Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/93 kur. 5-6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1993
Huduma Yetu ya Ufalme—1993
km 12/93 kur. 5-6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Septemba 6 hadi Desemba 20, 1993. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kitabu cha Ezra chahusu maandishi ya shughuli za Yehova pamoja na Wayahudi hadi kufikia wakati wa kukusanywa kwa orodha ya vitabu vya Kiebrania. [si-SW uku. 86 fu. 7]

2. Hapo awali vitabu vya Ezra na Nehemia vilikuwa kitabu kimoja, kilichoitwa Ezra. [si-SW uku. 88 fu. 3]

3. Unapotoa hotuba, ni vema kutozidisha mno shauku yako katika hotuba yako yote. [sg-SW uku. 164 fu. 6]

4. Mistari ya kufunga ya kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati yathibitisha kwamba miaka 70 kamili lazima ihesabiwe tangu ukiwa kamili wa Yuda hadi kurejeshwa kwa ibada safi katika 537 K.W.K. [si-SW uku. 84 fu. 35]

5. Kutoa maelezo kwa kawaida penye mikutano kutakusaidia uzoee kuhutubu mbele ya kikundi fulani. [sg-SW uku. 183 fu. 14]

6. “Mwanamke wa wana wa Dani” alikuwa ameolewa pia na mwanamume wa kabila la Dani. (2 Nya. 2:14) [Usomaji Biblia kila juma; ona w80-SW 1/1, uku. 24 au w79-E 4/15 uku. 31.]

7. Mambo ya Nyakati cha Pili 16:14 huonyesha kwamba maiti ya Mfalme Asa ilichomwa. [Usomaji Biblia kila juma; ona w76-E uku. 416.]

8. Katika Luka 11:51, ni wazi Yesu alikuwa akitaja juu ya kupigwa mawe kwa Zekaria mwana wa Yehoyada. (2 Nya. 24:20, 21) [Usomaji Biblia kila juma; ona w81-SW 12/15 uku. 6 au w80-E 3/1 uku. 31.]

9. Ikitukia wowote kati ya Mashahidi wa Yehova wakosa Ukumbusho, apaswa kuadhimisha siku 30 baadaye. (2 Nya. 30:2) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w85-SW 3/1 uku. 23 au w85-E 2/15 uku. 31.]

10. Wayahudi waliofukuzwa walikalishwa tena bara katika la nyumbani kwao kufikia “mwezi wa saba,” au kama Oktoba 1, 537 K.W.K. (Ezra 3:1) [Usomaji Biblia kila juma; ona si-SW uku. 283 fu. 29.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Ufuataji wa wakati wa hotuba kwa msingi wategemea nini? [sg-SW uku. 179 fu. 25]

12. Ni hekalu gani linalozidi mahekalu ya kidunia kuwa utukufu? [si-SW uku. 87 fu. 16]

13. Ubadilifu wa sauti ni nini? [sg-SW uku. 160 fu. 11]

14. Kwa nini ni lazima utumizi wa mfano udhihirishwe? [sg-SW uku. 169 fu. 10]

15. Ikiwa msemaji azidi wakati, huenda hili likawa na matokeo gani juu ya mwisho wake? [sg-SW uku. 177 fu. 16]

16. Kwa sababu gani si vibaya kurekodi katika utepe sala zinazotolewa hadharani? (2 Nya. 33:18) [Usomaji Biblia kila juma; ona w78-SW 5/1 uku. 23-24 au w78-E 1/1 uku. 32.]

17. Historia ya ulimwengu hutoa jina gani kwa Asenapari? (Ezra 4:10, NW) [Usomaji Biblia kila juma; ona w88-SW 2/15 uku. 28.]

18. Kwa nini watoto wa wake wageni walifukuzwa pamoja na mama zao? (Ezra 10:3, 44) [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 1/15 uku. 9.]

19. Ni mwaka gani uliokuwa “mwaka wa ishirini wa Artashasta”? (Neh. 2:1) [Usomaji Biblia kila juma; ona w92-SW 10/1 uku. 11.]

20. ‘Maana ya Torati ilielezwaje’? (Neh. 8:8) [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 26.]

21. Iweje kuhusu mfano wowote unaotumiwa katika hotuba? [sg-SW uku. 171 fu. 20]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

22. Baada ya kutekwa kwenda Babuloni, baki jaminifu la Wayahudi lilisimamisha madhabahu na kutoa dhabihu katika mwaka _________________________ . [si-SW uku. 85 fu. 3]

23. Ikiwa msemaji ana uchangamshi kuelekea wasikilizaji wake, unapaswa kuonekana katika _________________________ wake. [sg-SW uku. 166 fu. 13]

24. Ikiwa twatumia maneno ya kitheokrasi katika huduma yetu, ni muhimu kwamba _________________________ . [sg-SW uku. 173 fu. 5]

25. Kusudi kuu katika mwisho wa hotuba ni _________________________ . [sg-SW uku. 175 fu. 4]

26. Msemaji hapaswi _________________________ kinara cha msemaji. [sg-SW uku. 185 fu. 26]

27. Kulingana na 1 Timotheo 3:1, ndugu waweza kujifanya wenyewe wapatikane kwa _________________________ . [sg-SW uku. 190 fu. 10]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

28. Ezra alimaliza Mambo ya Nyakati (karibu 515; karibu 460; karibu 537) K.W.K. [si-SW uku. 79 fu. 1]

29. Nehemia alitumikia wakati wa utawala wa mfalme Mwajemi (Sairasi; Shasta; Artashasta). [si-SW uku. 88 fu. 1]

30. “Sikukuu” yarejezea Sikukuu ya (Vibanda; Majuma; Mkate Usiotiwa Chachu). (2 Nya. 7:8) [Usomaji Biblia kila juma; ona pm-E uku. 53.]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

2 Nya. 9:9; 2 Nya. 19:7; 2 Nya. 28:16, 20, 21; 2 Nya. 36:20, 21; Neh. 5:7

31. Mapatano yasiyo ya lazima na ulimwengu waweza kuleta msiba. [Usomaji Biblia kila juma; ona w85-SW 9/1 uku. 31.]

32. Kuhusu maoni yafaayo kuelekea hongo, Yehova mwenyewe huweka kiwango. [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 10/1 uku. 30.]

33. Jambo hilo lilikuwa ni kuvunja sheria ya Yehova katika Mambo ya Walawi 25:36 na Kumbukumbu la Torati 23:19 kwa njia ya moja kwa moja. [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 21.]

34. Hilo husema juu ya zawadi yenye thamani izidiyo dola 50,000,000. [Usomaji Biblia kila juma; ona g88-SW 11/8 uku. 4 au g87-E 11/22 uku. 4.]

35. Moja kati ya sababu zilizofanya Waisraeli watekwe kupelekwa Babuloni kwa miaka 70 ni kuvunjwa kwa sheria za Sabato ya Mungu. [Usomaji Biblia kila juma; ona g80-SW 7/8 uku. 7-8 au g79-E 9/22 uku. 9.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki