Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w13 10/1 uku. 6
  • “Tumempata Masihi”!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Tumempata Masihi”!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Kristo Ni Nani?
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
  • Yesu Kristo Ni Nani?
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Walimngoja Masihi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Masihi! Njia ya Mungu ya Wokovu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
w13 10/1 uku. 6
[Picha katika ukurasa wa 6]

HABARI KUU | BIBLIA INA UJUMBE GANI?

“Tumempata Masihi”!

Miaka mia nne hivi baada ya kitabu cha mwisho cha maandiko ya Kiebrania katika Biblia kuandikwa, unabii wa Mika kumhusu Masihi ulitimia: Yesu alizaliwa katika mji wa Bethlehemu. Miaka 30 hivi baadaye, katika mwaka wa 29 W.K., sehemu ya kwanza ya unabii wa Danieli kuhusu Masihi aliyeahidiwa ilitimia. Yesu alibatizwa kisha Mungu akamtia mafuta kwa roho takatifu. Ule Uzao yaani Masihi aliyesubiriwa kwa muda mrefu, alifika kwa wakati barabara!

Mara moja Yesu alianza huduma yake “[aki]tangaza habari njema ya ufalme wa Mungu.” (Luka 8:1) Kama tu ilivyotabiriwa, Yesu alikuwa mwenye fadhili, mpole, na aliwajali watu kikweli. Aliwafundisha watu kwa sababu aliwapenda na mafundisho yake yaliwanufaisha. Pia, aliwaponya “kila namna ya udhaifu,” na hivyo akathibitisha Mungu alikuwa pamoja naye. (Mathayo 4:23) Watu wa kila umri walimwendea Yesu na kusema: “Tumempata Masihi”!​—Yohana 1:41.

Yesu alitabiri kwamba kabla Ufalme wake haujaanza kutawala dunia, kungetokea vita, matetemeko ya ardhi, na matatizo mengine mengi. Aliwasihi watu wote “[waendelee] kukesha.”​—Marko 13:37.

Yesu alikuwa mwanadamu mkamilifu aliyemtii Mungu, lakini alikuwa na maadui ambao hatimaye walimuua. Kupitia kifo chake tunaweza kuwa na tumaini la kupata uzima wa milele ambao Adamu na Hawa walipoteza.

Kifo cha Yesu kilitimiza unabii. Pia, Mungu alitimiza unabii alipomfufua Yesu akiwa kiumbe wa roho mwenye nguvu siku tatu baadaye. Kisha Yesu akawatokea zaidi ya wanafunzi wake 500. Kabla hajarudi mbinguni, Yesu aliwaamuru wafuasi wake watangazie “watu wa mataifa yote” habari njema kumhusu yeye na Ufalme wake. (Mathayo 28:19) Walitangaza habari njema kwa kadiri gani?

​—Habari hii inategemea Mathayo, Marko, Luka, Yohana, 1 Wakorintho.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki