Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 24
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Daudi amwacha hai Sauli (1-22)

        • Daudi amheshimu mtiwa-mafuta wa Yehova (6)

1 Samweli 24:1

Marejeo

  • +1Sa 23:28, 29

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/1/1989, kur. 16-17

1 Samweli 24:2

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Igeni Imani Yao, makala 3

1 Samweli 24:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “afunike miguu yake.”

Marejeo

  • +Zb 57:utangulizi; 142:utangulizi

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    11/1/1989, uku. 16

1 Samweli 24:4

Marejeo

  • +1Sa 26:8, 23

1 Samweli 24:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “dhamiri ya Daudi ikaendelea kumchoma.”

Marejeo

  • +2Sa 24:10

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Dumu Katika Upendo wa Mungu, uku. 18

    Mnara wa Mlinzi,

    10/15/2007, uku. 22

  • Fahirishi ya Machapisho

    w07 10/15 22

1 Samweli 24:6

Marejeo

  • +Kut 22:28; 1Sa 26:11; 2Sa 1:14; 1Nya 16:22

1 Samweli 24:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “akawatawanya.”

1 Samweli 24:8

Marejeo

  • +1Sa 26:17

1 Samweli 24:9

Marejeo

  • +1Sa 26:19

1 Samweli 24:10

Marejeo

  • +1Sa 24:4
  • +1Sa 9:16; 10:1; 26:9; Zb 105:15

1 Samweli 24:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kuiua nafsi yangu.”

Marejeo

  • +1Sa 26:18; Zb 35:7
  • +1Sa 23:14

1 Samweli 24:12

Marejeo

  • +1Sa 26:23
  • +Kum 32:35
  • +1Sa 26:11

1 Samweli 24:14

Marejeo

  • +1Sa 26:20

1 Samweli 24:15

Marejeo

  • +1Sa 25:39; Zb 35:1

1 Samweli 24:16

Marejeo

  • +1Sa 26:17

1 Samweli 24:17

Marejeo

  • +1Sa 26:21

1 Samweli 24:18

Marejeo

  • +1Sa 24:4, 10

1 Samweli 24:19

Marejeo

  • +1Sa 26:25; Zb 18:20

1 Samweli 24:20

Marejeo

  • +1Sa 13:14; 15:28; 18:8; 20:31; 23:17

1 Samweli 24:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yangu.”

Marejeo

  • +Law 19:12; Kum 6:13
  • +2Sa 9:1; 21:7

1 Samweli 24:22

Marejeo

  • +1Sa 15:34
  • +1Sa 23:29

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

1 Sam. 24:11Sa 23:28, 29
1 Sam. 24:3Zb 57:utangulizi; 142:utangulizi
1 Sam. 24:41Sa 26:8, 23
1 Sam. 24:52Sa 24:10
1 Sam. 24:6Kut 22:28; 1Sa 26:11; 2Sa 1:14; 1Nya 16:22
1 Sam. 24:81Sa 26:17
1 Sam. 24:91Sa 26:19
1 Sam. 24:101Sa 24:4
1 Sam. 24:101Sa 9:16; 10:1; 26:9; Zb 105:15
1 Sam. 24:111Sa 26:18; Zb 35:7
1 Sam. 24:111Sa 23:14
1 Sam. 24:121Sa 26:23
1 Sam. 24:12Kum 32:35
1 Sam. 24:121Sa 26:11
1 Sam. 24:141Sa 26:20
1 Sam. 24:151Sa 25:39; Zb 35:1
1 Sam. 24:161Sa 26:17
1 Sam. 24:171Sa 26:21
1 Sam. 24:181Sa 24:4, 10
1 Sam. 24:191Sa 26:25; Zb 18:20
1 Sam. 24:201Sa 13:14; 15:28; 18:8; 20:31; 23:17
1 Sam. 24:21Law 19:12; Kum 6:13
1 Sam. 24:212Sa 9:1; 21:7
1 Sam. 24:221Sa 15:34
1 Sam. 24:221Sa 23:29
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
1 Samweli 24:1-22

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

24 Mara tu Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa hivi: “Tazama! Daudi yuko katika nyika ya En-gedi.”+

2 Basi Sauli akachukua wanaume 3,000 mashujaa kutoka nchi yote ya Israeli na kwenda kumtafuta Daudi na wanaume wake kwenye miamba ya mbuzi wa milimani. 3 Sauli akafika kwenye mazizi ya kondoo yaliyojengwa kwa mawe kando ya barabara, mahali ambapo palikuwa na pango, akaingia pangoni kwenda haja,* wakati huo Daudi na wanaume wake walikuwa wameketi ndani kabisa ya pango hilo.+ 4 Wanaume wa Daudi wakamwambia: “Hii ndiyo siku ambayo Yehova anakwambia, ‘Tazama! Ninamtia adui yako mikononi mwako,+ nawe unaweza kumtendea jambo lolote unalotaka.’” Kwa hiyo Daudi akasimama, akakata kimyakimya upindo wa joho la Sauli lisilo na mikono. 5 Lakini baadaye moyo wa Daudi ukaendelea kumchoma*+ kwa sababu alikuwa amekata upindo wa joho la Sauli lisilo na mikono. 6 Akawaambia wanaume wake: “Siwezi kamwe kuwazia, kulingana na maoni ya Yehova, kumtendea jambo kama hilo bwana wangu, mtiwa-mafuta wa Yehova, kwa kuinua mkono wangu dhidi yake, kwa kuwa yeye ni mtiwa-mafuta wa Yehova.”+ 7 Basi Daudi akawazuia* wanaume wake kwa maneno hayo, naye hakuwaruhusu wamshambulie Sauli. Sauli akaondoka pangoni na kwenda zake.

8 Baadaye Daudi akainuka na kutoka pangoni, akamwita Sauli: “Bwana wangu mfalme!”+ Sauli alipoangalia nyuma, Daudi aliinama hadi chini kifudifudi na kusujudu. 9 Daudi akamuuliza Sauli: “Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wanaosema, ‘Tazama! Daudi anataka kukudhuru’?+ 10 Siku hii ya leo umeona kwa macho yako mwenyewe jinsi Yehova alivyokutia mikononi mwangu pangoni. Lakini mtu fulani aliposema nikuue,+ nilikusikitikia nikasema, ‘Sitainua mkono wangu dhidi ya bwana wangu, kwa maana yeye ni mtiwa-mafuta wa Yehova.’+ 11 Tazama baba yangu, angalia nimeshika upindo wa joho lako lisilo na mikono; kwa sababu nilipokata upindo wa joho lako lisilo na mikono, sikukuua. Sasa unaweza kuona na kuelewa kwamba sikusudii kukudhuru wala kukuasi, nami sijakutendea dhambi,+ lakini wewe unaniwinda ili kuniua.*+ 12 Yehova na ahukumu kati yangu na wewe,+ na Yehova anilipizie kisasi mambo unayonitendea,+ lakini sitainua mkono wangu dhidi yako.+ 13 Kama methali ya kale inavyosema, ‘Kutoka kwa mwovu hutoka uovu,’ lakini sitainua mkono wangu dhidi yako. 14 Mfalme wa Israeli ametoka kumtafuta nani? Unamfuatia nani? Mbwa aliyekufa? Kiroboto mmoja?+ 15 Yehova na awe mwamuzi, atahukumu kati yangu na wewe, naye ataona na kunitetea na kuamua kesi yangu+ na kuniokoa kutoka mikononi mwako.”

16 Mara tu Daudi alipomaliza kumwambia maneno hayo, Sauli akasema: “Je, hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?”+ Kisha Sauli akaanza kulia kwa sauti kubwa. 17 Akamwambia Daudi: “Wewe ni mwadilifu kuliko mimi, kwa maana umenitendea mema lakini mimi nimekulipa kwa uovu.+ 18 Naam, leo umeniambia mema uliyotenda kwa kukosa kuniua Yehova aliponitia mikononi mwako.+ 19 Ni mtu gani anayempata adui yake na kumwacha aende zake bila kumdhuru? Yehova atakuthawabisha wewe kwa mema+ kwa sababu ya mambo uliyonifanyia leo. 20 Sasa tazama! Najua kwa hakika kwamba utatawala ukiwa mfalme+ na kwamba ufalme wa Israeli utadumu mikononi mwako. 21 Sasa niapie mbele za Yehova+ kwamba hutawafagilia mbali wazao wangu* baada yangu na kwamba hutalifutilia mbali jina langu kutoka katika nyumba ya baba yangu.”+ 22 Kwa hiyo Daudi akamwapia Sauli, kisha Sauli akaenda nyumbani kwake.+ Lakini Daudi na wanaume wake wakapanda kwenda ndani ya ngome.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki