Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pitio vitabu vimefungwa la habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Septemba 2 hadi Desemba 23, 1991. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Angalia: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. New World Translation ndiyo tafsiri ya kwanza kurudisha jina la Kimungu katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo. [si uku. 327 fu. 2]
2. Silinda ya Koreshi hujulisha sera ya Mfalme Koreshi ya kurejesha kwenye sehemu zao za awali vikundi vya watu vilivyotekwa. [si uku. 336 fu. 15]
3. Musa alikubaliwa kuwa mwandikaji wa Pentateuki si na Wayahudi tu bali pia na waandikaji wengine wa kale, ambao baadhi yao walikuwa maadui wa Wayahudi. [si uku. 338 fu. 5]
4. Kwa wazi Shekemu alimlala Dina kinguvu. (Mwa. 34:1-3) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w85 6/5 uku. 31.]
5. Simulizi katika Mwanzo 38:8-10 linalosimulia kwamba Onani alimwaga chini akapoteza bure shahawa zake hupinga utumizi wa vizuia mimba. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w73 uku. 255 (au w74-SW uku. 48).]
6. Ijapokuwa Yuda hakutenda kwa unyoofu kwa kuwa na uhusiano wa kingono na mwanamke aliyemfikiria kuwa malaya, hata hivyo yeye hakuvunja amri hususa ya sheria ya Mungu. (Mwa. 38:11-18) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w73 uku. 384.]
7. Kwa kufaa Mashahidi wa Yehova husimama, husujudu, au hata kulala kifudi-fudi mbele ya mtawala kwa kuheshimu na kustahi cheo chake ikiwa hiyo ni desturi ya nchi hiyo. (Mwa. 44:14) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w74 uku. 62.]
8. Baada ya Musa kugeuza maji yote ya Misri kuwa damu, makuhani Wamisri waliiga tendo hilo kuu na pengine walitumia maji kutoka kwa kisima kufanya tendo lao la kimizungu. (Kut. 7:19-24) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w83 10/15 uku. 30 (au w84-SW 8/1 uku. 21).]
9. Ile nuru ya Shekina ilionekana ndani ya Patakatifu Zaidi pa Tabenakulo (hema) na hekalu la Sulemani. (Linganisha Kutoka 25:21, 22.) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w66 uku. 543.]
10. “Madhara zaidi [aksidenti yenye kutokeza kifo, NW] inahusu mama peke yake. (Kut. 21:23) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w77 kur. 479-80.]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Tafsiri nyingi za Biblia zina kasoro nyingi zipi? [si uku. 324 fu. 17]
12. Matokeo yanakuwa nini wakati watafsiri wa Biblia wanapoachia mbali tafsiri halisi kwa ajili ya kile wanachofikiria kuwa fahari ya lugha na umbo? [si uku. 326 fu. 34]
13. Ni jinsi gani New World Translation ni yenye upatano katika tafsiri zayo za maneno? [si uku. 328 fu. 7]
14. Ni nini ambacho kwa kutokeza huonyesha uasilia wa Biblia? [si uku. 342 fu. 25]
15. Kwa nini Raheli alikuwa na nia ya kumpa Lea fursa ya kuchukua mimba kwa kubadilishana na matunda ya tunguja, kama kinavyosimulia Mwanzo 30:14, 15? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w67 uku. 320.]
16. Mwanzo 39:9 huonyeshaje kwamba kufundisha watoto Neno la Mungu kutawanufaisha baadaye maishani? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w73 uku. 556 mafu. 17, 18. (au w74-SW uku. 127 mafu. 17, 18).]
17. Kwa nini Mungu alimwagiza Musa amwombe Farao ruhusa wafunge safari ya siku tatu kwenda jangwani, hali alikusudia Waisraeli waondoke Misri kabisa? (Kut. 3:18) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w82 1/1 uku. 31.]
18. Je! mtu kuwa na jina lake katika ‘kitabu cha uzima’ cha Mungu humpa uhakikisho wa uhai wa milele? (Kut. 32:32, 33) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w87-SW 9/1 uku. 29.]
19. Tunaweza kuelezaje kwamba “BWANA [Yehova, NW] alisema na Musa uso kwa uso”? (Kut. 33:11) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w70 uku. 320.]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha taarifa zifuatazo:
20. Mojawapo sababu za ukosefu wa usahihi katika kutafsiri namna ya vitenzi vya Kiebrania ni nadharia ya kisarufi iitwayo leo. [si uku. 330 fu. 14]
21. Kufikia 1989 New World Translation ilikuwa imetokea katika lugha kukiwa nakala zaidi ya zilizochapwa. [si uku. 331 fu. 21]
22. Kulingana na mwakiolojia mmoja, chanzo ambacho kutoka hapo lugha zote zilienea palikuwa. [si uku 339 fu. 13]
23. Msingi pekee wa talaka kukiwa na haki ya kufunga ndoa upya ni. [pe-SW sura ya 29 fu. 28]
24. Jina Shilo lamaanisha kiunabii lilielekeza kwa. (Mwa. 49:10) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona re-SW kur. 83-4.]
25. Lile agano husaidia katika kufanyiza “ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.” (Kut. 19:6) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w89-SW 2/1 kur. 18-19.]
Chagua jibu sahihi katika taarifa zifuatazo:
26. Mavumbuzi ya kiakiolojia kwenye Gihoni huenda yakapatana na maandishi ya Biblia ya (Mnara wa Babeli; ule mtaro wa maji kwenye Jiji la Daudi; uvamizi wa Shishaki juu ya Yuda). [si uku. 332 fu. 4]
27. (Ile Nusu Duara ya Tito; maandishi ya Pontio Pilato; Areopago) ungali uko Athene, kuthibitisha kikao cha Matendo 17:16-34. [si uku. 336 fu. 19]
28. Utafiti wa tiba wa kisasa unaonyesha kwamba hasira yaweza kuathiri mkazo wa damu na kutokeza hisia za moyoni, maumivu ya kichwa, kutokwa damu puani, kizunguzungu, na kutoweza kutamka maneno hupatana na (Mithali 14:30; Ayubu 19:20; Zaburi 12:3). [si uku. 340 fu. 15]
29. Ule Usemi “kati ya jioni mbili,” hurejezea wakati wa kuanzia (mchana katikati mpaka kushuka kwa jua; jioni ya siku moja ya kalenda mpaka nyingine). (Kut. 12:6, NW) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w73 uku. 175 (au w90-SW 2/15 uku. 14 mafu. 21, 22).]
30. Ni nini kinachoelezwa kwenye Hesabu 40:34 kuwa (ushuhuda wa kwamba Yehova alionyesha kibali juu ya hema [tabanakulo, NW]; kikumbusha cha kwamba Yehova alikuwa asiyeonekana; ishara ya nyakati zenye huzuni za wakati ujao). [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona hs uku. 71 fu. 30.]
Linganisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Kut. 14:21; Kum. 23:9-14; 2 Fal. 3:4, 5; Zab. 19:7-10; Zab. 77:11, 12
31. Lile Jiwe la Moabi huthibitisha simulizi hili la Biblia [si uku. 333 fu. 6]
32. Ushauri wa Biblia juu ya usafi wa kiafya unathibitishwa na tiba. [si uku. 340 fu. 17]
33. Daudi alionyesha uthamini wake wa kutoka moyoni kwa hekima ya Mungu. [si uku. 350 fu. 7]
34. Ili kunufaishwa na Maandiko, ni lazima sisi tutafakari daima juu ya Neno la Mungu [si uku. 351 fu. 12]
35. Ijapokuwa kuna maelezo mengi yenye kusifika yanayotolewa, hakika hiki ni kisa cha kujiingiza kwa kimungu badala ya kuwa namna fulani ya ajabu kuu ya kiasili. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w81 8/15 uku. 18.]