Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1996
MAAGIZO
Wakati wa 1996, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango wakati wa kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli [uw-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation [*td] au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [td-SW], Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele [kl-SW], na Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW] vitakuwa msingi wa migawo.
Shule yapaswa kuanza KWA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha kisha kuendelea kama ifuatavyo:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma, nao utategemea habari katika kitabu Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapishwa katika kichapo hicho. Lengo lapasa kuwa si kuzungumza juu ya habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, ukikazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa chapasa kitumiwe. Wote wanatiwa moyo wafanye matayarisho ya kimbele kwa uangalifu ili wasikilizaji wanufaike kikamili na habari hiyo.
Ndugu waliogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa ni lazima, au ikiwa msemaji ameomba shauri.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma atakayeonyesha kwa matokeo jinsi habari hiyo inavyohusu mahitaji ya mahali hapo. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Pitio la ujumla la sekunde 30 hadi 60 la sura ambazo zimegawiwa laweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
MGAWO NA. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa habari iliyotolewa kuwa mgawo utakaotolewa na ndugu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika shule kubwa na pia katika vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo mafupi katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyogawiwa yapasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa isomwe haifuatani mfululizo, mwanafunzi aweza kutaja mstari mahali ambapo usomaji waendelea.
MGAWO NA. 3: Dakika 5. Huu utagawiwa akina dada. Habari za utoaji huu zitategemea “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia, au kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Mwanafunzi aliyegawiwa apaswa awe anaweza kusoma. Wakati wa kutoa habari hii, mwanafunzi aweza kuwa ameketi au amesimama. Unapotegemea habari katika “Bible Topics for Discussion,” au Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia, akina dada waliogawiwa sehemu hii watahitaji kutumia kikao kinachofaa kichwa na habari zitakazoshughulikiwa, hasa kile kinachohusu utumishi wa shambani au ushahidi wa vivi-hivi. Unapotegemea habari katika kitabu Ujuzi, huo waweza kushughulikiwa ukiwa ziara ya kurudia au funzo la Biblia nyumbani. Mwangalizi wa shule atapendezwa hasa na njia ambayo mwanafunzi amsaidia mwenye nyumba atoe sababu na kuelewa habari na jinsi maandiko yanavyotumiwa. Mafungu katika kitabu hayahitaji kusomwa. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini msaidizi wa ziada aweza kutumiwa. Si kikao kinachopasa kupewa uangalifu mkuu bali ni matumizi ya habari yenye matokeo.
MGAWO NA. 4: Dakika 5. Huu utagawiwa ndugu au dada. Utategemea habari katika kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Unapogawiwa ndugu, huu wapaswa uwe hotuba kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi kwa huyo ndugu kutayarisha hotuba yake akifikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Dada anapopewa sehemu hii, habari yapasa itolewe kama vile ilivyoonyeshwa kwa Mgawo Na. 3.
SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila utoaji wa mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri hususa, bila kufuata kwa lazima programu ya shauri ya hatua kwa hatua iliyoonyeshwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala yake, apaswa kukazia fikira sehemu zile ambazo mwanafunzi ahitaji kufanyia maendeleo. Ikiwa mwanafunzi astahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri apaswa atie duara kuzunguka kisanduku, ambamo kwa kawaida alama “V,” “M,” au “T” zingewekwa, cha sifa ya usemi ambayo mwanafunzi apaswa kufanyia kazi safari nyingine. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89-SW) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale watakaoshiriki katika programu wapaswa wakae kuelekea mbele ya jumba. Hiyo itaokoa wakati na itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati uruhusupo baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuarifu na yenye mafaa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo mengine yoyote mafupi baada ya kila utoaji wa mwanafunzi. Ikiwa ule mgawo wa mambo makuu ya Biblia haukuridhisha, shauri la faragha laweza kutolewa.
KUTAYARISHA MIGAWO: Kabla ya kutayarisha sehemu iliyogawiwa, mwanafunzi apaswa kusoma kwa uangalifu habari ya Kiongozi cha Shule inayoshughulikia sifa ya usemi ipasayo kufanyiwa kazi. Wanafunzi waliopewa Mgawo Na. 2 waweza kuchagua kichwa kinachofaa sehemu ya Biblia inayopasa isomwe. Migawo mingine itatayarishwa kulingana na kichwa kilichoonyeshwa kwenye ratiba iliyochapishwa.
KUFUATA WAKATI: Hakuna apaswaye kupita wakati uliowekwa, wala shauri na maelezo ya mshauri hayapaswi kupita wakati uliowekwa. Migawo Na. 2 hadi 4 zapasa zikatizwe kwa busara wakati unapokwisha. Yule anayechaguliwa kutoa ishara ya kuacha apaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulikia Mgawo Na. 1 na mambo makuu ya Biblia wanapopitisha wakati wao wapaswa wapewe shauri la faragha. Wote wapaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Programu kwa jumla: Dakika 45, bila wimbo na sala.
PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi pitio la kuandika litatolewa. Katika kujitayarisha, pitia habari iliyogawiwa na kukamilisha usomaji wa Biblia ulioratibiwa. Biblia pekee ndiyo yaweza kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atapitia majibu ya maswali ya pitio pamoja na wasikilizaji na kukazia fikira maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayaelewe majibu kwa wazi. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zafanya iwe lazima, pitio la kuandika laweza kutolewa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa kwenye ratiba.
MAKUTANIKO MAKUBWA: Makutaniko yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikishwa huenda yakataka kupanga vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine sehemu zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasiobatizwa ambao maisha zao zapatana na kanuni za Kikristo waweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.
WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kutaniko waweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kujitahidi kuwapo kwenye kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa kudhamiria. Mwanafunzi asipokuwapo wakati ameratibiwa, mjitoleaji aweza kuchukua mgawo huo, akifanya matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule aweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.
RATIBA
*td – “Bible Topics for Discussion” kama ipatikanavyo katika New World Translation au td-SW
Jan. 1 Kusoma Biblia: Yeremia 13 hadi 15
Na. 1: Namna Umoja wa Kweli wa Kikristo Unavyopatikana (uw-SW kur. 5-7 maf. 1-7)
Na. 2: Yeremia 14:10-22
Na. 3: *td 23A au td-SW 42B Mambo Ambayo Ufalme wa Mungu Utafanyia Wanadamu
Na. 4: Yesu Hakuenda Mbinguni Akiwa na Mwili Wenye Kuonekana (rs-SW uku. 334 fu. 2–uku. 335 fu. 2)
Jan. 8 Kusoma Biblia: Yeremia 16 hadi 19
Na. 1: Mambo Makuu Yanayosaidia Kuwe na Umoja wa Kikristo (uw-SW uku. 8 fu. 8 hadi 8[3])
Na. 2: Yeremia 18:1-17
Na. 3: *td 23B au td-SW 42C Utawala wa Ufalme Waanza Adui za Kristo Wakiwa Wangali Waendelea na Kazi Zao
Na. 4: Sababu Kwa Nini Yesu Alionekana Katika Miili Iliyofanyizwa (rs-SW uku. 335 fu. 3–uku. 336 fu. 2)
Jan. 15 Kusoma Biblia: Yeremia 20 hadi 22
Na. 1: Mambo Mengine Yanayounganisha Wakristo (uw-SW uku. 9 maf. 8[4] hadi 9)
Na. 2: Yeremia 20:1-13
Na. 3: *td 23C au td-SW 42E Ufalme wa Mungu Hauji Kupitia Jitihada za Mwanadamu
Na. 4: Wale Wanaofufuliwa Kutawala Pamoja na Kristo Watakuwa Kama Yeye (rs-SW uku. 336 maf. 4–8)
Jan. 22 Kusoma Biblia: Yeremia 23 hadi 25
Na. 1: Epuka Mavutano Yenye Kugawanya (uw-SW kur. 10-11 maf. 10-12)
Na. 2: Yeremia 23:16-32
Na. 3: *td 24A au td-SW 40A Maana ya “Mwisho wa Ulimwengu”
Na. 4: Kile Ambacho Ufufuo Utamaanisha kwa Wanadamu kwa Ujumla (rs-SW uku. 337 fu. 1–uku. 338 fu. 2)
Jan. 29 Kusoma Biblia: Yeremia 26 hadi 28
Na. 1: Namna Alivyo Yehova (uw-SW kur. 12-13 maf. 1-4)
Na. 2: Yeremia 26:1-16
Na. 3: *td 24B au td-SW 40B Uwe Macho Kuona Uthibitisho wa Siku za Mwisho
Na. 4: Sababu Kwa Nini Wanaofufuliwa Hawatahukumiwa kwa Matendo Yao ya Wakati Uliopita (rs-SW uku. 338 fu. 4)
Feb. 5 Kusoma Biblia: Yeremia 29 hadi 31
Na. 1: Iga Kielelezo cha Yehova cha Upendo (uw-SW kur. 14-15 maf. 5-7)
Na. 2: Yeremia 31:27-40
Na. 3: *td 25A au td-SW 51B Mungu Aahidi Uhai Udumuo Milele kwa Wanadamu Watiifu
Na. 4: Jinsi “Mabaki ya Wafu” Wanavyokuja Kwenye Uhai Duniani (rs-SW uku. 339 maf. 1–4)
Feb. 12 Kusoma Biblia: Yeremia 32 na 33
Na. 1: Fundisha Watu Kweli Juu Ya Mungu (uw-SW kur. 15-17 maf. 8-11[2])
Na. 2: Yeremia 33:1-3, 14-26
Na. 3: *td 25B au td-SW 51D Ni Wale Walio Katika Mwili wa Kristo tu Wanaoenda Mbinguni
Na. 4: Wale Wanaotiwa Katika Ufufuo wa Kidunia (rs-SW uku. 340 fu. 1-uku. 341 fu. 1)
Feb. 19 Kusoma Biblia: Yeremia 34 hadi 37
Na. 1: Kuna Yehova Mmoja Pekee (uw-SW kur. 17-18 maf. 11[3] hadi 12)
Na. 2: Yeremia 35:1-11, 17-19
Na. 3: *td 25C au td-SW 51E Uhai Udumuo Milele Umeahidiwa Idadi Isiyo na Mpaka ya “Kondoo Wengine”
Na. 4: Matukio Yanayohusiana na Kuwapo kwa Kristo Yanatukia kwa Kipindi cha Miaka Mingi (rs-SW uku. 127 fu. 2-uku. 128 fu. 1)
Feb. 26 Kusoma Biblia: Yeremia 38 hadi 41
Na. 1: Kinachomaanishwa na Kutembea Katika Jina la Mungu (uw-SW kur. 18-19 maf. 13-15)
Na. 2: Yeremia 38:1-13
Na. 3: *td 26A au td-SW 32B Lazima Muungano wa Ndoa Uheshimike
Na. 4: Kurudi kwa Kristo Hakuonekani kwa Macho ya Kibinadamu (rs-SW uku. 128 maf. 2–4)
Mac. 4 Kusoma Biblia: Yeremia 42 hadi 45
Na. 1: Saidia Wengine Wakubali Biblia Kuwa Neno la Mungu (uw-SW kur. 20-22 maf. 1-6)
Na. 2: Yeremia 43:1-13
Na. 3: *td 26B au td-SW 32C Lazima Wakristo Waheshimu Kanuni ya Ukichwa
Na. 4: Jinsi ya Kuja kwa Yesu na Jinsi Kila Jicho Litakavyomwona Yeye (rs-SW uku. 129 fu. 1–uku. 130 fu. 3)
Mac. 11 Kusoma Biblia: Yeremia 46 hadi 48
Na. 1: Soma Biblia Kila Siku (uw-SW kur. 23-25 maf. 7-11)
Na. 2: Yeremia 48:1-15
Na. 3: *td 26C au td-SW 32D Daraka la Wazazi Wakristo Juu Ya Watoto
Na. 4: Matukio Yanayohusiana na Kuwapo kwa Kristo (rs-SW uku. 130 fu. 4-uku. 131 fu. 3)
Mac. 18 Kusoma Biblia: Yeremia 49 na 50
Na. 1: Jifunze Ili Upate Kujua Juu Ya Yehova (uw-SW kur. 25-26 fu. 12 hadi 12[1])
Na. 2: Yeremia 49:1-11, 15-18
Na. 3: *td 26D au td-SW 32E Wakristo Wapaswa Waoe au Waolewe na Wakristo Wenzao Tu
Na. 4: Wakristo Hawako Chini ya Takwa la Kushika Sabato (rs-SW uku. 269 fu. 1–uku. 270 fu. 2)
Mac. 25 Kusoma Biblia: Yeremia 51 na 52
Na. 1: Yeremia—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 129 maf. 36-39)
Na. 2: Yeremia 51:41-57
Na. 3: *td 26E au td-SW 32F Wakristo wa Kweli Hawaoi Wake Zaidi ya Mmoja
Na. 4: Hakuna Rekodi ya Biblia Juu Ya Kushika kwa Adamu Siku ya Sabato (rs-SW uku. 270 fu. 3–uku. 271 fu. 1)
Apr. 1 Kusoma Biblia: Maombolezo 1 na 2
Na. 1: Utangulizi kwa Maombolezo (si-SW kur. 130-131 maf. 1-7)
Na. 2: Maombolezo 2:13-22
Na. 3: *td 27A au td-SW 14A Mariamu Hakuwa “Mama ya Mungu”
Na. 4: Yesu Hakugawanya Sheria ya Kimusa Katika Sehemu za “Sherehe” na “Adili” (rs-SW uku. 271 maf. 2, 3)
Apr. 8 Kusoma Biblia: Maombolezo 3 hadi 5
Na. 1: Maombolezo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 132 maf. 13-15)
Na. 2: Maombolezo 5:1-22
Na. 3: *td 27B au td-SW 14C Biblia Huonyesha Kwamba Mariamu Hakuendelea Kuwa “Bikira Nyakati Zote”
Na. 4: Amri Kumi Zilipitilia Mbali Pamoja na Sheria ya Kimusa (rs-SW uku. 272 maf. 1, 2)
Apr. 15 Kusoma Biblia: Ezekieli 1 hadi 4
Na. 1: Utangulizi kwa Ezekieli (si-SW kur. 132-133 maf. 1-6)
Na. 2: Ezekieli 3:16-27
Na. 3: *td 28A au td-SW 45A Kile Ambacho Maandiko Husema Juu Ya Ukumbusho
Na. 4: Sababu Kwa Nini Kizuizi cha Adili Hakikuondolewa Wakati Amri Kumi Zilipopitilia Mbali (rs-SW uku. 273 maf. 1, 2)
Apr. 22 Kusoma Biblia: Ezekieli 5 hadi 8
Na. 1: Fikiria Kichwa cha Biblia na Muktadha wa Maandiko (uw-SW uku. 26 fu. 12[2] na 12[3])
Na. 2: Ezekieli 5:1-15
Na. 3: *td 28B au td-SW 45B Mwadhimisho wa Misa Ni Kinyume cha Maandiko
Na. 4: Kile Ambacho Sabato Yamaanisha kwa Wakristo (rs-SW uku. 273 fu. 3–uku. 274 fu. 2)
Apr. 29 Pitio la Kuandika. Kamilisha Yeremia 13 hadi Ezekieli 8
Mei 6 Kusoma Biblia: Ezekieli 9 hadi 11
Na. 1: Tumia Kibinafsi Yale Unayojifunza na Ushiriki na Wengine (uw-SW kur. 26-28 maf. 12[4] hadi 13)
Na. 2: Ezekieli 9:1-11
Na. 3: Mungu Ataka Uwe na Wakati Ujao Wenye Furaha (kl-SW kur. 6-7 maf. 1-5)
Na. 4: Wale Ambao Biblia Hurejezea Kuwa Watakatifu (rs-SW uku. 406 fu. 2–uku. 407 fu. 2)
Mei 13 Kusoma Biblia: Ezekieli 12 hadi 14
Na. 1: Kile Ambacho Manabii Wasema Juu Ya Yesu (uw-SW kur. 29-31 maf. 1-6)
Na. 2: Ezekieli 14:1-14
Na. 3: Uhai Udumuo Milele Katika Paradiso—Si Ndoto (kl-SW kur. 7-9 maf. 6-10)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Hatusali kwa “Watakatifu” (rs-SW uku. 407 fu. 3-uku. 408 fu. 1)
Mei 20 Kusoma Biblia: Ezekieli 15 na 16
Na. 1: Kazia Uangalifu Mifano ya Kiunabii (uw-SW kur. 32-33 maf. 7 hadi 8[2])
Na. 2: Ezekieli 16:46-63
Na. 3: Jinsi Uhai Utakavyokuwa Katika Paradiso (kl-SW kur. 9-10 maf. 11-16)
Na. 4: Ukweli Juu Ya Kuheshimu Sana Masalio na Mifano ya “Watakatifu” (rs-SW uku. 408 fu. 2-uku. 409 fu. 2)
Mei 27 Kusoma Biblia: Ezekieli 17 hadi 19
Na. 1: Kuhani Wetu Mkuu Afananishwa (uw-SW uku. 33 fu. 8[3] na 8[4])
Na. 2: Ezekieli 18:21-32
Na. 3: Sababu Kwa Nini Ujuzi Juu Ya Mungu Ni Muhimu (kl-SW kur. 10-11 maf. 17-19)
Na. 4: Watakatifu Walio Wakristo wa Kweli Hawako Huru na Dhambi (rs-SW uku. 409 fu. 3)
Juni 3 Kusoma Biblia: Ezekieli 20 na 21
Na. 1: Jinsi Tuwezavyo Kuonyesha Imani Yetu Katika Kristo (uw-SW kur. 33-37 maf. 9-14)
Na. 2: Ezekieli 21:18-32
Na. 3: Kitabu Kifunuacho Ujuzi Juu Ya Mungu (kl-SW kur. 12-13 maf. 1-6)
Na. 4: Wokovu wa Ulimwengu Wote Mzima Ni Kinyume cha Biblia (rs-SW uku. 416 fu. 1)
Juni 10 Kusoma Biblia: Ezekieli 22 na 23
Na. 1: Utii kwa Mungu Huleta Uhuru wa Kweli (uw-SW kur. 38-39 maf. 1-5)
Na. 2: Ezekieli 22:17-31
Na. 3: Kile Ambacho Biblia Hufunua Kuhusu Mungu (kl-SW kur. 13-15 maf. 7-9)
Na. 4: Je, Wanadamu Wote Mwishowe Wataokolewa? (rs-SW uku. 416 fu. 2)
Juni 17 Kusoma Biblia: Ezekieli 24 hadi 26
Na. 1: Mahali Uhuru wa Kweli Unapoweza Kupatikana Leo (uw-SW kur. 40-42 maf. 6-9)
Na. 2: Ezekieli 26:1-14
Na. 3: Sababu Kwa Nini Waweza Kuitumaini Biblia (kl-SW kur. 15-16 maf. 10-13)
Na. 4: “Watu wa Namna Zote” Wataokolewa (rs-SW uku. 417 fu. 1)
Juni 24 Kusoma Biblia: Ezekieli 27 hadi 29
Na. 1: Uhuru wa Kilimwengu Kwa Kweli Ni Utumwa (uw-SW kur. 42-43 maf. 10-12)
Na. 2: Ezekieli 29:1-16
Na. 3: Biblia Ni Sahihi na Yenye Kutegemeka (kl-SW uku. 17 maf. 14, 15)
Na. 4: Biblia Husema Kwamba Wengine Hawataokolewa Kamwe (rs-SW uku. 417 maf. 2-4)
Julai 1 Kusoma Biblia: Ezekieli 30 hadi 32
Na. 1: Jinsi ya Kutambulisha Mashirika Mabaya (uw-SW kur. 44-45 maf. 13, 14)
Na. 2: Ezekieli 31:1-14
Na. 3: Biblia Ni Kitabu Chenye Unabii (kl-SW kur. 17-18 maf. 16-18)
Na. 4: Mtu Akiisha Kuokolewa Hakumaanishi Ameokolewa Sikuzote (rs-SW uku. 417 fu. 5–uku. 418 fu. 3)
Julai 8 Kusoma Biblia: Ezekieli 33 na 34
Na. 1: Lile Suala Kubwa Ambalo Lazima Kila Mtu Akabili (uw-SW kur. 46-47 maf. 1-3)
Na. 2: Ezekieli 34:17-30
Na. 3: Biblia Hutoa Unabii Juu Ya Yesu (kl-SW kur. 19-21 maf. 19, 20)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Lazima Imani Iwe na Kazi (rs-SW uku. 418 fu. 4-uku. 419 fu. 2)
Julai 15 Kusoma Biblia: Ezekieli 35 hadi 37
Na. 1: Iga Imani ya Walio Waaminifu-Washikamanifu (uw-SW kur. 47-52 maf. 4-11)
Na. 2: Ezekieli 35:1-15
Na. 3: Fanyiza Hamu Sana ya Ujuzi Juu Ya Mungu (kl-SW kur. 21-22 maf. 21-23)
Na. 4: Jinsi Tujuavyo Kama Kweli Kuna Ibilisi (rs-SW uku. 284 fu. 2–uku. 285 fu. 1)
Julai 22 Kusoma Biblia: Ezekieli 38 na 39
Na. 1: Kumheshimu Yehova kwa Mwenendo Wetu (uw-SW kur. 52-54 maf. 12-15)
Na. 2: Ezekieli 38:1-4, 10-12, 18-23
Na. 3: Mungu wa Kweli na Jina Lake (kl-SW kur. 23-24 maf. 1-5)
Na. 4: Shetani Si Uovu Tu Ulio Ndani ya Watu (rs-SW uku. 285 fu. 2–uku. 286 fu. 1)
Julai 29 Kusoma Biblia: Ezekieli 40 hadi 44
Na. 1: Kile Ambacho Twajifunza Kutokana na Mungu Kuruhusu Uovu (uw-SW kur. 55-57 maf. 1-7)
Na. 2: Ezekieli 40:1-15
Na. 3: Sababu Kwa Nini Ulitumie Jina la Mungu (kl-SW kur. 24-25 maf. 6-8)
Na. 4: Mungu Hakumuumba Ibilisi (rs-SW uku. 286 fu. 2)
Ago. 5 Kusoma Biblia: Ezekieli 45 hadi 48
Na. 1: Ezekieli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 137 maf. 29-33)
Na. 2: Ezekieli 47:1-12
Na. 3: Jinsi Yehova Alivyofanya Jina Lake Liwe Kubwa (kl-SW kur. 25-27 maf. 9-13)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Mungu Hakumharibu Shetani Mara Baada ya Yeye Kuasi (rs-SW uku. 286 fu. 3–uku. 287 fu. 1)
Ago. 12 Kusoma Biblia: Danieli 1 na 2
Na. 1: Utangulizi kwa Danieli (si-SW kur. 138-139 maf. 1-6)
Na. 2: Danieli 2:31-45
Na. 3: Sifa za Mungu wa Kweli (kl-SW kur. 27-28 maf. 14-16)
Na. 4: Usidhanie Nguvu za Ibilisi Kuwa Kidogo (rs-SW uku. 287 fu. 2–uku. 288 fu. 2)
Ago. 19 Kusoma Biblia: Danieli 3 na 4
Na. 1: Hakuna Ukosefu wa Haki kwa Mungu Kamwe (uw-SW kur. 57-61 maf. 8-16)
Na. 2: Danieli 3:16-30
Na. 3: Yehova Mungu Ni Mwenye Rehema na Mwenye Fadhili (kl-SW kur. 28-29 maf. 17-19)
Na. 4: Kitulizo Kutoka Katika Uvutano Mwovu wa Shetani Kiko Karibu (rs-SW uku. 288 fu. 3-uku. 289 fu. 3)
Ago. 26 Pitio la Kuandika. Kamilisha Ezekieli 9 hadi Danieli 4
Sept. 2 Kusoma Biblia: Danieli 5 na 6
Na. 1: Kinza Majeshi ya Roho Waovu (uw-SW kur. 62-64 maf. 1-5)
Na. 2: Danieli 6:4-11, 16, 19-23
Na. 3: Yehova Si Mwepesi wa Hasira, Hana Upendeleo, na Ni Mwadilifu (kl-SW uku. 30 maf. 20, 21)
Na. 4: Je, Mahusiano Yote ya Ngono Ni Yenye Dhambi? (rs-SW uku. 252 fu. 3–uku. 254 fu. 1)
Sept. 9 Kusoma Biblia: Danieli 7 na 8
Na. 1: Uwe Macho Kuona Mbinu za Ujanja za Ibilisi (uw-SW kur. 64-67 maf. 6-12)
Na. 2: Danieli 7:2-14
Na. 3: Yehova Mungu Ndiye Mmoja (kl-SW kur. 30-31 maf. 22, 23)
Na. 4: Kile Ambacho Biblia Husema Juu Ya Ugoni-Jinsia-Moja (rs-SW uku. 254 maf. 3–5)
Sept. 16 Kusoma Biblia: Danieli 9 na 10
Na. 1: Vaa Silaha Zote Kutoka kwa Mungu (uw-SW kur. 67-69 maf. 13-15)
Na. 2: Danieli 9:20-27
Na. 3: Yesu Kristo Ndiye Ufunguo Uongozao Kwenye Ujuzi Juu Ya Mungu (kl-SW uku. 32 maf. 1-3)
Na. 4: Mabadiliko Ambayo Ni Lazima Yafanywe Ili Kumpendeza Mungu (rs-SW uku. 254 fu. 6–uku. 255 fu. 2)
Sept. 23 Kusoma Biblia: Danieli 11 na 12
Na. 1: Danieli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 141-142 maf. 19-23)
Na. 2: Danieli 12:1-13
Na. 3: Mesiya Aliyeahidiwa (kl-SW uku. 33 maf. 4, 5)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Mtu Mkamilifu Aliweza Kufanya Dhambi (rs-SW uku. 63 fu. 1–uku. 64 fu. 1)
Sept. 30 Kusoma Biblia: Hosea 1 hadi 5
Na. 1: Utangulizi kwa Hosea (si-SW kur. 143-144 maf. 1-8)
Na. 2: Hosea 5:1-15
Na. 3: Nasaba ya Yesu Yamtambulisha Yeye Kuwa Ndiye Mesiya (kl-SW uku. 34 fu. 6)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Twatambua Dhambi Kuwa Halisi (rs-SW uku. 64 fu. 3–uku. 65 fu. 3)
Okt. 7 Kusoma Biblia: Hosea 6 hadi 10
Na. 1: Ujuzi, Imani, na Ufufuo (uw-SW kur. 70-73 maf. 1-7)
Na. 2: Hosea 8:1-14
Na. 3: Unabii Uliotimizwa Wamtambulisha Yesu Kuwa Ndiye Mesiya (kl-SW kur. 34-36 maf. 7, 8)
Na. 4: Jinsi Dhambi Ilivyoathiri Uhusiano Wetu na Mungu (rs-SW uku. 66 maf. 1–4)
Okt. 14 Kusoma Biblia: Hosea 11 hadi 14
Na. 1: Hosea—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 145 maf. 14-17)
Na. 2: Hosea 11:1-12
Na. 3: Ithibati Zaidi Kwamba Yesu Alikuwa Ndiye Mesiya (kl-SW uku. 36 fu. 9)
Na. 4: Kile Ambacho Biblia Husema Juu Ya Nafsi (rs-SW uku. 232 maf. 1–5)
Okt. 21 Kusoma Biblia: Yoeli 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Yoeli na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 146-148 maf. 1-5, 12-14)
Na. 2: Yoeli 2:1-11, 28-32
Na. 3: Yehova Ashuhudia Kuhusu Mwana Wake (kl-SW uku. 38 maf. 10, 11)
Na. 4: Biblia Husema Kwamba Wanyama Ni Nafsi (rs-SW uku. 233 fu. 1–uku. 234 fu. 1)
Okt. 28 Kusoma Biblia: Amosi 1 hadi 5
Na. 1: Utangulizi kwa Amosi (si-SW kur. 148-149 maf. 1-6)
Na. 2: Amosi 3:1-15
Na. 3: Kuwako kwa Yesu Kabla ya Kuwa Binadamu (kl-SW uku. 39 maf. 12-14)
Na. 4: Wakati wa Kifo Wala Nafsi Wala Roho Haiendelei Kuwa na Uhai Wenye Ufahamu (rs-SW uku. 234 fu. 2–uku. 236 fu. 3)
Nov. 4 Kusoma Biblia: Amosi 6 hadi 9
Na. 1: Amosi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 150 maf. 13-17)
Na. 2: Amosi 8:1-14
Na. 3: Mwendo wa Maisha wa Yesu Akiwa Duniani (kl-SW kur. 40-41 maf. 15-17)
Na. 4: Jinsi Ambavyo Biblia Hufafanua Roho Takatifu (rs-SW uku. 261 maf. 1–3)
Nov. 11 Kusoma Biblia: Obadia hadi Yona 4
Na. 1: Utangulizi kwa Obadia na Yona na Kwa Nini Ni Vyenye Mafaa (si-SW kur. 151-153 maf. 1-5, 10-14; kur. 153-155 maf. 1-4, 9-12)
Na. 2: Yona 3:10; 4:1-11
Na. 3: Yesu Yu Hai na Anatawala Akiwa Mfalme (kl-SW kur. 41-42 maf. 18-20)
Na. 4: Uthibitisho wa Kwamba Mtu Yuna Roho Takatifu (rs-SW uku. 262 fu. 2–uku. 263 fu. 1)
Nov. 18 Kusoma Biblia: Mika 1 hadi 4
Na. 1: Utangulizi kwa Mika (si-SW kur. 155-156 maf. 1-8)
Na. 2: Mika 4:1-12
Na. 3: Ibada Ambayo Mungu Hukubali (kl-SW kur. 43-45 maf. 1-5)
Na. 4: Hakuna Sehemu ya Mtu Iliyo Roho Inayoendelea Kuishi Baada ya Kifo cha Mwili (rs-SW uku. 263 fu. 5–uku. 264 fu. 2)
Nov. 25 Kusoma Biblia: Mika 5 hadi 7
Na. 1: Mika—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 157-158 maf. 16-19)
Na. 2: Mika 6:1-16
Na. 3: Kuyafanya Mapenzi ya Mungu (kl-SW kur. 46-47 maf. 6-10)
Na. 4: Hakuna Uwasiliano na “Roho” ya Mtu Aliyekufa (rs-SW uku. 145 maf. 1–5)
Des. 2 Kusoma Biblia: Nahumu 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Nahumu na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 158-160 maf. 1-7, 11, 12)
Na. 2: Nahumu 1:2-14
Na. 3: Mwabudu Mungu kwa Njia Yake (kl-SW uku. 48 maf. 11-13)
Na. 4: Sababu Kwa Nini Wakristo wa Kweli Hukataa Katakata Mazoea Yote ya Kuwasiliana na Ulimwengu wa Roho (rs-SW uku. 146 fu. 1)
Des. 9 Kusoma Biblia: Habakuki 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Habakuki na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 161-163 maf. 1-5, 12-14)
Na. 2: Habakuki 1:12–2:8
Na. 3: Jilinde Dhidi ya Kumchukiza Mungu (kl-SW kur. 49-50 maf. 14-17)
Na. 4: Epuka Mazoea ya Kuwasiliana na Ulimwengu wa Roho (rs-SW uku. 146 fu. 2–uku. 147 fu. 6)
Des. 16 Kusoma Biblia: Sefania 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Sefania na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 163-166 maf. 1-6, 10-12)
Na. 2: Sefania 1:7-18
Na. 3: Fuata Viwango vya Juu vya Mungu (kl-SW kur. 50-51 maf. 18, 19)
Na. 4: Usiwe Mwenye Udadisi Juu Ya Nguvu za Roho Waovu (rs-SW uku. 148 fu. 1–uku. 149 fu. 1)
Des. 23 Kusoma Biblia: Hagai 1 na 2
Na. 1: Utangulizi kwa Hagai na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 166-168 maf. 1-7, 13-16)
Na. 2: Hagai 2:6-19
Na. 3: Mpe Yehova Ibada ya Nafsi Yote (kl-SW kur. 51-52 maf. 20-22)
Na. 4: Jinsi ya Kujiweka Huru na Uvutano wa Kuwasiliana na Ulimwengu wa Roho (rs-SW uku. 149 fu. 2–uku. 150 fu. 2)
Des. 30 Pitio la Kuandika. Kamilisha Danieli 5 hadi Hagai 2