Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 9/94 uku. 3
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1994
Huduma Yetu ya Ufalme—1994
km 9/94 uku. 3

Matangazo

◼ Fasihi itakayotumiwa wakati wa Septemba: Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Oktoba: Uandikishaji wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Novemba: New World Translation of the Holy Scriptures pamoja na kitabu Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu? Desemba: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. TAARIFA: Makutaniko ambayo bado hayajaagiza vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa kufanya hivyo kwenye Agizo la Fasihi (S-14-SW) lao la kila mwezi litakalofuata. Tafadhali agizeni magazeti ya ziada yanayohitajiwa kwa ajili ya ugawaji wa Oktoba.

◼ Mwangalizi-msimamizi au mtu yeyote aliyewekwa naye apaswa kukagua hesabu ya kutaniko katika Septemba 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo. Tangazieni kutaniko jambo hili lifanywapo.

◼ Wahubiri wanaopanga kufanya upainia msaidizi katika Oktoba wanapaswa kutoa ombi lao mapema. Hilo litaruhusu wazee kufanya mipango ya lazima kwa ajili ya fasihi na eneo.

◼ Wazee wanakumbushwa kufuatia maagizo yaliyotolewa kwenye kurasa 21-3 za Mnara wa Mlinzi la Aprili 15, 1991, kuhusu watu wowote waliotengwa na ushirika au waliojitenga na ushirika ambao huenda wana mwelekeo wa kurudi.

◼ Kuanzia Januari 1, 1994, toleo la mara moja kwa mwezi la Mnara wa Mlinzi katika lugha ya Kiajemi limekuwa likipatikana. Nakala za kugawanya na maandikisho ya kibinafsi yanaweza kuagizwa na makutaniko.

◼ Toleo la mara moja kwa mwezi la Mnara wa Mlinzi katika lugha ya Kikambodia linachapishwa kuanzia Septemba 1, 1994. Nakala za kugawanya na maandikisho ya kibinafsi yanaweza kuagizwa na makutaniko.

◼ Kuanzia toleo la Julai 8, 1994, gazeti la Amkeni! la Kichina limekuwa likipatikana mara mbili kwa mwezi sawa na Kiingereza.

◼ Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika Kichina (Sahili) yanafanywa yapatikane katika nchi zote. Mnara wa Mlinzi unachapwa kwa rangi kamili. Magazeti hayo yanapatikana mara mbili kwa mwezi na yatakuwa sawa na ya Kiingereza. Nakala za kugawanya na maandikisho ya kibinafsi yanaweza kuagizwa na makutaniko.

◼ Kuanzia Julai 1994, toleo la mara moja kwa mwezi la Mnara wa Mlinzi katika lugha ya Kigeorgia limekuwa likipatikana kwa njia ya posta.

◼ Orodha ya Bei imetayarishwa kwa nchi fulani na nakala nne zinapelekwa kwenye kila kutaniko. Zapaswa kugawanywa kwa mwandishi na ndugu wanaoshughulikia fasihi, magazeti, na hesabu.

◼ Tuna ugavi wa Kuyachunguza Maandiko Kila Siku ya miaka ya 1993 na 1994 katika lugha ya Kiswahili. Hivi vyaweza kutumiwa kuwa badala au kwa wahubiri wapya wasiobatizwa au watu wenye kupendezwa. Maagizo yaweza kupelekwa pamoja na Agizo la Fasihi litakalofuata la kutaniko. Hivi ni vifaa vya kuagizwa kipekee.

◼ Vichapo Vipya Vinavyopatikana:

Kiarabu: Apply Yourself to Reading and Writing. Kihindi: Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia. Kiingereza: Watch Tower Publications Index 1991-1993. Punjabi: Je! Ulimwengu Huu Utaokoka? (Trakti Na. 19); Faraja kwa Walioshuka Moyo (Trakti Na. 20); Furahia Maisha ya Familia (Trakti Na. 21); Ni Nani Hasa Anayeutawala Ulimwengu? (Trakti Na. 22).

◼ Kaseti Mpya Zinazopatikana:

Kiingereza: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi (seti ya tepe nane katika kiwekeo).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki