Ratiba ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi ya 1992
MAAGIZO
Wakati wa 1992, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango ya kuongozea Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], Kiongozi cha Shule ya Huduma ya Kitheokrasi [sg-SW], Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi [gt-SW], Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW], na Maswali Wanayouliza Vijana—Majibu Yafanyayo Kazi [yp-SW] vitakuwa msingi wa migawo.
Shule itaanza kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha, kisha itaendelea hivi:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma mwenye kustahili. Vichwa vya hotuba hii vitategemea habari katika kitabu “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” au Kiongozi cha Shule ya Huduma ya Kitheokrasi. Mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika sehemu hiyo. Lengo lapasa kuwa si kufanya mwenezo wa habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kundi yakikaziwa. Mahali inapohitajiwa, kichwa kimepasa kichaguliwe. Wote wanatiwa moyo wafanye matayarisho ya kimbele kwa uangalifu ili wanufaike kikamili na habari hiyo.
Ndugu waliogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa iwapo lazima.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Hii yapasa ishughulikiwe na mwangalizi wa shule au mzee mwingine anayestahili au na mtumishi wa huduma aliyepewa mgawo na mwangalizi wa shule. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliotolewa kuwa mgawo usomwe. Baada ya kutoa mwono mfupi wa ujumla wa sura zilizotolewa kuwa mgawo, saidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Chunguza matoleo ya Mnara wa Mlinzi upate habari zaidi za kukaziwa. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
HOTUBA NA. 2: Dakika 5. Hii ni kusoma Biblia juu ya habari iliyotolewa kuwa mgawo itakayotolewa na ndugu. Hii itakuwa hivyo katika shule kubwa na pia vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia, na hata katika mambo makuu ya katikati. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho na jinsi kanuni zinavyohusu, yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyotolewa kuwa mgawo yapasa isomwe kabisa.
HOTUBA NA. 3: Dakika 5. Hotuba hii watagawiwa dada. Vichwa vya hotuba hii vitategemea kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Wanafunzi waliogawiwa wapaswa wawe wanaweza kusoma. Wakati wa kutoa hotuba hii, mwanafunzi aweza kuwa ameketi au amesimama. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini wasaidizi wa ziada wanaweza kutumiwa. Ni afadhali vikao vihusishe utumishi wa shambani au utoaji wa ushahidi wa vivi hivi. Anayetoa hotuba aweza ama kuanzisha mazungumzo ili kuweka kikao au kuacha msaidizi (wasaidizi) wake afanye hivyo. Habari wala si kikao ndiyo ya kufikiriwa kwanza. Mwanafunzi apaswa kutumia kichwa kilichoonyeshwa.
HOTUBA NA. 4: Dakika 5. Igawiwe ndugu au dada. Vichwa vya hotuba hii vitapokezana zamu kati ya vitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko na Maswali Wanayouliza Vijana—Majibu Yafanyayo Kazi, hicho cha pili kitagawiwa hasa wanafunzi wachanga au walio wapya zaidi. Mwanafunzi aliyegawiwa apaswa awe anaweza kusoma. Inapogawiwa ndugu, yapaswa iwe hotuba inayotolewa kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi ndugu huyo atayarishe hotuba yake akiwa anafikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Hata hivyo, endapo habari hiyo yataka kikao cha aina nyingine ya wasikilizaji chenye kutumika na kinachofaa, ndugu huyo aweza kuchagua kusitawisha hotuba yake kwa njia hiyo. Mwanafunzi apaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
Inapogawiwa dada, habari hii yapasa itolewe kama ambavyo Hotuba Na. 3 imetolewa muhtasari.
SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila hotuba ya mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri hususa, si lazima afuate mpango wa shauri lenye kufuliza kama ilivyoandikwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala yake, anapaswa kukaza fikira juu ya sehemu zile ambazo mwanafunzi anahitaji kufanyia maendeleo. Ikiwa mhutubu-mwanafunzi anastahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri amepaswa atie duara kuzunguka sifa ya usemi ambayo mwanafunzi atafanyia kazi safari nyingine, afanye hivyo katika kisanduku ambamo kwa kawaida alama hizi “V” “M” au “T” zingewekwa. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89-SW) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale wanaotoa hotuba wamepaswa wakalie viti vya mbele karibu na jukwaa. Hiyo itaokoa wakati, na pia itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati unaporuhusu baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuelimisha na yanayofaa kutumiwa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo baada ya kila hotuba ya mwanafunzi. Ikiwa ule utoaji wa mambo makuu ya Biblia haukuridhisha, shauri la faragha laweza kutolewa.
KUTAYARISHA HOTUBA: Ndugu wanaotoa Mgawo Na. 1 wapaswa wachague kichwa inapohitajiwa. Wanafunzi waliogawiwa hotuba ya pili wapaswa kuchagua kichwa kitakachowezesha mwenezo unaofaa zaidi wa habari hiyo. Wanafunzi waliogawiwa hotuba ya tatu na ya nne wapaswa watumie kichwa kilichoonyeshwa. Kabla ya kutoa hotuba, ingefaa wanafunzi warudie kusoma habari ya Kiongozi cha Shule inayoshughulika na sifa ya usemi inayofanyiwa kazi.
KUFUATA WAKATI: Kusiwe hotuba ya kupita wakati uliowekwa. Wala shauri na maelezo ya mshauri. Hotuba Na. 2 hadi 4 zapasa zikatizwe kwa busara ikiwa wakati unakwisha. Aliyepewa mgawo wa kutoa “ishara ya kuacha” amepaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulikia Mgawo Na. 1 wanapopitisha wakati wamepaswa washauriwe kwa faragha. Wote wapaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Programu kwa jumla: Dakika 45, bila wimbo na sala.
PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi pitio la kuandika litatolewa. Katika kujitayarisha, pitia migawo ya habari na kukamilisha ratiba ya kusoma Biblia. Biblia pekee ndiyo ya kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atasoma majibu yote na kukaza fikira juu ya maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayafahamu majibu vizuri. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zafanya iwe lazima, pitio la kuandika laweza kutumiwa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa kwenye ratiba.
MAKUNDI MAKUBWA NA MADOGO: Makundi yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikishwa huenda yakataka kupanga vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine hotuba zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasio wakfu wanaoishi kupatana na kanuni za Kikristo wanaweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.
WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kundi wanaweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kujitahidi kuwapo kwenye kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa dhati. Mwanafunzi asipokuwapo wakati ameratibiwa, mtu mwingine anaweza kujitolea kuchukua mgawo huo, akionyesha matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule anaweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.
RATIBA
Jan. 6 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 1 hadi 4
Wimbo Na. 46
Na. 1: Utangulizi kwa Mambo ya Walawi—Sehemu 1 (si-SW kur. 25-6 maf. 1-5)
Na. 2: Mambo ya Walawi 1:1-13
Na. 3: Kutambua Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi (gt-SW utangu. maf. 1-4)
Na. 4: Sababu Biblia Ina Ukweli Kamili (rs-SW uku. 84 fu. 1)
Jan. 13 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 5 hadi 7
Wimbo Na. 205
Na. 1: Utangulizi kwa Mambo ya Walawi—Sehemu 2 (si-SW uku. 26 maf. 6-10)
Na. 2: Mambo ya Walawi 5:1-13
Na. 3: Je! Yesu Aliishi Kikweli? (gt-SW utangu. maf. 5-11)
Na. 4: Jinsi ya Kufanya Maksi za Shule Ziwe Nzuri (yp-SW sura 18)
Jan. 20 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 8 hadi 10
Wimbo Na. 111
Na. 1: sg-SW kur. 5-7 maf. 1-9
Na. 2: Mambo ya Walawi 10:1-11
Na. 3: Kwa Kweli, Yesu Alikuwa Nani? (gt-SW utangu. maf. 12-15)
Na. 4: Falsafa za Kibinadamu Zina Hitilafu Gani Tatu? (rs-SW uku. 84 fu. 2 hadi uku. 85 fu. 2)
Jan. 27 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 11 hadi 13
Wimbo Na. 224
Na. 1: sg-SW kur. 7-9 maf. 10-16
Na. 2: Mambo ya Walawi 11:1-12, 46, 47
Na. 3: Ni Nini Kilichomfanya Yesu Kuwa Mtu Mkuu Zaidi (gt-SW utangu. maf. 16-19)
Na. 4: Kuepuka Kuchokozwa Shuleni (yp-SW sura 19)
Feb. 3 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 14 na 15
Wimbo Na. 105
Na. 1: sg-SW kur. 9-11 maf. 1-12
Na. 2: Mambo ya Walawi 14:1-13
Na. 3: Kwa Nini Ujifunze Juu ya Yesu, na Tunavyoweza (gt-SW utangu. maf. 20-23)
Na. 4: Kujifunza Maisha ya Yesu Ni Ushuhuda wa Kufikiri Kuzuri (rs-SW uku. 85 maf. 3, 4)
Feb. 10 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 16 hadi 18
Wimbo Na. 180
Na. 1: sg-SW kur. 12-13 maf. 13-20
Na. 2: Mambo ya Walawi 16:1-14
Na. 3: Gabrieli Atokea Zekaria na Mariamu (gt-SW sura 1)
Na. 4: Kusikilizana na Mwalimu Wako (yp-SW sura 20)
Feb. 17 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 19 hadi 21
Wimbo Na. 170
Na. 1: sg-SW kur. 14-17 maf. 1-10
Na. 2: Mambo ya Walawi 19:1-15
Na. 3: Yesu Aheshimiwa Kabla ya Kuzaliwa (gt-SW sura 2)
Na. 4: Mungu Huona Hekima ya Kibinadamu Kuwa Upumbavu (rs-SW uku. 86 maf. 1, 2)
Feb. 24 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 22 hadi 24
Wimbo Na. 64
Na. 1: Mambo ya Walawi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 1 (si-SW kur. 28-9 maf. 28-35)
Na. 2: Mambo ya Walawi 23:1-14
Na. 3: Kuzaliwa kwa Yohana (gt-SW sura 3)
Na. 4: Jinsi ya Kupata na Kudumisha Kazi (yp-SW sura 21)
Mac. 2 Kusoma Biblia: Mambo ya Walawi 25 hadi 27
Wimbo Na. 7
Na. 1: Mambo ya Walawi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 2 (si-SW kur. 29-30 maf. 36-39)
Na. 2: Mambo ya Walawi 25:1-12
Na. 3: Yusufu Amwoa Mariamu Mwenye Mimba (gt-SW sura 4)
Na. 4: Mungu Husikia Sala za Nani? (rs-SW uku. 276 fu. 1 hadi uku. 277 fu. 1)
Mac. 9 Kusoma Biblia: Hesabu 1 hadi 3
Wimbo Na. 172
Na. 1: Utangulizi kwa Hesabu—Sehemu 1 (si-SW kur. 30-1 maf. 1-6)
Na. 2: Hesabu 3:38-51
Na. 3: Kuzaliwa kwa Yesu—Wapi na Wakati Gani? (gt-SW sura 5)
Na. 4: Chagua Kazi-Maisha Iliyo Bora Zaidi (yp-SW sura 22)
Mac. 16 Kusoma Biblia: Hesabu 4 hadi 6
Wimbo Na. 128
Na. 1: Utangulizi kwa Hesabu—Sehemu 2 (si-SW uku. 31 maf. 7-10)
Na. 2: Hesabu 6:1-12
Na. 3: Mtoto wa Ahadi (gt-SW sura 6)
Na. 4: Ni Nini Hufanya Baadhi ya Sala Kutokubalika (rs-SW uku. 277 fu. 2 hadi uku. 278 fu. 1)
Mac. 23 Kusoma Biblia: Hesabu 7 hadi 9
Wimbo Na. 106
Na. 1: sg-SW kur. 17-19 maf. 11-17
Na. 2: Hesabu 8:14-26
Na. 3: Yesu na Wanajimu (gt-SW sura 7)
Na. 4: Sababu Ngono Kabla ya Ndoa Ni Kosa (yp-SW sura 23)
Mac. 30 Kusoma Biblia: Hesabu 10 hadi 12
Wimbo Na. 45
Na. 1: sg-SW kur. 19-21 maf. 1-9
Na. 2: Hesabu 12:1-16
Na. 3: Kumkimbia Mtawala Mkatili (gt-SW sura 8)
Na. 4: Mambo Ambayo Yafaa Kusali Juu Yayo (rs-SW uku. 278 maf. 2-9)
Apr. 6 Kusoma Biblia: Hesabu 13 hadi 15
Wimbo Na. 124
Na. 1: sg-SW kur. 21-4 maf. 10-20
Na. 2: Hesabu 14:1-12
Na. 3: Maisha ya Mapema ya Familia ya Yesu (gt-SW sura 9)
Na. 4: Jinsi ya Kuepuka Ukosefu wa Adili za Kingono (yp-SW sura 24)
Apr. 13 Kusoma Biblia: Hesabu 16 hadi 19
Wimbo Na. 151
Na. 1: sg-SW kur. 24-6 maf. 1-11
Na. 2: Hesabu 17:1-13
Na. 3: Katika Yerusalemu Akiwa na Miaka 12 (gt-SW sura 10)
Na. 4: Jinsi ya Kushughulika na Ombi la Mwenye Nyumba juu ya Sala (rs-SW uku. 279 maf. 1, 2)
Apr. 20 Kusoma Biblia: Hesabu 20 hadi 22
Wimbo Na. 138
Na. 1: sg-SW kur. 27-9 maf. 12-20
Na. 2: Hesabu 20:1-13
Na. 3: Yohana Atayarisha Njia kwa Ajili ya Yesu (gt-SW sura 11)
Na. 4: Je! Kupiga Punyeto Ni Kosa Zito? (yp-SW sura 25)
Apr. 27 Pitio la Kuandika. Kamilisha Mambo ya Walawi 1 hadi Hesabu 22
Wimbo Na. 217
Mei 4 Kusoma Biblia: Hesabu 23 hadi 26
Wimbo Na. 112
Na. 1: sg-SW kur. 29-31 maf. 1-7
Na. 2: Hesabu 25:1-13
Na. 3: Kinachotukia Anapobatizwa Yesu (gt-SW sura 12)
Na. 4: Ni Baadhi ya Unabii Gani Unaongojea Kutimizwa Katika Wakati Ujao Ulio Karibu? (rs-SW uku. 362 maf. 2-6)
Mei 11 Kusoma Biblia: Hesabu 27 hadi 30
Wimbo Na. 132
Na. 1: sg-SW kur. 31-3 maf. 8-15
Na. 2: Hesabu 30:1-16
Na. 3: Kujifunza Kutokana na Vishawishi vya Yesu (gt-SW sura 13)
Na. 4: Kuepuka Mtego wa Kupiga Punyeto (yp-SW sura 26)
Mei 18 Kusoma Biblia: Hesabu 31 na 32
Wimbo Na. 222
Na. 1: Hesabu—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 1 (si-SW kur. 34-5 maf. 32-34)
Na. 2: Hesabu 31:1-12
Na. 3: Wanafunzi wa Kwanza wa Yesu (gt-SW sura 14)
Na. 4: Ni Upi Baadhi ya Unabii Mbalimbali wa Baada ya Har–Magedoni? (rs-SW uku. 363 maf. 1-4)
Mei 25 Kusoma Biblia: Hesabu 33 hadi 36
Wimbo Na. 160
Na. 1: Hesabu—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 2 (si-SW uku. 35 maf. 35-38)
Na. 2: Hesabu 35:9-25
Na. 3: Mwujiza wa Kwanza wa Yesu (gt-SW sura 15)
Na. 4: Sababu Haki Ndiyo Sera Bora Zaidi (yp-SW sura 27)
Juni 1 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 1 hadi 3
Wimbo Na. 187
Na. 1: Utangulizi kwa Kumbukumbu la Torati—Sehemu 1 (si-SW uku. 36 maf. 1-6)
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 1:29-46
Na. 3: Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Yehova (gt-SW sura 16)
Na. 4: Sababu Wakristo Wapendezwa na Unabii Mbalimbali (rs-SW uku. 363 fu. 5 hadi uku. 364 fu. 3)
Juni 8 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 4 hadi 6
Wimbo Na. 91
Na. 1: Utangulizi kwa Kumbukumbu la Torati—Sehemu 2 (si-SW uku. 37 maf. 7-9)
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 5:6-22
Na. 3: Kumfundisha Nikodemo (gt-SW sura 17)
Na. 4: Kushinda Upendo wa Kupumbazwa (yp-SW sura 28)
Juni 15 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 7 hadi 10
Wimbo Na. 162
Na. 1: sg-SW kur. 33-5 maf. 1-9
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 7:1-11
Na. 3: Yohana Apungua, Yesu Azidi (gt-SW sura 18)
Na. 4: Fundisho la Tohara (Purgatori) na Ambayo Maandiko Husema (rs-SW uku. 316 fu. 1 hadi uku. 317 fu. 6)
Juni 22 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 11 hadi 14
Wimbo Na. 206
Na. 1: sg-SW kur. 36-8 maf. 10-17
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 13:1-11
Na. 3: Kufundisha Mwanamke Msamaria (gt-SW sura 19 maf. 1-14)
Na. 4: Jinsi ya Kujua Ikiwa Mtu Yu Tayari Kufanya Urafiki na Mtu wa Jinsia Tofauti (yp-SW sura 29 kur. 225-31, 234-5)
Juni 29 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 15 hadi 19
Wimbo Na. 150
Na. 1: sg-SW kur. 39-41 maf. 1-11
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 18:9-22
Na. 3: Sababu Wasamaria Wengi Waamini (gt-SW sura 19 maf. 15-21)
Na. 4: Jamii Mbalimbali za Watu Zilitoka Wapi? (rs-SW uku. 95 maf. 1-3)
Julai 6 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 20 hadi 23
Wimbo Na. 79
Na. 1: sg-SW kur. 41-3 maf. 12-18
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 23:9-25
Na. 3: Mwujiza wa Pili Anapokuwa Kana (gt-SW sura 20)
Na. 4: Urafiki Pamoja na Jinsia Tofauti—Je! Kuna Hatari? (yp-SW sura 29 kur. 232-3)
Julai 13 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 24 hadi 27
Wimbo Na. 59
Na. 1: sg-SW kur. 44-6 maf. 1-8
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 24:10-22
Na. 3: Yesu Ahubiri Katika Mji wa Kwao (gt-SW sura 21)
Na. 4: Kaini Alitoa Wapi Mke Wake? (rs-SW uku. 95 fu. 4 hadi uku. 96 fu. 3)
Julai 20 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 28 hadi 30
Wimbo Na. 175
Na. 1: sg-SW kur. 46-8 maf. 9-20
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 30:8-20
Na. 3: Wanafunzi Wanne Waitwa (gt-SW sura 22)
Na. 4: Kujua Uko Tayari kwa Ajili ya Ndoa (yp-SW sura 30)
Julai 27 Kusoma Biblia: Kumbukumbu la Torati 31 hadi 34
Wimbo Na. 41
Na. 1: Kumbukumbu la Torati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 40-1 maf. 30-34)
Na. 2: Kumbukumbu la Torati 32:1-14
Na. 3: Miujiza Zaidi Katika Kapernaumu (gt-SW sura 23)
Na. 4: Tofauti za Kijamii na Itikadi Kwamba Weusi Wamelaaniwa (rs-SW uku. 96 fu. 4 hadi uku. 97 fu. 2)
Ago. 3 Kusoma Biblia: Yoshua 1 hadi 5
Wimbo Na. 40
Na. 1: Utangulizi kwa Yoshua (si-SW uku. 42 maf. 1-5)
Na. 2: Yoshua 1:1-11
Na. 3: Sababu Iliyomfanya Yesu Aje Duniani (gt-SW sura 24)
Na. 4: Kutambua Upendo Halisi (yp-SW sura 31 kur. 242-7, 250-1)
Ago. 10 Kusoma Biblia: Yoshua 6 hadi 9
Wimbo Na. 18
Na. 1: sg-SW kur. 49-51 maf. 1-8
Na. 2: Yoshua 6:12-27
Na. 3: Huruma kwa Mwenye Ukoma (gt-SW sura 25)
Na. 4: Je! Wanadamu Wote Ni Watoto wa Mungu? (rs-SW uku. 98 fu. 1-5)
Ago. 17 Kusoma Biblia: Yoshua 10 hadi 13
Wimbo Na. 213
Na. 1: sg-SW kur. 51-3 maf. 9-18
Na. 2: Yoshua 10:1-14
Na. 3: Yesu Asamehe Dhambi na Kuponya (gt-SW sura 26)
Na. 4: Kupona Moyo Uliovunjika (yp-SW sura 31 kur. 248-9)
Ago. 24 Kusoma Biblia: Yoshua 14 hadi 17
Wimbo Na. 50
Na. 1: sg-SW kur. 54-6 maf. 1-8
Na. 2: Yoshua 14:1-14
Na. 3: Mathayo Aitwa na Afanya Karamu (gt-SW sura 27)
Na. 4: Wakati Jamii Zote Zitakapounganishwa (rs-SW uku. 99 maf. 1-4)
Ago. 31 Pitio la Kuandika. Kamilisha Hesabu 23 hadi Yoshua 17
Wimbo Na. 42
Sept. 7 Kusoma Biblia: Yoshua 18 hadi 20
Wimbo Na. 204
Na. 1: sg-SW kur. 56-8 maf. 9-16
Na. 2: Yoshua 20:1-9
Na. 3: Aulizwa Maswali Juu ya Kufunga (gt-SW sura 28)
Na. 4: Jinsi ya Kufanikisha Utafutaji wa Mapenzi (yp-SW sura 32)
Sept. 14 Kusoma Biblia: Yoshua 21 hadi 24
Wimbo Na. 131
Na. 1: Yoshua—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 45-6 maf. 21-24)
Na. 2: Yoshua 24:1-15
Na. 3: Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato (gt-SW sura 29)
Na. 4: Kifo cha Yesu Kilikuwa cha Kipekee (rs-SW uku. 346 fu. 3 hadi uku. 347 fu. 2)
Sept. 21 Kusoma Biblia: Waamuzi 1 hadi 4
Wimbo Na. 26
Na. 1: Utangulizi kwa Waamuzi (si-SW kur. 46-7 maf. 1-7)
Na. 2: Waamuzi 2:8-23
Na. 3: Yesu Ajibu Washtaki Wake (gt-SW sura 30)
Na. 4: Hatari za Unywaji wa Matineja (yp-SW sura 33)
Sept. 28 Kusoma Biblia: Waamuzi 5 hadi 7
Wimbo Na. 150
Na. 1: sg-SW kur. 58-61 maf. 1-12
Na. 2: Waamuzi 7:7-22
Na. 3: Je! Ni Halali Kuvunja Suke la Nafaka Siku ya Sabato? (gt-SW sura 31)
Na. 4: Kwa Nini Uhai wa Milele Wategemea Ukombozi? (rs-SW uku. 347 maf. 3-5)
Okt. 5 Kusoma Biblia: Waamuzi 8 hadi 10
Wimbo Na. 207
Na. 1: sg-SW kur. 61-3 maf. 13-18
Na. 2: Waamuzi 8:13-28
Na. 3: Ni Jambo Gani Lililo Halali Siku ya Sabato? (gt-SW sura 32)
Na. 4: Sababu Uepuke Madawa ya Kulevya (yp-SW sura 34)
Okt. 12 Kusoma Biblia: Waamuzi 11 hadi 14
Wimbo Na. 144
Na. 1: sg-SW kur. 63-6 maf. 1-10
Na. 2: Waamuzi 11:28-40
Na. 3: Kutimiza Unabii wa Isaya (gt-SW sura 33)
Na. 4: Ni Kwa Nini Wazao wa Adamu Hutaabishwa na Dhambi Zake? (rs-SW uku. 348 fu. 1 hadi uku. 349 fu. 1)
Okt. 19 Kusoma Biblia: Waamuzi 15 hadi 18
Wimbo Na. 191
Na. 1: sg-SW kur. 66-9 maf. 11-22
Na. 2: Waamuzi 16:18-31
Na. 3: Kuchagua Mitume Wake (gt-SW sura 34)
Na. 4: Uwe Mteuzi Katika Unayosoma (yp-SW sura 35)
Okt. 26 Kusoma Biblia: Waamuzi 19 hadi 21
Wimbo Na. 11
Na. 1: Waamuzi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 50 maf. 26-28)
Na. 2: Waamuzi 21:8-25
Na. 3: Mahubiri Yenye Sifa Zaidi ya Yote Yaliyopata Kutolewa (gt-SW sura 35 maf. 1-6)
Na. 4: Ni Nani Wanaonufaika Kwanza na Ukombozi? (rs-SW uku. 349 maf. 2, 3)
Nov. 2 Kusoma Biblia: Ruthu 1 hadi 4
Wimbo Na. 57
Na. 1: Ruthu: Utangulizi na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 51-3 maf. 1-3, 9, 10)
Na. 2: Ruthu 1:7-22
Na. 3: Ni Nani Wenye Furaha Kikweli? (gt-SW sura 35 maf. 7-17)
Na. 4: Dhibiti Utazamaji Wako wa TV (yp-SW sura 36)
Nov. 9 Kusoma Biblia: 1 Samweli 1 hadi 3
Wimbo Na. 127
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Samweli (si-SW kur. 53-4 maf. 1-6)
Na. 2: 1 Samweli 3:2-18
Na. 3: Kiwango cha Juu kwa Wafuasi Wake (gt-SW sura 35 maf. 18-27)
Na. 4: “Kondoo Wengine” Wanufaika na Ukombozi (rs-SW uku. 349 fu. 4 hadi uku. 350 fu. 2)
Nov. 16 Kusoma Biblia: 1 Samweli 4 hadi 7
Wimbo Na. 45
Na. 1: sg-SW kur. 69-71 maf. 1-8
Na. 2: 1 Samweli 7:1-14
Na. 3: Sala, na Kumtumaini Mungu (gt-SW sura 35 maf. 28-37)
Na. 4: Maoni Yaliyosawazika Juu ya Tafrija (yp-SW sura 37)
Nov. 23 Kusoma Biblia: 1 Samweli 8 hadi 11
Wimbo Na. 222
Na. 1: sg-SW kur. 72-3 maf. 9-13
Na. 2: 1 Samweli 11:1-15
Na. 3: Njia ya Uhai (gt-SW sura 35 maf. 38-49)
Na. 4: Ni Baraka Zipi za Wakati Ujao Zitakazofurahiwa kwa Sababu ya Ukombozi? (rs-SW uku. 350 fu. 3 hadi uku. 351 fu. 2)
Nov. 30 Kusoma Biblia: 1 Samweli 12 hadi 14
Wimbo Na. 156
Na. 1: sg-SW kur. 73-5 maf. 1-8
Na. 2: 1 Samweli 13:1-14
Na. 3: Imani Kubwa ya Ofisa wa Jeshi (gt-SW sura 36)
Na. 4: Ambayo Wakati Ujao Umeweka Akibani (yp-SW sura 38)
Des. 7 Kusoma Biblia: 1 Samweli 15 hadi 17
Wimbo Na. 86
Na. 1: sg-SW kur. 75-8 maf. 9-17
Na. 2: 1 Samweli 15:5-23
Na. 3: Yesu Aondolea Mbali Huzuni ya Mjane (gt-SW sura 37)
Na. 4: Mungu Ameonyeshaje Upendo Wake Kwetu, Nasi Twaweza Kunufaikaje? (rs-SW uku. 351 maf. 3-6)
Des. 14 Kusoma Biblia: 1 Samweli 18 hadi 20
Wimbo Na. 140
Na. 1: sg-SW kur. 78-80 maf. 1-10
Na. 2: 1 Samweli 18:1-16
Na. 3: Je! Yohana Alikosa Imani? (gt-SW sura 38)
Na. 4: Jinsi ya Kukaribia Mungu (yp-SW sura 39)
Des. 21 Kusoma Biblia: 1 Samweli 21 hadi 24
Wimbo Na. 138
Na. 1: sg-SW kur. 80-4 maf. 11-24
Na. 2: 1 Samweli 23:13-29
Na. 3: Wenye Kiburi na Wenye Udhalili (gt-SW sura 39)
Na. 4: Ukombozi Wapaswa Uwe na Tokeo Gani Maishani Mwetu? (rs-SW uku. 352 maf. 1-3)
Des. 28 Pitio la Kuandika. Kamilisha Yoshua 18 hadi 1 Samweli 24
Wimbo Na. 155