Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w17 Machi uku. 32
  • Jina la Kibiblia Katika Mtungi wa Kale

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jina la Kibiblia Katika Mtungi wa Kale
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Jina la Mungu
    Amkeni!—2017
  • Je! Jina Lenyewe Linapasa Kutumiwa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Jina la Mungu Katika Vizazi Vingi
    Jina la Mungu Litakaloendelea Milele
  • Jina la Mungu—Maana na Matumizi
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
w17 Machi uku. 32
Maandishi ya kale ya Wakanaani yaliyopatikana katika mtungi wa udongo uliotengenezwa miaka 3,000 iliyopita, yafunua jina la Kibiblia

Jina la Kibiblia Katika Mtungi wa Kale

Mtungi wa udongo uliotengenezwa miaka 3,000 iliyopita

Hivi karibuni, watafiti walipendezwa na vipande vya mtungi wa udongo uliotengenezwa miaka 3,000 iliyopita, vilivyochimbuliwa mwaka 2012. Ni nini kilichokuwa cha pekee sana kuhusu uvumbuzi huo? Si vipande vya mtungi huo, bali maandishi yaliyokuwa juu ya vipande hivyo.

Wavumbuzi wa vitu vya kale walipounganisha vipande hivyo, walifaulu kusoma maandishi hayo ya kale ya Wakanaani. Maandishi hayo yalikuwa: “Eshba’al Ben [mwana wa] Beda’.” Hiyo ndiyo mara ya kwanza kwa wavumbuzi kupata jina hilo katika maandishi ya kale.

Kwa kweli, Eshbaali mwingine anatajwa katika Biblia, na alikuwa kati ya wana wa Mfalme Sauli. (1 Nya. 8:33; 9:39) Profesa Yosef Garfinkel, ambaye alishiriki katika uvumbuzi huo anasema hivi: “Inapendeza kuona kwamba jina Eshba’al linapatikana katika Biblia, na sasa pia kwenye rekodi za wavumbuzi, wakati wa utawala wa Mfalme Daudi pekee.” Baadhi ya watu hufikiri kwamba jina hilo lilitumiwa katika kipindi hicho pekee. Kwa mara nyingine tena, habari fulani inayopatikana katika Biblia imethibitishwa na wavumbuzi.

Katika andiko lingine la Biblia, jina Eshbaali limeandikwa kuwa Ish-boshethi, “boshethi” likichukua mahali pa “baali.” (2 Sam. 2:10) Kwa nini? Watafiti wanaeleza hivi: “Katika Samweli cha Pili watu walisita kutumia jina Eshba’al, ambalo lilifanana na jina la mungu wa dhoruba wa Wakanaani Ba’al, lakini jina halisi . . . lilihifadhiwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki