Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 6/1 uku. 18
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Kuhani Mkuu Aliyemhukumu Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Kayafa Alikuwa Mpinzani Mkali wa Ibada ya Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Yesu Apelekwa kwa Anasi, Kisha kwa Kayafa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Apelekwa kwa Anasi, Kisha kwa Kayafa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 6/1 uku. 18

Je, Wajua?

Tunaweza kujifunza nini kumhusu mtume Petro kutokana na ukweli wa kwamba alikaa na mtengenezaji fulani wa ngozi kabla ya kuambiwa aende kwa Kornelio?

▪ Simulizi fulani katika kitabu cha Matendo linasema kwamba Petro alikaa “Yopa siku kadhaa pamoja na mtu fulani anayeitwa Simoni, mtengenezaji wa ngozi” aliyekuwa na “nyumba kando ya bahari.” (Matendo 9:43; 10:6) Wayahudi waliiona kazi ya mtengenezaji wa ngozi kuwa isiyo safi na yenye aibu. Kulingana Talmud (kitabu kuhusu dini ya Wayahudi) kazi ya mtengenezaji wa ngozi ilikuwa ya hali ya chini kuliko ya mkusanyaji wa kinyesi. Kazi ya Simoni ilimfanya aguse kwa ukawaida wanyama waliokufa, ikimaanisha kuwa yeye angekuwa asiye safi wakati wote. (Mambo ya Walawi 5:2; 11:39) Vyanzo vingine vya habari kuhusu kazi ya Simoni, vinasema kwamba huenda ikawa alitumia maji ya bahari katika kazi yake, na kwamba yaelekea jengo alimofanyia kazi lilikuwa nje ya mji, kwa sababu kazi ya kutengeneza ngozi ilitokeza “harufu mbaya sana.”

Ingawa hali ilikuwa hivyo, Petro alikubali kukaa na Simoni. Hilo linaonyesha kwamba kwa kumwiga Yesu ambaye hakuwa na ubaguzi, yaelekea Petro alikuwa amejifunza kupuuza ubaguzi wa Wayahudi kuelekea watu waliowaona kuwa wasio safi.—Mathayo 9:11; Luka 7:36-50.

Maneno ya Yesu “wewe mwenyewe umesema” yanamaanisha nini?

▪ Wakati alipoagizwa na Kayafa, kuhani mkuu wa Wayahudi, atangaze hadharani kama yeye ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, Yesu alimjibu: “Wewe mwenyewe umesema.” (Mathayo 26:63, 64) Alimaanisha nini?

Yesu hakuwa anajaribu kuepuka kumjibu Kayafa. Yaelekea maneno “wewe mwenyewe umesema” ulikuwa msemo wa Wayahudi wa kuthibitisha kwamba jambo lililosemwa ni la kweli. Kwa mfano, Talmud ya Palestina (Yerusalemu), kitabu kuhusu dini ya Wayahudi kilichoandikwa katika karne ya nne W.K., kinataja mwanamume Myahudi ambaye alipoulizwa kama rabi fulani amekufa, alijibu hivi: “Wewe umesema.” Maneno hayo yalieleweka kuwa uthibitisho kwamba rabi huyo alikuwa amekufa.

Yesu alitambua mamlaka ya kuhani mkuu ya kumweka chini ya kiapo ili aseme ukweli. Zaidi ya hayo, kukaa kimya kungemaanisha kuwa Yesu anakana kuwa yeye ndiye Kristo. Kwa hiyo jibu la Yesu: “Wewe mwenyewe umesema” lilionyesha kuwa Yesu alikubaliana na maneno ya kuhani huyo. Katika simulizi lingine kama hilo katika kitabu cha Marko, Kayafa alimuuliza Yesu moja kwa moja kama Yeye ndiye Masihi. Yesu alimjibu hivi kwa ujasiri: “Mimi ndiye.”—Marko 14:62; ona pia Mathayo 26:25 na Marko 15:2.

[Picha katika ukurasa wa 18]

Eneo la kutengenezea ngozi huko Fez, Morocco

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki