Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/92 uku. 7
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1992
Huduma Yetu ya Ufalme—1992
km 8/92 uku. 7

Matangazo

◼ Toleo la fasihi kwa Agosti: Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Septemba: Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? au ikiwa hakipatikani, kitabu Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani au Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia vinaweza kutumiwa. Oktoba: Uandikishaji wa Amkeni! au Mnara wa Mlinzi au yote mawili. Maandikisho yanaweza kufanywa kwa mwaka mmoja au miezi sita. Hakuna mpango wa maandikisho ya miezi mitatu. Maandikisho ya miaka mingi mfululizo hayatakubaliwa. Novemba: Biblia New World Translation pamoja na kitabu Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu? ANGALIA: Makundi ambayo bado hayajaagiza vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa yafanye hivyo kwenye Fomu ya Agizo la Vitabu (S-14-SW) ya mwezi utakaofuata.

◼ Wote wanaoshirikiana na kundi wapaswa wafanye upya maandikisho yao ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kupitia kwa kundi.

◼ Sosaiti haitakuwa tena ikishughulikia maagizo ya fasihi yanayofanywa na mhubiri mmoja mmoja. Wale wanaotaka kifaa fulani wanaweza kumwarifu mtumishi wa vitabu, ambaye atakitia ndani bila kukawia katika agizo la vitabu la kundi la kila mwezi.

◼ Makundi yanapaswa yaanze kuagiza kalenda za 1993 pamoja na agizo lao la fasihi la Septemba. Kalenda zitapatikana katika Kiingereza na Kifaransa.

◼ Kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 2, Sosaiti itafanya hesabu ya fasihi yote iliyo akibani katika Betheli. Kwa sababu ya kuhesabu huko, hakuna maagizo ya fasihi ya kundi yatakayoshughulikiwa ili kupelekwa au kuchukuliwa wakati wa siku hizo.

◼ Kila kundi litapokea fomu tatu za Orodha ya Vitabu na lapasa kuhesabu kihalisi fasihi ya kampeni. Tafadhali jazeni fomu hizo kikamili, na kupeleka ya awali kwetu, si baada ya Septemba 6, 1992. Tunzeni nakala ya kaboni katika faili zenu. Twawapelekea nakala ya tatu iwe nakala ya kufanyia kazi.

◼ Ugavi wa kutosha wa fomu kwa ajili ya utumizi katika mwaka wa utumishi wa 1993 unapelekwa kwa kila kundi. Fomu hizo hazipaswi kutumiwa ovyoovyo. Zapaswa zitumiwe kwa kusudi lazo pekee.

◼ Maombi ya mikopo kwa ajili ya Majumba ya Ufalme yatapitia kwa mwangalizi wa mzunguko ambaye atayapeleka kwa Sosaiti pamoja na mapendekezo yake.

◼ Tafadhali fanyeni marekebisho yafuatayo katika kitabu Kutoa Sababu:

Kwenye ukurasa 116, fungu la 2, mstari wa saba usomeke hivi: “. . . waende mbinguni kabla ya dhiki kubwa, sivyo? Badala yake, huenda likaonyesha kwamba baadhi yao, pamoja na washiriki katika mnofu wataokoka dhiki kubwa hiyo duniani.)”

Kwenye ukurasa 245, fungu la 4, mstari wa kwanza usomeke hivi: “. . . Kaini alimwoa mmoja wa dada zake (Mwa. 4:17; 5:4), au yawezekana mpwa wa kike, na kwamba Abramu . . . ”

◼ Vichapo Vipya Vinavyopatikana:

Kimasai: Biblia. Kiswahili: Jitihada ya Ainabinadamu ya Kutafuta Mungu.

◼ Vichapo Vinavyotazamiwa Karibuni:

Kiingereza: Mabuku ya Mnara wa Mlinzi ya 1980-1982. Kiswahili: “All Scripture Is Inspired of God and Beneficial”; Kitabu-Mwaka cha Mashahidi wa Yehova 1992.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki