosheka kamwe. Mfalme Sulemani aliandika hivi: “Anayependa fedha hatatosheka na fedha, wala anayependa mali hatatosheka na mapato.”—Mhubiri 5:10.

UNAWEZA KUFANYA NINI? Mwige Yesu, na ujifunze kuwapenda watu zaidi kuliko mali. Yesu alikuwa tayari kutoa vyote alivyokuwa navyo, hata uhai wake mwenyewe, kwa sababu aliwapenda watu. (Yohana 15:13) Alisema: “Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.” (Matendo 20:35) Tukijizoeza kutumia wakati na mali zetu kuwasaidia wengine, wao pia watatutendea vivyo hivyo. Yesu alisema, “Muwe na mazoea ya kuwapa watu, na watu watawapa ninyi.” (Luka 6:38) Wale wanaofuatilia pesa na mali wanapata mateso na maumivu. (1 Timotheo 6:9, 10) Kwa upande mwingine, uradhi wa kweli unatokana na kupendwa na kuwapenda wengine.

Kwa nini usijaribu kuchanganua hali zako na kuona kama unaweza kurahisisha maisha yako? Je, unaweza kupunguza vitu ulivyo navyo, au vitu unavyotaka kununua? Ukifanya hivyo, huenda ukagundua kwamba una muda na nguvu zaidi za kufanya mambo muhimu katika maisha, yaani, kuwasaidia watu na kumtumikia Mungu, ambaye amekupa vyote ulivyo navyo.—Mathayo 6:24; Matendo 17:28.

[Picha katika ukurasa wa 4]

“Muwe na mazoea ya kuwapa watu, na watu watawapa ninyi”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki