Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/94 kur. 3-6
  • Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1995

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1995
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1994
  • Vichwa vidogo
  • MAAGIZO
  • RATIBA
Huduma Yetu ya Ufalme—1994
km 10/94 kur. 3-6

Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1995

MAAGIZO

Wakati wa 1995, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango ya kuongozea Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.

VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli [uw-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” [si-SW], Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi [gt-SW], na “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation [*td] au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [td-SW] vitakuwa msingi wa migawo.

Shule itaanza kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha kisha itaendelea hivi:

MGAWO NA. 1: Dakika 15. Hotuba hii yapasa ishughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma, na itategemea habari katika kitabu Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika kichapo hicho. Lengo lapasa kuwa si kutoa habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, kwa kukazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa kinapasa kitumiwe. Wote wanatiwa moyo wafanye matayarisho ya kimbele kwa uangalifu ili wanufaike kikamili na habari hiyo.

Ndugu waliogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa lazima au ikiwa msemaji ameomba shauri hilo kimbele.

MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Hii yapasa ishughulikiwe na mwangalizi wa shule au na mzee mwingine au mtumishi wa huduma atakayeonyesha kwa matokeo jinsi habari hiyo inavyohusu mahitaji ya mahali hapo. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Tumia sekunde 30 hadi 60 tu kupitia kwa ujumla. Lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wafahamu ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.

HOTUBA NA. 2: Dakika 5. Hii ni kusoma Biblia juu ya habari iliyotolewa kuwa mgawo itakayotolewa na ndugu. Itakuwa hivyo katika shule kubwa na pia vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo mafupi katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho na matumizi ya kanuni, yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyotolewa kuwa mgawo yapasa hasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa isomwe haifuatani mfululizo, mwanafunzi anaweza kutaja mstari mahali ambapo usomaji waendelea.

HOTUBA NA. 3: Dakika 5. Hotuba hii watagawiwa akina dada. Vichwa vya hotuba hii vitategemea kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi au “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation [*td] au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [td-SW]. Mwanafunzi aliyegawiwa apaswa awe anaweza kusoma. Wakati wa kutoa hotuba hii, mwanafunzi aweza kuwa ameketi au amesimama. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini wasaidizi wa ziada wanaweza kutumiwa. Akina dada wanaogawiwa hotuba hii watahitaji kutengeneza kichwa na habari itakayoshughulikiwa kwa kikao chenye kutumika, hasa kile kinachohusu utumishi wa shambani au ushahidi wa vivi hivi. Uangalifu mwingi wapaswa kuwekwa kwa matumizi ya habari yenye matokeo badala ya kikao.

HOTUBA NA. 4: Dakika 5. Igawiwe ndugu au dada. Itategemea “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia. Inapogawiwa ndugu, yapaswa iwe hotuba inayotolewa kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi ndugu huyo atayarishe hotuba yake akiwa anafikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Inapogawiwa dada, habari hii yapasa itolewe kama ilivyoonyeshwa katika Hotuba Na. 3.

SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila hotuba ya mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri hususa, si lazima afuate mfuatano wa mashauri kama yalivyoorodheshwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala yake, anapaswa kukaza fikira juu ya sehemu zile ambazo mwanafunzi anahitaji kufanyia maendeleo. Ikiwa mhutubu-mwanafunzi anastahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri apaswa kutia duara inayozunguka sifa ya usemi ambayo mwanafunzi atafanyia kazi safari nyingine, afanye hivyo katika kisanduku ambamo kwa kawaida alama hizi “V,” “M,” au “T” zingewekwa. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89-SW) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale wanaotoa hotuba wamepaswa wakalie viti vya mbele karibu na jukwaa. Hiyo itaokoa wakati na pia itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati unaporuhusu baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuelimisha na yanayofaa kutumiwa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo mengine mafupi baada ya kila hotuba ya mwanafunzi. Ikiwa utoaji wa mambo makuu ya Biblia haukuridhisha, shauri la faragha laweza kutolewa.

KUTAYARISHA HOTUBA: Kabla ya kutayarisha mgawo wa hotuba, mwanafunzi anapaswa kusoma kwa uangalifu habari ya Kiongozi cha Shule inayoshughulikia sifa ya usemi ipasayo kufanyiwa kazi. Wanafunzi waliogawiwa hotuba ya pili wanaweza kuchagua kichwa kinachofaa sehemu ya Biblia inayopasa isomwe. Hotuba nyingine zitatayarishwa kulingana na kichwa kilichoonyeshwa kwenye ratiba iliyochapishwa.

KUFUATA WAKATI: Haipasi hotuba, wala shauri na maelezo ya mshauri kupita wakati uliowekwa. Hotuba Na. 2 hadi 4 zapasa zikatizwe kwa busara wakati unapokwisha. Aliyepewa mgawo wa kutoa ishara ya kukatisha hotuba amepaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulikia Mgawo Na. 1 na mambo makuu ya Biblia wanapopitisha wakati wamepaswa washauriwe kwa faragha. Wote wapaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Programu yote: Dakika 45, bila kutia wimbo na sala.

PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi pitio la kuandika litatolewa. Katika kujitayarisha, pitia migawo ya habari, na kukamilisha ratiba ya kusoma Biblia. Biblia pekee ndiyo inayoweza kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atapitia majibu ya maswali ya pitio pamoja na wasikilizaji na kukaza fikira juu ya maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayafahamu majibu vizuri. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zafanya iwe lazima, pitio la kuandika laweza kufanywa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa kwenye ratiba.

MAKUTANIKO MAKUBWA: Makutaniko yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikishwa huenda yakataka kupanga vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine hotuba zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasiobatizwa wanaoishi kupatana na kanuni za Kikristo wanaweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.

WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kutaniko wanaweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kujitahidi kuwapo kwenye kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa kudhamiria. Mwanafunzi asipokuwapo wakati ameratibiwa, mtu mwingine anaweza kujitolea kuchukua mgawo huo, akionyesha matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au mwangalizi wa shule anaweza kuzungumzia habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.

RATIBA

*td – “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation au td-SW—Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia

Jan. 2 Kusoma Biblia: Zaburi 119:113-176

Wimbo Na. 127

Na. 1: Kuutambulisha Mkutano Mkubwa (uw-SW kur. 103-4 maf. 1-4)

Na. 2: Zaburi 119:161-176

Na. 3: Sababu ya Yesu Kuitwa “Mtu Huyu” (gt-SW sura 123)

Na. 4: *td 32A au td-SW 13A Mwanadamu Hajaandikiwa Yatakayompata

Jan. 9 Kusoma Biblia: Zaburi 120 hadi 130

Wimbo Na. 26

Na. 1: Tabia Ambazo Ni Lazima Kondoo Wengine Wadhihirishe (uw-SW uku. 105 fu. 5)

Na. 2: Zaburi 122:1–123:4

Na. 3: Sababu ya Pilato Kumhofu Yesu (gt-SW sura 124)

Na. 4: *td 33A au td-SW 44A Uhai wa Yesu wa Kibinadamu Ulikuwa Ukombozi Kwa Ajili ya Wote

Jan. 16 Kusoma Biblia: Zaburi 131 hadi 136

Wimbo Na. 129

Na. 1: Sababu Inayofanya Mkutano Mkubwa Uokoke Dhiki Kubwa (uw-SW kur. 106-9 maf. 6-13)

Na. 2: Zaburi 132:1-18

Na. 3: Mathibitisho ya Upendo wa Yesu Kwa Jamii ya Kibinadamu (gt-SW sura 125)

Na. 4: *td 33B au td-SW 44B Kwa Nini Yesu Aliweza Kulipa Ukombozi

Jan. 23 Kusoma Biblia: Zaburi 137 hadi 140

Wimbo Na. 205

Na. 1: Sababu ya Kuwapo kwa Warithi wa Ufalme Wachache Sana Duniani Leo (uw-SW kur. 110-12 maf. 1-7)

Na. 2: Zaburi 137:1–138:8

Na. 3: Jinsi Yesu Alivyokuwa Kielelezo Chema Hadi Mwisho (gt-SW sura 126)

Na. 4: *td 34A au td-SW 5A Jinsi ya Kuitambulisha Ile Dini Moja ya Kweli

Jan. 30 Kusoma Biblia: Zaburi 141 hadi 145

Wimbo Na. 165

Na. 1: Zaburi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 1 (si-SW kur. 104-5 maf. 23-7)

Na. 2: Zaburi 144:1-15

Na. 3: Sababu Inayofanya Maziko ya Yesu na Ziara Tupu Vitupendeze (gt-SW sura 127)

Na. 4: *td 34B au td-SW 5C Je, Ni Vibaya Kushutumu Mafundisho ya Uongo?

Feb. 6 Kusoma Biblia: Zaburi 146 hadi 150

Wimbo Na. 102

Na. 1: Zaburi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 2 (si-SW kur. 105-6 maf. 28-32)

Na. 2: Zaburi 148:1-14

Na. 3: Shangwe ya Ufufuo wa Yesu (gt-SW sura 128)

Na. 4: *td 34C au td-SW 5E Wakati Mungu Akubalipo Mtu Anapobadili Dini

Feb. 13 Kusoma Biblia: Mithali 1 na 2

Wimbo Na. 185

Na. 1: Utangulizi kwa Mithali—Sehemu 1 (si-SW kur. 106-7 maf. 1-5)

Na. 2: Mithali 2:1-19

Na. 3: Jinsi Imani Katika Ufufuo Inavyoimarishwa (gt-SW sura 129)

Na. 4: *td 34D au td-SW 5G Je, Mungu Huona Wema Katika Dini Zote?

Feb. 20 Kusoma Biblia: Mithali 3 na 4

Wimbo Na. 200

Na. 1: Utangulizi kwa Mithali—Sehemu 2 (si-SW kur. 107-8 maf. 6-11)

Na. 2: Mithali 3:1-18

Na. 3: Yesu Aeleza Jinsi ya Kuonyesha Upendo (gt-SW sura 130)

Na. 4: *td 35A au td-SW 43A Ni Nani Watakaofufuliwa Kutoka kwa Wafu?

Feb. 27 Kusoma Biblia: Mithali 5 na 6

Wimbo Na. 11

Na. 1: Wanajuaje Wao Ni Wana wa Kiroho? (uw-SW kur. 112-16 maf. 8-14)

Na. 2: Mithali 6:1-19

Na. 3: Jinsi Yesu Awaimarishavyo Wanafunzi Wake (gt-SW sura 131)

Na. 4: *td 35B au td-SW 43B Wafu Watafufuliwa Wapi?

Mac. 6 Kusoma Biblia: Mithali 7 na 8

Wimbo Na. 105

Na. 1: Kutambulisha Tengenezo la Yehova Lionekanalo (uw-SW kur. 117-20 maf. 1-7)

Na. 2: Mithali 8:22-36

Na. 3: Kile Yesu Afanya Kwenye Mkono wa Kuume wa Mungu (gt-SW sura 132)

Na. 4: *td 36A au td-SW 16A Kurudi kwa Kristo Hakuonekani

Mac. 13 Kusoma Biblia: Mithali 9 na 10

Wimbo Na. 224

Na. 1: Daraka la Kimaandiko la Baraza Linaloongoza (uw-SW kur. 120-22 maf. 8-12)

Na. 2: Mithali 10:16-32

Na. 3: Kwa Nini Yesu Alikuwa Ndiye Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi (gt-SW sura 133)

Na. 4: *td 36B au td-SW 16B Kurudi kwa Kristo Kunatambuliwa kwa Matukio Yanayoonekana

Mac. 20 Kusoma Biblia: Mithali 11 na 12

Wimbo Na. 38

Na. 1: Kuchanganua Uthamini Wetu Kuelekea Tengenezo la Mungu (uw-SW kur. 123-4 maf. 13, 14)

Na. 2: Mithali 11:1-14

Na. 3: Kwa Nini Kila Mtu Apaswa Kukisoma Kitabu Mtu Mkuu Zaidi (gt-SW—Tayarisha kutoka kwenye habari ya utangulizi katika kitabu.)

Na. 4: *td 37A au td-SW 34A Wakristo Hawana Wajibu wa Kuadhimisha Sabato

Mac. 27 Kusoma Biblia: Mithali 13 na 14

Wimbo Na. 139

Na. 1: Kwa Nini Usikilize Shauri? (uw-SW kur. 125-7 maf. 1-4)

Na. 2: Mithali 14:1-16

Na. 3: *td 37B au td-SW 34B Sheria ya Sabato Haikupewa Wakristo

Na. 4: *td 37C au td-SW 34C Wakati Pumziko la Mungu la Sabato Lianzapo na Kumalizika

Apr. 3 Kusoma Biblia: Mithali 15 na 16

Wimbo Na. 59

Na. 1: Fuata Kielelezo cha Wale Waliokubali Shauri (uw-SW kur. 127-8 maf. 5, 6)

Na. 2: Mithali 15:1-16

Na. 3: *td 38A au td-SW 54B Mungu Atoa Wokovu Kupitia Kristo Pekee

Na. 4: *td 38B au td-SW 54D Wazo la Kusema “Ukiisha Okolewa, Umeokolewa Daima” Halipatani na Maandiko

Apr. 10 Kusoma Biblia: Mithali 17 na 18

Wimbo Na. 163

Na. 1: Sitawisha Sifa Zenye Bei Kubwa (uw-SW kur. 128-31 maf. 7-14)

Na. 2: Mithali 18:1-15

Na. 3: *td 38C au td-SW 54E Imani ya “Kuokoa Ulimwengu Wote” Haipatani na Maandiko

Na. 4: *td 39A au td-SW 4A Maana ya Dhambi

Apr. 17 Kusoma Biblia: Mithali 19 na 20

Wimbo Na. 35

Na. 1: Upendo Hutambulisha Wakristo wa Kweli (uw-SW kur. 132-3 maf. 1-5)

Na. 2: Mithali 19:8-23

Na. 3: *td 39B au td-SW 4B Kwa Nini Wanadamu Wote Hutaabishwa na Dhambi ya Adamu

Na. 4: *td 39C au td-SW 4C Tunda Lililokatazwa Lilikuwa Nini?

Apr. 24 Pitio la Kuandika. Kamilisha Zaburi 119:113 hadi Mithali 20

Wimbo Na. 6

Mei 1 Kusoma Biblia: Mithali 21 na 22

Wimbo Na. 95

Na. 1: La Kufanya Matatizo Yanapotokea (uw-SW uku. 134 maf. 6-9)

Na. 2: Mithali 22:1-16

Na. 3: *td 39D au td-SW 4F Ni Nini Maana ya Kukosea Roho Takatifu?

Na. 4: *td 40A au td-SW 31A Nafsi Ni Nini?

Mei 8 Kusoma Biblia: Mithali 23 na 24

Wimbo Na. 46

Na. 1: Shughulika na Matatizo Kimaandiko (uw-SW kur. 135-8 maf. 10-17)

Na. 2: Mithali 24:1-16

Na. 3: *td 40B au td-SW 31B Nafsi na Roho Zatofautianaje?

Na. 4: *td 41A au td-SW 33A Roho Takatifu Ni Nini?

Mei 15 Kusoma Biblia: Mithali 25 na 26

Wimbo Na. 145

Na. 1: Zoea Utawa Nyumbani (uw-SW kur. 139-41 maf. 1-5)

Na. 2: Mithali 25:1-13

Na. 3: *td 41B au td-SW 33B Nguvu ya Uhai ya Mwanadamu na ya Mnyama Inaitwa Roho

Na. 4: *td 41C au td-SW 33C Sababu Inayotufanya Tuepuke Namna Zote za Uchawi

Mei 22 Kusoma Biblia: Mithali 27 na 28

Wimbo Na. 84

Na. 1: Mithali—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 1 (si-SW kur. 109-10 maf. 19-28)

Na. 2: Mithali 28:1-14

Na. 3: *td 42A au td-SW 49A Kwa Nini Yehova Hawezi Kuwa Sehemu ya Utatu

Na. 4: *td 42B au td-SW 49B Mwana Si Sawa na Baba

Mei 29 Kusoma Biblia: Mithali 29 hadi 31

Wimbo Na. 50

Na. 1: Mithali—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa—Sehemu 2 (si-SW kur. 110-11 maf. 29-38)

Na. 2: Mithali 31:10-31

Na. 3: *td 42C au td-SW 49D Jinsi Mungu na Kristo Ni Umoja

Na. 4: *td 42D au td-SW 49E Roho Takatifu Si Mtu

Juni 5 Kusoma Biblia: Mhubiri 1 hadi 3

Wimbo Na. 41

Na. 1: Utangulizi kwa Mhubiri (si-SW kur. 112-13 maf. 1-8)

Na. 2: Mhubiri 3:1-9, 18-22

Na. 3: *td 43A au td-SW 46C Taabu za Ulimwengu Haziletwi na Mungu

Na. 4: *td 43B au td-SW 46D Sababu Mungu Ameruhusu Uovu

Juni 12 Kusoma Biblia: Mhubiri 4 hadi 6

Wimbo Na. 62

Na. 1: Timiza Sehemu Yako Katika Mpango wa Mungu wa Familia (uw-SW kur. 142-4 maf. 6-13)

Na. 2: Mhubiri 5:1-8, 18-20

Na. 3: *td 43C au td-SW 46E Mungu Adhihirisha Rehema Yake Kubwa

Na. 4: *td 43D au td-SW 46F Ufalme wa Mungu Ndilo Suluhisho Pekee

Juni 19 Kusoma Biblia: Mhubiri 7 hadi 9

Wimbo Na. 162

Na. 1: Sababu za Kimaandiko Zinazotufanya Tusiwe Chini ya Torati ya Musa (uw-SW kur. 146-8 maf. 1-6)

Na. 2: Mhubiri 7:1-12

Na. 3: *td 44A au td-SW 18A Lazima Wakristo Wote wa Kweli Washuhudie Kweli

Na. 4: *td 44B au td-SW 18B Sababu Sisi Twaendelea Kutembelea Watu

Juni 26 Kusoma Biblia: Mhubiri 10 hadi 12

Wimbo Na. 133

Na. 1: Mhubiri—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 114 maf. 15-19)

Na. 2: Mhubiri 12:1-14

Na. 3: *td 44C au td-SW 18F Kutoa Ushuhuda Kwatuondolea Hatia ya Damu

Na. 4: *td 1A au td-SW 12A Sababu Kuabudu Wazazi Waliokufa Ni Kazi Bure

Julai 3 Kusoma Biblia: Wimbo Ulio Bora 1 hadi 4

Wimbo Na. 168

Na. 1: Utangulizi kwa Wimbo Ulio Bora (si-SW uku. 115 maf. 1-4)

Na. 2: Wimbo Ulio Bora 2:1-14

Na. 3: *td 1B au td-SW 12B Twaweza Kuheshimu Wanadamu, Lakini Twamwabudu Mungu Pekee

Na. 4: *td 2A au td-SW 7A Vita ya Mungu ya Kumaliza Uovu

Julai 10 Kusoma Biblia: Wimbo Ulio Bora 5 hadi 8

Wimbo Na. 152

Na. 1: Wimbo Ulio Bora—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 117 maf. 16-18)

Na. 2: Wimbo Ulio Bora 8:1-14

Na. 3: *td 2B au td-SW 7C Har–Magedoni Haipingani na Upendo wa Mungu

Na. 4: *td 3A au td-SW 41A Ubatizo Ni Takwa la Kikristo

Julai 17 Kusoma Biblia: Isaya 1 hadi 3

Wimbo Na. 180

Na. 1: Utangulizi kwa Isaya (si-SW kur. 118-19 maf. 1-8)

Na. 2: Isaya 1:1-13

Na. 3: *td 3B au td-SW 41B Ubatizo Hausafishi Dhambi

Na. 4: *td 4A au td-SW 1A Biblia Ni Neno la Mungu Lenye Pumzi

Julai 24 Kusoma Biblia: Isaya 4 hadi 7

Wimbo Na. 144

Na. 1: Imani Ni Muhimu Ili Kupata Msamaha na Wokovu (uw-SW kur. 148-50 maf. 7-10)

Na. 2: Isaya 6:1-13

Na. 3: *td 4B au td-SW 1C Biblia Ni Uongozi Unaofaa Siku Zetu

Na. 4: *td 4C au td-SW 1F Biblia Iliandikwa Kwa Ajili ya Watu wa Mataifa na Jamii Zote

Julai 31 Kusoma Biblia: Isaya 8 hadi 10

Wimbo Na. 140

Na. 1: Faida za Kuijua Torati (uw-SW kur. 150-1 maf. 11-13; uku. 153 fu. 14)

Na. 2: Isaya 9:1-12

Na. 3: *td 5A au td-SW 2A Kutiwa Damu Mishipani Kunavunja Sheria ya Mungu

Na. 4: *td 5B au td-SW 2B Kumtii Mungu Ni Muhimu

Ago. 7 Kusoma Biblia: Isaya 11 hadi 13

Wimbo Na. 44

Na. 1: Kanuni za Msingi Zilizo Katika Torati ya Musa: “Madaraka Kuelekea kwa Mungu” (uw-SW uku. 152)

Na. 2: Isaya 11:1-10

Na. 3: *td 6A au td-SW 40D Nyakati za Mataifa Zilimalizika 1914

Na. 4: *td 7A au td-SW 10A Kutambulisha Kanisa la Kikristo Halisi

Ago. 14 Kusoma Biblia: Isaya 14 hadi 17

Wimbo Na. 170

Na. 1: Kanuni za Msingi Zilizo Katika Torati ya Musa: “Mazoea ya Kidini Yaliyokatazwa” (uw-SW uku. 152)

Na. 2: Isaya 14:3-20

Na. 3: *td 7B au td-SW 10D Kanisa la Kikristo la Kweli Limejengwa juu ya Kristo

Na. 4: *td 8A au td-SW 50A Uumbaji Unakubaliana na Sayansi Iliyohakikishwa

Ago. 21 Kusoma Biblia: Isaya 18 hadi 22

Wimbo Na. 175

Na. 1: Kanuni za Msingi Zilizo Katika Torati ya Musa: “Ndoa na Maisha ya Jamaa” (uw-SW uku. 152)

Na. 2: Isaya 21:1-17

Na. 3: *td 8B au td-SW 50B Siku za Kuumba Hazikuwa Siku za Saa 24

Na. 4: *td 9A au td-SW 28A Yesu Alikufa juu ya Mti wa Aibu, Si juu ya Msalaba

Ago. 28 Pitio la Kuandika. Kamilisha Mithali 21 hadi Isaya 22

Wimbo Na. 204

Sept. 4 Kusoma Biblia: Isaya 23 hadi 26

Wimbo Na. 106

Na. 1: Kanuni za Msingi Zilizo Katika Torati ya Musa: “Kazi Zinazohusu Watu Wengine” (uw-SW uku. 152)

Na. 2: Isaya 25:1-12

Na. 3: *td 9B au td-SW 28B Sababu Kuabudu Msalaba Ni Ibada ya Sanamu

Na. 4: *td 10A au td-SW 24A Sababu Binadamu Hufa

Sept. 11. Kusoma Biblia: Isaya 27 hadi 29

Wimbo Na. 27

Na. 1: Uhai na Damu Ni Vitakatifu (uw-SW kur. 154-6 maf. 1-6)

Na. 2: Isaya 28:1-13

Na. 3: *td 10B au td-SW 24B Wafu Hawana Fahamu na Hawajui Lolote

Na. 4: *td 10C au td-SW 24C Sababu Haiwezekani Kusema na Wafu

Sept. 18 Kusoma Biblia: Isaya 30 hadi 33

Wimbo Na. 160

Na. 1: Matumizi ya Damu kwa Utibabu na Daraka la Mkristo (uw-SW kur. 156-60 maf. 7-12)

Na. 2: Isaya 32:1-8, 16-20

Na. 3: *td 11A au td-SW 9A Ibilisi Yuko Kweli-Kweli

Na. 4: *td 11B au td-SW 9B Ibilisi Atawala Mfumo Huu wa Mambo

Sept. 25 Kusoma Biblia: Isaya 34 hadi 37

Wimbo Na. 146

Na. 1: Wakristo wa Kweli Si Sehemu ya Ulimwengu (uw-SW kur. 161-3 maf. 1-6)

Na. 2: Isaya 35:1-10

Na. 3: *td 11C au td-SW 9D Malaika Waliojiunga na Shetani Walijifanya Wenyewe Mashetani

Na. 4: *td 12A au td-SW 6A Kusudi la Mungu kwa Dunia

Okt. 2 Kusoma Biblia: Isaya 38 hadi 40

Wimbo Na. 143

Na. 1: Kile Ambacho Kutokuwa Sehemu ya Ulimwengu Chataka Kutoka kwa Wakristo (uw-SW kur. 163-8 maf. 7-16)

Na. 2: Isaya 40:12-26

Na. 3: *td 12B au td-SW 6C Dunia Itakaliwa Sikuzote

Na. 4: *td 13A au td-SW 21A Jinsi ya Kutambulisha Manabii wa Uongo

Okt. 9 Kusoma Biblia: Isaya 41 hadi 43

Wimbo Na. 92

Na. 1: Endelea Kusema Neno la Mungu kwa Ujasiri (uw-SW kur. 169-71 maf. 1-7)

Na. 2: Isaya 43:1-15

Na. 3: *td 14A au td-SW 15A Ponyo la Kiroho Lina Faida Zenye Kudumu

Na. 4: *td 14B au td-SW 15B Ufalme wa Mungu Utaleta Maponyo ya Kimwili Yenye Kudumu

Okt. 16 Kusoma Biblia: Isaya 44 hadi 46

Wimbo Na. 166

Na. 1: Kunufaika na Kielelezo cha Mitume (uw-SW uku. 172 fu. 8)

Na. 2: Isaya 46:1-13

Na. 3: *td 14C au td-SW 15C Maponyo ya Imani ya Kisasa Hayana Uthibitisho wa Kukubaliwa na Mungu

Na. 4: *td 14D au td-SW 15D Kusema kwa Lugha Kulitimiza Kusudi Layo

Okt. 23 Kusoma Biblia: Isaya 47 hadi 49

Wimbo Na. 56

Na. 1: Kuhubiri kwa Ujasiri na kwa Busara (uw-SW kur. 173-5 maf. 9-13)

Na. 2: Isaya 48:1-11, 16-19

Na. 3: *td 15A au td-SW 25B Ni 144,000 Peke Yao Waendao Mbinguni

Na. 4: *td 16A Hakuna Anayeteswa Katika Helo (Moto wa Mateso)

Okt. 30 Kusoma Biblia: Isaya 50 hadi 53

Wimbo Na. 132

Na. 1: Weka Karibu Katika Akili Kwamba Siku ya Yehova Iko Karibu (uw-SW kur. 176-7 maf. 1-4)

Na. 2: Isaya 52:1-15

Na. 3: *td 16B au td-SW 27A Moto Ni Mfano wa Maangamizi

Na. 4: *td 16C au td-SW 27C Hamna Moto Halisi Katika Kielezi cha Tajiri na Lazaro

Nov. 6 Kusoma Biblia: Isaya 54 hadi 57

Wimbo Na. 187

Na. 1: Endelea Kukaa Chonjo Uone Matukio Yanayotimiza Ile Ishara (uw-SW kur. 178-9 maf. 5, 6)

Na. 2: Isaya 55:1-13

Na. 3: *td 17A au td-SW 39B Wakristo wa Mapema Hawakuadhimisha Siku za Kuzaliwa Wala Krismasi

Na. 4: *td 18A au td-SW 36A Ibada ya Sanamu Ni Chukizo kwa Mungu

Nov. 13 Kusoma Biblia: Isaya 58 hadi 62

Wimbo Na. 107

Na. 1: Kazi Kubwa ya Kutenganisha—Uthibitisho Kwamba Mwisho Uko Karibu (uw-SW kur. 180-83 maf. 7-14)

Na. 2: Isaya 60:4-17

Na. 3: *td 18B au td-SW 36B Ibada ya Sanamu Ilikuwa Mtego kwa Israeli

Na. 4: *td 18C au td-SW 36C Ibada Ambayo Yehova Hukataa Kabisa

Nov. 20 Kusoma Biblia: Isaya 63 hadi 66

Wimbo Na. 77

Na. 1: Isaya—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 123 maf. 34-9)

Na. 2: Isaya 65:11-25

Na. 3: *td 19A au td-SW 26A Mungu Hakubali Mchanganyiko wa Dini Nyingi

Na. 4: *td 19B au td-SW 26B Ujitoaji wa Pekee Wahitajiwa na Mungu

Nov. 27 Kusoma Biblia: Yeremia 1 hadi 3

Wimbo Na. 70

Na. 1: Utangulizi kwa Yeremia (si-SW uku. 124 maf. 1-5)

Na. 2: Yeremia 1:4-19

Na. 3: *td 20A au td-SW 55A Lazima Wakristo wa Kweli Walijue na Kulitumia Jina la Mungu

Na. 4: *td 20B au td-SW 55C Biblia na Uumbaji Vyashuhudia Kuwako kwa Mungu

Des. 4 Kusoma Biblia: Yeremia 4 hadi 6

Wimbo Na. 97

Na. 1: Kusudi la Yehova Lenye Hekima na Lenye Upendo (uw-SW kur. 184-5 maf. 1-5)

Na. 2: Yeremia 5:1-14

Na. 3: *td 20C au td-SW 55D Sifa Nzuri Ajabu za Yehova

Na. 4: *td 20D au td-SW 55F Si Wote Wanaomtumikia Mungu Yule Yule

Des. 11 Kusoma Biblia: Yeremia 7 hadi 9

Wimbo Na. 158

Na. 1: Yehova Anawafanya Watu Wake Wawe Wenye Umoja (uw-SW kur. 186-8 maf. 6-9)

Na. 2: Yeremia 9:12-26

Na. 3: *td 21A au td-SW 22A Chanzo cha Mashahidi wa Yehova

Na. 4: *td 22A au td-SW 56B Yesu Ni Mwana wa Mungu na Mfalme Aliyewekwa Rasmi

Des. 18 Kusoma Biblia: Yeremia 10 hadi 12

Wimbo Na. 222

Na. 1: Viumbe vya Kibinadamu Vitawekwa Huru (uw-SW kur. 188-91 maf. 10-17)

Na. 2: Yeremia 10:6-15, 22-25

Na. 3: *td 22B au td-SW 56D Sababu Ni Lazima Tumwamini Yesu Kristo

Na. 4: *td 22C au td-SW 56E Lazima Kumwamini Kristo Kuandamane na Matendo

Des. 25 Pitio la Kuandika. Kamilisha Isaya 23 hadi Yeremia 12

Wimbo Na. 34

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki