Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w14 4/1 uku. 3
  • Kwa nini watu husali?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa nini watu husali?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Habari Zinazolingana
  • Mkaribie Mungu Kupitia Sala
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
  • Yesu Anatufundisha Kusali
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Kumkaribia Mungu Katika Sala
    Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • Zawadi ya Sala
    Biblia Inatufundisha Nini?
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
w14 4/1 uku. 3
Mvulana mdogo akisali

HABARI KUU | KWA NINI UNAPASWA KUSALI?

Kwa Nini Watu Husali?

Je, wewe husali kwa ukawaida? Watu wengi husali, hata wale wasioamini Mungu. Lakini kwa nini watu husali? Uchunguzi uliofanywa nchini Ufaransa unaonyesha kwamba nusu ya raia wa nchi hiyo husali au kutafakari nyakati fulani “ili tu wahisi vizuri.” Kama watu wengi barani Ulaya, hawasali ili kumwabudu Mungu. Badala yake, wanataka kupata “kitulizo kinachotokana na sala.” Kwa upande mwingine, baadhi ya waumini husali tu kwa Mungu wanapohitaji msaada, wakitazamia kwamba atajibu haraka maombi yao.​—Isaya 26:16.

Namna gani wewe? Je, unafikiri sala ni njia tu ya kutuliza mawazo? Kama unamwamini Mungu, je, umeona akijibu sala zako? Au, unahisi kwamba sala zako hazijibiwi? Biblia inaweza kukusaidia uone sala, si kama njia ya kukusaidia uhisi vizuri bali kama njia muhimu ya kumkaribia Mungu.

Watu wakisali: Mchezaji wa mpira baada ya kufunga bao, mwanamume na mkewe mgonjwa hospitalini, wanajeshi wakati wa vita
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki