Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 11/1 kur. 30-31
  • Waokolewa Kutoka Kwenye Tanuru ya Moto!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Waokolewa Kutoka Kwenye Tanuru ya Moto!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Uharibifu wa Sodoma na Gomora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Waliopanga Njama ya Kuua Wauawa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Ashinda Vishawishi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Jinsi Paradiso Ilivyopotea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 11/1 kur. 30-31

Kwa Ajili ya Vijana

Waokolewa Kutoka Kwenye Tanuru ya Moto!

Maagizo: Fanya zoezi hili katika mazingira matulivu. Unaposoma maandiko, jiwazie ukiwa katika matukio yanayozungumziwa. Wazia kikao. Sikia sauti. Hisi kama wahusika wakuu wanavyohisi. Wazia kwamba masimulizi haya ni halisi kabisa.

Wahusika wakuu: Shadraki, Meshaki, Abednego, na Nebukadneza

Muhtasari: Imani ya vijana watatu Waebrania yajaribiwa.

1 CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA DANIELI 3:1-30.

Eleza sauti “ulizosikia” uliposoma mstari wa 3-7.

․․․․․

Eleza jinsi tanuru ya moto ilivyoonekana, kama unavyoiwazia.

․․․․․

Unatambua hisia gani katika sauti ya Nebukadneza anapoamuru tanuru itiwe moto mara saba kuliko ilivyokuwa kawaida? (Soma tena mstari wa 19 na 20.)

․․․․․

Eleza jinsi mwanamume wa nne katika tanuru anavyoonekana, kama unavyomwazia. (Soma tena mstari wa 24 na 25.)

․․․․․

Shadraki, Meshaki, na Abednego wanaonyesha sifa gani wanapozungumza na Nebukadneza kwenye mstari wa 16-18?

․․․․․

2 CHIMBA ZAIDI.

Ukitumia vifaa vya kufanyia utafiti unavyoweza kupata, chunguza urefu wa kipimo cha mkono mmoja, kisha ufanye hesabu ili kujua ukubwa wa sanamu ambayo Nebukadneza alitengeneza. (Soma tena mstari wa 1.)

․․․․․

Unaposoma mstari wa 19 na 20 na ulinganishe na mstari wa 28 na 29, Nebukadneza anaonekana kuwa mtu wa aina gani?

․․․․․

3 TUMIA MAMBO ULIYOJIFUNZA. ANDIKA MAMBO ULIYOJIFUNZA KUHUSU . . .

Kuwaheshimu wenye mamlaka.

․․․․․

Umuhimu wa kutetea imani yako.

․․․․․

Msaada wa Yehova wakati wa majaribu.

․․․․․

NJIA NYINGINE UNAYOWEZA KUTUMIA MAMBO HAYO.

Imani yako inaweza kujaribiwa ukiwa katika hali gani?

․․․․․

Simulizi kuhusu Shadraki, Meshaki, na Abednego litakusaidiaje kuendelea kuwa mwaminifu?

․․․․․

4 NI MAMBO GANI KATIKA SIMULIZI HILI AMBAYO YAMEKUGUSA MOYO SANA, NA KWA NINI?

․․․․

Ikiwa huna Biblia, waombe Mashahidi wa Yehova wakupe moja, au soma habari zaidi katika Intaneti www.watchtower.org

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki