Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 3/1 uku. 15
  • “Nchi Inayotiririka Maziwa Na Asali”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Nchi Inayotiririka Maziwa Na Asali”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Asali—Zawadi ya Nyuki kwa Wanadamu
    Amkeni!—2005
  • Sababu Kwa Nini Matoleo ya Asali Hayakukubaliwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Ufugaji wa Nyuki—Hadithi “Tamu”
    Amkeni!—1997
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 3/1 uku. 15

“Nchi Inayotiririka Maziwa Na Asali”

YEHOVA MUNGU alipowakomboa Waisraeli kutoka Misri, aliwaahidi kuwa atawapeleka “kwenye nchi nzuri na kubwa, nchi inayotiririka maziwa na asali.”—Kutoka 3:8.

Waisraeli walipoingia katika Nchi ya Ahadi, walifuga ng’ombe, kondoo, mbuzi, na hivyo wakapata maziwa mengi sana. Namna gani asali? Watu fulani wanaamini kuwa neno asali linamaanisha umajimaji mtamu uliotengenezwa kutokana na tende, tini, au zabibu. Na katika sehemu nyingi ambapo Biblia inataja asali ya nyuki, inarejelea asali ya mwituni, bali si asali ya nyuki wa kufugwa. (Waamuzi 14:8, 9; 1 Samweli 14:27; Mathayo 3:1, 4) Je, kwa kweli nchi hiyo ‘ilitiririka’ asali na maziwa?

Uvumbuzi wa hivi karibuni wa vitu vya kale katika Israeli ya kisasa unatusaidia kuelewa jambo hilo. Kuhusu uvumbuzi huo, taarifa ya chuo kikuu kimoja (Hebrew University) inasema: “Hapa ndipo mahali pa kufugia nyuki pa kale zaidi kuwahi kuchimbuliwa katika Mashariki ya Karibu ya Kale, akasema Profesa (Amihai) Mazar. Eneo hilo lilitumiwa kwa ufugaji wa nyuki kuanzia karne ya 10 mpaka mwanzoni mwa karne ya 9 K.W.K.”

Wataalamu hao wa vitu vya kale walipata safu tatu zilizokuwa na jumla ya mizinga zaidi ya 30 ya nyuki, na walikadiria kuwa eneo lote lingeweza kuwa na mizinga 100 hivi. Mizinga hiyo ilipochunguzwa, mabaki ya nyuki na molekuli za nta ya nyuki zilipatikana. Wasomi wanakadiria kuwa “asali yenye uzito wa karibu nusu tani ingeweza kukusanywa kila mwaka katika mizinga hiyo.”

Nyakati za kale, asali ilikuwa chakula kitamu, nayo nta iliyotengenezwa kutokana na masega ilitumiwa katika viwanda vya kutengenezea bidhaa za chuma na ngozi. Nta pia ilitumiwa katika mabamba ya kuandikia. Mabamba hayo yalikuwa na sehemu iliyojazwa nta na mwandikaji angeweza kuandika ujumbe juu ya nta hiyo, kisha kuiyeyusha iwapo alitaka kuandika tena. Wataalamu wa vitu vya kale wamefikia mkataa gani baada ya uvumbuzi huu?

“Ingawa Biblia haituambii chochote kuhusu ufugaji wa nyuki nchini Israeli wakati huo,” inaendelea ile taarifa ya chuo kikuu, “uvumbuzi wa eneo la Tel Rehov ambapo nyuki walifugwa, unaonyesha kwamba ufugaji wa nyuki na ukusanyaji wa asali na masega ya asali ni kazi iliyokuwa imesitawi sana mapema wakati wa kipindi cha Hekalu la Kwanza [la Sulemani]. Kwa hiyo, inawezekana kuwa neno ‘asali’ katika Biblia linamaanisha asali ya nyuki.”

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 15]

Institute of Archaeology/Hebrew University © Tel Rehov Excavations

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki