Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w19 Januari uku. 31
  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Habari Zinazolingana
  • Nahodha James Cook—Mvinjari Hodari wa Pasifiki
    Amkeni!—1995
  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Washiriki Wapya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Washiriki Wapya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
w19 Januari uku. 31
Kenneth E. Cook, Jr., na Jamie, mke wake

Kenneth E. Cook, Jr., na Jamie, mke wake

Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza

JUMATANO asubuhi, Januari 24, 2018, washiriki wa familia ya Betheli ya Marekani na Kanada walifurahia kusikia tangazo hili la pekee: Ndugu Kenneth Cook, Jr., sasa ni mshiriki wa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova.

Ndugu Cook alizaliwa na kulelewa huko Pennsylvania, Marekani. Alijifunza kweli kutoka kwa mwanafunzi mwenzake muda mfupi kabla ya kuhitimu shule ya sekondari na alibatizwa Juni 7, 1980. Alianza utumishi wa wakati wote akiwa painia wa kawaida Septemba 1, 1982. Baada ya kufanya upainia kwa miaka miwili, alialikwa Betheli, ambapo alianza utumishi huo Oktoba 12, 1984, huko Wallkill, New York.

Kwa miaka 25 iliyofuata Ndugu Cook alishughulikia migawo mbalimbali kwenye kiwanda cha uchapishaji na pia kwenye Ofisi ya makao ya Betheli. Alifunga ndoa na Dada Jamie, mwaka wa 1996, kisha Jamie akajiunga naye katika utumishi wa Betheli huko Wallkill. Katika mwezi wa Desemba 2009, Ndugu na Dada Cook waliombwa wakatumikie katika Kituo cha Elimu cha Watchtower huko Patterson, New York, ambapo Ndugu Cook alipewa mgawo katika Idara ya Kushughulikia Maswali ya Wasomaji. Mwezi wa Aprili 2016, baada ya kurudi Wallkill kwa muda mfupi, Ndugu na Dada Cook walipewa mgawo wa kutumikia huko Brooklyn, New York. Miezi mitano baadaye, walihamia kwenye makao makuu mapya ya ulimwenguni pote huko Warwick, New York. Januari 2017, Ndugu Cook aliwekwa rasmi kuwa msaidizi wa Halmashauri ya Uandikaji ya Baraza Linaloongoza.

Sasa Baraza Linaloongoza lina ndugu wanane watiwa-mafuta:

K. E. Cook, Jr.; S. F. Herd; G. W. Jackson; M. S. Lett; G. Lösch; A. Morris III; D. M. Sanderson; D. H. Splane

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki