Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp17 Na. 3 uku. 3
  • Wapanda Farasi Wanne​—Jinsi Wanavyokuhusu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wapanda Farasi Wanne​—Jinsi Wanavyokuhusu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Wapanda-Farasi wa Kifumbo wa Kitabu cha Ufunuo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Kulifumbua Fumbo la Wapanda-Farasi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Wapanda Farasi Wanne​—Jinsi Wanavyokuhusu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
wp17 Na. 3 uku. 3
Mbio za wapanda farasi wanne

HABARI KUU | WAPANDA FARASI WANNE​—JINSI WANAVYOKUHUSU

Wapanda Farasi Wanne—Jinsi Wanavyokuhusu

Wanakimbia kwa kishindo kikubwa! Wapanda farasi wanne na farasi zao hufanyiza picha iliyo wazi sana akilini ambayo huvuta uangalifu katika Biblia! Farasi wa kwanza ni mweupe, mpanda farasi wake ni mfalme mwenye utukufu aliyewekwa rasmi hivi karibuni. Anafuatwa na farasi wa rangi ya moto, na mpandaji wake anaondoa amani duniani kote. Farasi wa tatu ni mweusi kama giza, na aliyeketi juu yake amebeba mizani, ishara ya upungufu wa chakula. Farasi wa nne ni wa rangi ya kijivu, akiashiria magonjwa na mambo mengine yanayosababisha vifo, mpandaji wake ni Kifo chenyewe. Nalo Kaburi, linafuata kwa ukaribu, likivuna idadi kubwa ya watu!—Ufunuo 6:1-8.

“Mwanzoni niliogopa sana niliposoma simulizi la wapanda farasi wanne. Nilihisi kwamba Siku ya Hukumu iko karibu sana na singeokoka kwa sababu sikuwa nimejitayarisha.”—Crystal.

“Nilivutiwa sana na wapanda farasi hao wanne walioketi juu ya farasi wenye rangi tofauti-tofauti. Nilipojua maana ya maono hayo, nilielewa kwa nini wapanda farasi hao wanaelezwa kwa njia hiyo.”—Ed

Je, unahisi kama Crystal kuhusu wapanda farasi wanne wa Apokalipsi? Au una maoni kama ya Ed? Vyovyote vile, mbio za wapanda farasi wanne ndilo simulizi linalojulikana sana katika kitabu cha mwisho cha Biblia cha Ufunuo. Je, unajua kwamba utafaidika kwa kuelewa maono hayo? Jinsi gani? Mungu anaahidi kwamba unaweza kuwa na furaha ya kweli kwa kusoma, kujifunza na kuishi kupatana na mambo yaliyoandikwa katika kitabu hicho cha kinabii.—Ufunuo 1:1-3.

Ingawa baadhi ya watu huogopa maono hayo ya wapanda farasi wanne, hayakukusudiwa kukuogopesha. Kwa kupendeza, mamilioni ya watu wametambua kwamba maono hayo yanaimarisha imani na kuwapa tumaini zuri la wakati ujao. Inaweza kuwa hivyo kwako pia. Tafadhali chunguza makala inayofuata.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki