Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Septemba 7 hadi Desemba 21, 1992. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Angalia: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Ni bora zaidi kukariri hotuba moyoni ili usitumie muhtasari yoyote ya habari. [sg-SW uku. 62. fu. 17]
2. Ili kufanyia maendeleo hali ya sauti yako, inafaa usikilize sauti yako mwenyewe katika utepe. [sg-SW uku. 64 fu. 3]
3. Hatuhitaji kuwa wenye busara tunapoongea na washiriki wa familia wasioamini. [sg-SW uku. 72 fu. 12]
4. Utumizi wa maulizo ya maoni ni wenye faida sana katika kufikia moyo wa mtu. [sg-SW uku. 76 fu. 10]
5. Kwa kukaa katika mji wa makimbilio, mwuaji asiye wa kukusudia angekaziwa uzito wa jambo alilokuwa amefanya na pia rehema ya Yehova katika kumruhusu akimbilie huko. (Yos. 20:6) [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w73 uku. 304 au w73-SW uku. 516.]
6. Kama ilivyofafanuliwa katika ule usimulizi kwenye Waamuzi 6:37-39, Gideoni alikuwa mwenye nadhari kupita kiasi. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w88-SW 4/1 uku. 30.]
7. Ingawa Manoa hakumwona Mungu kikweli, alihisi kwamba alikuwa amemwona kwa sababu alikuwa ameona mnenaji wa Mungu wa kimalaika aliyejivika mwili. (Amu. 13:22) [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w88-SW 5/15 uku. 23.]
8. Samweli na wanawe kwa kawaida hawahesabiwi kati ya waamuzi waliotumika baada ya Yoshua. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w86-SW 6/1 p. 31.]
9. Ingawa hakuwa kuhani, Samweli alitenda ifaavyo kwa kutoa dhabihu, kama ilivyorekodiwa kwenye 1 Samweli 10:8. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w71 uku. 478.]
10. Kwa kumpa Daudi mavazi yake, upanga wake, upinde wake, na mshipi wake, Yonathani alionyesha utambuzi na ujitiisho kwa Daudi akiwa mtu aliyepakwa mafuta kuwa mfalme. (1 Sam. 18:3, 4) [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 1/1 uku. 24 fu. 4.]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Kwa nini kwa kufaa Yehova aliamuru waabudu wa Baali wafutiliwe mbali? [si uku. 47 fu. 7 (chapa ya 1983 uku. 47 fu. 8)]
12. Usemi wa bila kutazamia una faida gani mbili? [sg-SW kur. 59-60 maf. 5-7]
13. Busara yaweza kuelezwaje? [sg-SW uku. 69 fu. 2]
14. Tunapowafundisha wengine, kwa nini tujitahidi kufanya zaidi ya kuwasilisha maarifa tu? [sg-SW uku. 75 maf. 7, 8]
15. Zaidi ya kusema, ni nini linalotiwa katika kuongea? [sg-SW uku. 79 fu. 3]
16. Maongezi ya kikundi yakiacha kuwa yenye kujenga, sisi binafsi twaweza kufanya nini juu yake? [sg-SW uku. 83 fu. 22]
17. Kulingana na Waamuzi 4:4, je, Debora aweza kuonwa kuwa mmoja wa waamuzi wa Israeli ya kale? Eleza. [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 6/1 uku. 31.]
18. Kwa nini Samsoni alikwenda mahali pa kahaba katika mji wa Gaza katika Filistia? (Amu. 16:1) [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w79 2/15 uku. 31 au w79-SW 11/1 uku. 24.]
19. Kwa nini Yehova ‘alijuta kwa sababu ya kumtawaza Sauli awe mfalme’? (1 Sam. 15:10, 11) [Usomaji Biblia kila juma; ona pia g77 3/22 uku. 28.]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila ya taarifa zifuatazo:
20. Matukio yanayozidi nguvu za kibinadamu yasiyo ya kawaida yaliyoandikwa kwenye Yoshua 10:10-14 ni vikumbusho vyenye nguvu vya . [si uku. 45 fu. 23 (uku. 46 fu. 23)]
21. Kwa kawaida kinywa cha mtu chapaswa kiwe kadiri ya inchi kutoka kwa kikuza-sauti. [sg-SW uku. 68 fu. 19]
22. Kwa msaada wa roho ya Yehova, twaweza kuwa wenye nguvu kiroho kama alivyokuwa kimwili tukisali kwa Yehova na kumwegemea. [si uku. 50 fu. 27 (uku. 50 fu. 28)]
23. Kitabu cha Ruthu hukazia kusudi la Yehova la kutokeza . [si uku. 51 fu. 1 (uku. 51 fu. 1)]
24. Habari kwenye Waamuzi 19:15 husimulia kisa cha ajabu cha Waisraeli kukosa kuonyesha wa kawaida. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w75 uku. 359 au w76-SW uku. 138.]
25. Sheria la Mungu kuhusu haiwezi kupuuzwa katika nyakati za tukio la dharura. (1 Sam. 14:31-34) [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w86-SW 9/1 uku. 25.]
Chagua jibu sahihi katika kila ya taarifa zifuatazo:
26. Waamuzi kilimalizwa kuandikwa (c. (karibu) 1090; c. 1100; 1078) K.W.K. [si uku. 46 fu. 3 na sanduku (uku. 46 fu. 3)]
27. (Ruthu; Rahabu; Debora) aliacha bara la kwao ili afuatie ibada ya Yehova na alijithibitisha kuwa mshikamanifu na mtiifu na mfanya kazi mwenye nia. [si uku. 52 fu. 9 (uku. 52 fu. 9)]
28. Katika mwaka (917; 1017; 1117) K.W.K., kulitokea badiliko kubwa katika tengenezo la kitaifa la Israeli. [si uku. 53 fu. 1 (uku. 53 fu. 1)]
29. Waandikaji wa 1 Samweli walikuwa (Samweli; Gadi; Nathani; Daudi; Sauli). [si uku. 53 fu. 2 (uku. 53 fu. 2)]
30. Mtu mmoja aliyewaheshimu washiriki wa familia yake zaidi ya Mungu alikuwa (Manoah; Eli; Sauli). (1 Sam. 2:29, 30) [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w87-SW 12/15 uku. 16 fu. 8.]
Linganisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Yos. 22:9-31; Amu. 8:23; Rut. 2:9; 1 Sam. 21:13-15; Efe. 5:3, 4
31. Neno la Mungu linatuongoza juu ya namna ya msemo wa kuepuka katika maisha ya kila siku. [sg-SW uku. 56 fu. 9]
32. Yehova hapendezwi na kusumbuliwa-sumbuliwa kwa wanawake kuhusiana na ngono. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w87-SW 3/15 uku. 5.]
33. Tunapokabiliwa na matatizo, Yehova anatazamia sisi tutumie uwezo wetu wa akili wala si kumtazamia tu atufanyie kila kitu. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w87-SW 4/15 uku. 19 fu. 14.]
34. Wanadamu wasio wakamilifu wanapaswa wapinge sana kishawishi cha kutumia vibaya uwezo. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w86-SW 8/15 uku. 11 fu. 13.]
35. Utambuzi utatusaidia tuepuke kuwekea vitendo vya wengine makusudio mabaya. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w86 11/1 uku. 23 fu. 10.]