Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Mei 1 hadi Agosti 21, 1995. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Ibada ya Mungu ni jambo la kibinafsi na haitegemei kwa njia yoyote uhusiano wetu pamoja na wengine. (1 Yoh. 4:20) [uw-SW uku. 134 fu. 7]
2. Shauri la baraza linaloongoza kwa Wakristo Mataifa kwamba wajiepushe na ibada ya sanamu, damu, na uasherati lilitegemea Torati ya Musa. (Mdo. 15:28, 29) [uw-SW uku. 149 fu. 8]
3. Awali, Torati ya Musa ilikusudiwa ihusu wanadamu wote. (Zab. 147:19, 20) [uw-SW uku. 147 fu. 5]
4. Sura ya 53 ya Isaya, iliyoandikwa miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, ni kama simulizi la ushahidi wa kujionea kiwaziwazi unaofafanua Yesu Kristo na jinsi alivyotendewa. [si-SW uku. 119 fu. 8]
5. Maneno ya Sulemani kwenye Mhubiri 3:1, 2 hurejezea tu hali yenye kuendelea ya maisha na kifo na si kuamuliwa kimbele yatakayompata mtu mmoja-mmoja. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 10/15 uku. 5.]
6. Hakuna chanzo cha kilimwengu kinachoweza kutoshana na ushauri ufaao ambao Biblia hutoa kwa mambo ya familia. [uw-SW uku. 144 fu. 11]
7. Kitabu cha Mithali chafikia kiini cha matatizo yetu katika kushauri kwamba tutumaini Mungu kwa ukamili. [si-SW uku. 111 fu. 35]
8. Wazazi wanaoruhusu watoto wao watazame chochote kile ambacho huenda kikawa katika televisheni, ni sawa na kuwafungulia wazurure. (Mit. 29:15) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 8/1 uku. 12 fu. 8.]
9. Matatizo yatokeapo katika ndoa, Mkristo wa kweli hatatumia makosa ya mwenzi wake kuwa kisababu cha kuwekea kando madaraka yake mwenyewe. [uw-SW kur. 140-141 maf. 4, 5]
10. Taarifa ya Sulemani katika kitabu cha Mhubiri kwamba yote ni ubatili hutia ndani kila kitu. [si-SW uku. 114 fu. 15]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Ni nini iliyo kanuni ya msingi ya Kutoka 20:7? [uw-SW uku. 152]
12. Ni nani wawili kati ya waliokuwa wafalme wanne waliotawala katika Yuda, Isaya alipokuwa akitumikia akiwa nabii? [si-SW uku. 118 fu. 3]
13. Kama ilivyosimuliwa kwenye Isaya 14:4, 12-14, ni mtazamo wa nani ulioonyeshwa na mfalme wa Babiloni? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w85-SW 8/15 uku. 27 fu. 2.]
14. Kulingana na Kutoka 19:10, 11, Yehova ataka waabudu wake waweje? [uw-SW uku. 152]
15. Mlinzi wa siku ya kisasa ni nani, naye atangaza nini? (Isa. 21:8, 12) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 3/1 uku. 12 fu. 10.]
16. Kwa sababu gani Mhubiri 12:12 hutoa maoni hasi hivyo kuhusu vitabu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 9/15 uku. 25.]
17. Kupatana na Mithali 1:2-4, kitabu cha Mithali chakazia nini? [si-SW uku. 109 fu. 19]
18. Paulo alimaanisha nini alipowasihi Wakorintho ‘wapanuke’? (2 Kor. 6:13, NW) [uw-SW uku. 137 fu. 14]
19. Upendo unakuwaje na “nguvu kama mauti”? (Wim. 8:6, 7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 11/15 uku. 25.]
20. Ni masomo gani yenye kutumika yanayofundishwa katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora chenye kuvutia? [si-SW uku. 117 fu. 16]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Ijapokuwa hatuko chini ya Torati ya Musa, twafaidika na maarifa sahihi ya _________________________ zinazoitegemeza na ile mifano ya _________________________ iliyomo. [uw-SW uku. 153 fu. 14]
22. Sheria kwenye Kutoka 20:4-6 hukataza _________________________ , na andiko lenyewe huonyesha kwamba sheria hii yategemea kanuni ya kwamba Yehova hutaka _________________________ . [uw-SW uku. 152]
23. Kanuni iliyo kwenye Kumbukumbu la Torati 7:1-4 huonyesha waziwazi kwamba mtumishi wa Mungu hapaswi kufanya mapatano ya _________________________ na mtu asiyemtumikia _________________________ . [uw-SW uku. 152]
24. Kwenye Wimbo Ulio Bora 2:1-3, semi zatumiwa zinazoonyesha unyenyekevu na kiasi cha _________________________ , na vilevile tabia na ustadi wenye kupendeza wa mpenzi wake _________________________ . [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 11/15 uku. 24.]
25. Watumishi waaminifu wa Yehova hukataa zoea la kutaka kujua kutoka _________________________ kwa niaba ya _________________________ , kwa kuwa uwasiliano kama huo kwa kweli ni pamoja na _________________________ . (Isa. 8:19) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 3/15 uku. 20 fu. 11.]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Kulingana na Mithali 26:20, 21, tukiwa (wepesi kujibu; kutokeza; wenye hali pole), badala ya ‘kuongeza kuni kwenye moto’ na kuchokoza wengine, tutakuwa na (matatizo ya kibinafsi; uwasiliano dhaifu; uhusiano mzuri) nao. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 10/15 uku. 13 fu. 16.]
27. Kulingana na Mithali 27:6, mtu akupendaye (hatasema kamwe chochote cha kuumiza hisia zako; ataogopa kukuambia kweli kukuhusu; hatakosa kukupa shauri unapolihitaji). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 9/15 uku. 28.]
28. Uthibitisho wa kwamba Sulemani alikuwa mwandikaji wa kitabu cha Mhubiri waweza kuonekana kwa kuwa (jina lake lapatikana kotekote kwenye hicho kitabu; waandikaji wa vitabu vingine vya Biblia wanamtaja kuwa mwandikaji wacho; kitabu chenyewe chamthibitisha Sulemani kuwa mwandikaji bila kumtaja). [si-SW uku. 112 fu. 4]
29. Watu ambao hufikiri kwamba mtazamo wa leo wa kutohukumu-hukumu, kukubali chochote kinachosemwa au kutendwa ni kutiwa nuru, huo kwa kweli ni (kutokuwa kwenye kudhuru; kuvumilia tu; kuwa katika giza la kiroho). (Isa. 5:20) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 3/1 uku. 11.]
30. Wimbo Ulio Bora hukazia (daraka la Sulemani akiwa mfalme; utajiri mwingi wa Sulemani; uaminifu wa msichana wa mashambani kwa mvulana mchungaji). [si-SW uku. 115 fu. 2]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Mit. 22:3; Mhu. 7:21, 22; Isa. 13:19, 20; Mt. 5:23, 24; Kol. 3:18-20, 23, 24
31. Ijapokuwa Yehova haokoi watu wake kimuujiza kutokana na aksidenti, vita ya kikabila, au uhalifu, kujizoeza hekima yenye kutumika inayotegemea Biblia kwaweza kuwa na thamani. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 1/1 uku. 17 fu. 23.]
32. Kuna uthibitisho wa kutosha kutotilia shaka kamwe utimizo wa unabii uliopuliziwa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 5/15 uku. 6.]
33. Mkristo wa kweli huchukua hatua ya kwanza kutokeza mahusiano ya amani pamoja na ndugu zake. [uw-SW uku. 135 fu. 10]
34. Maendeleo katika mahusiano ya familia huja, si kila mmoja angojapo yule mwingine afanye jambo fulani, bali kila mmoja afanyapo sehemu yake vizuri, hivyo akionyesha kwamba yeye binafsi hujizoeza ujitoaji kimungu. [uw-SW uku. 143 fu. 10]
35. Usitazamie isivyo kihalisi ukamilifu wako au wa mahusiano na wanadamu wengine wasio wakamilifu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 3/1 uku. 8.]