Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/97 uku. 5
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 4/97 uku. 5

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Januari 6 hadi Aprili 21, 1997. Tumia karatasi tofauti ya kuandikia majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kiburi chaweza kuwa kizuizi cha kukubali makosa yetu wenyewe na kupokea shauri. [rs-SW uku. 266 fu. 3]

2. Hakuna mamlaka yoyote duniani ambayo ingeweza kusamehe mtu dhambi hadi Yesu alipokufa na kuandaa fidia. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 4/15 uku. 29.]

3. Kwa utimizo wa Zekaria 9:2-4, Tiro liliharibiwa kabisa na Nebukadreza. [si-SW uku. 169 fu. 4]

4. Ubatizo ni uhakikisho wa wokovu. [uw-SW uku. 100 fu. 12]

5. Mungu si wa kulaumiwa kwa sababu ya “misiba-asilia” ambayo ilitabiriwa kwa siku yetu kama vile watabiri-hewa wasivyolaumika kwa sababu ya hali-hewa wanayotabiri. [rs-SW uku. 136 maf. 1-3]

6. Dhambi zote za wanadamu wasio wakamilifu zinafunikwa kwa fidia. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 12/15 uku. 29.]

7. Miongoni mwa “mbuzi” wanaotajwa kwenye Mathayo 25:31-46, ambao watapata uharibifu wa milele, watakuwa washiriki watendaji wa Babiloni Mkubwa na viongozi wao wa kidini. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 10/15 uku. 26 maf. 13-15.]

8. Maneno ya Yesu yaliyorekodiwa kwenye Mathayo 23:33 yaonyesha kwamba waandishi na Mafarisayo, wakiwa kikundi, walikuwa sehemu ya mbegu ya Nyoka. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 6/1 uku. 11 fu. 11.]

9. Kusamehe wengine hufungulia njia dhambi zetu zisamehewe na Mungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 9/15 uku. 7.]

10. Ubatizo wa Yesu katika kifo ulianza 29 W.K., nao haukumalizika mpaka alipokufa hakika na kufufuliwa. [uw-SW uku. 97 fu. 6]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Ni katika maana gani Ufalme wa Yesu hautaangamizwa? (Dan. 7:14) [uw-SW uku. 86 fu. 15]

12. Ni mafungu gani mawili yaliyotimizwa na Yesu Kristo yanayofafanuliwa kwenye Zekaria 6:12, 13? [si-SW uku. 172 fu. 25]

13. Badala ya kulaumu wale ambao huenda tukaona wanaweza kufanya zaidi katika utumishi wa Ufalme, twapaswa kufanya nini sisi wenyewe? (Gal. 6:4) [uw-SW uku. 93 fu. 13]

14. Binadamu wananufaikaje kutokana na dhabihu ya Yesu wakati huu? [kl-SW kur. 68-69 maf. 17-19]

15. Kwa nini Mungu hakumsamehe Adamu na kusahau tu dhambi yake? [rs-SW uku. 135 fu. 2]

16. Ni katika maana gani “Eliya nabii” alitokea katika karne ya kwanza, kwa utimizo wa Malaki 4:5? [si-SW uku. 174 fu. 15]

17. Mtu aweza kumwibiaje Mungu? (Mal. 3:8) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 4/15 uku. 18 fu. 15.]

18. Ni wapi katika kitabu cha Mathayo tupatapo shauri zito ambalo Yesu alitoa la kutatua matatizo mazito? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 7/15 uku. 22.]

19. “Dinari” inayotajwa katika mfano wa Yesu uliorekodiwa kwenye Mathayo 20:1-16 ni nini? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona gt-SW 97 fu. 6.]

20. Kwa nini twaweza kusema kwa usahihi kwamba si kuteseka kote kwa binadamu kunakosababishwa moja kwa moja na Ibilisi pamoja na roho wake waovu? (Mit. 1:30-33; Gal. 6:7) [rs-SW uku. 132 fu. 1]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Gospeli tatu za kwanza mara nyingi huitwa sainoptiki, kumaanisha “ ___________________ .” [si-SW uku. 175 fu. 3]

22. Ikiwa mtu anayedai kuwa na roho ya Mungu hatokezi _________________________ ya roho maishani mwake na hajitengi na _________________________ na mazoea yao, dai lake halina msingi. [rs-SW uku. 238 fu. 5-uku. 239 fu. 2]

23. Wafu wanaorejezewa kwenye Ufunuo 20:12 watahukumiwa kulingana na matendo yao waliyofanya _________________________ ya ufufuo wao. Hilo latusaidia tung’amue kwamba ufufuo wao hautakuwa kwa lazima ufufuo wa _________________________ . (Yn. 5:28, 29) [uw-SW uku. 75 fu. 12]

24. Ijapokuwa Yesu kwa kweli hakupewa jina la kibinafsi _________________________ , daraka lake akiwa binadamu lilitimiza _________________________ ya jina hilo. (Isa. 7:14; Mt. 1:22, 23) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 1/15 uku. 22.]

25. Ile “roho” inayowatoka wanadamu wakati wa kifo ni ile _________________________ ambayo hutokana na Mungu. (Zab. 146:4) [kl-SW uku. 81 maf. 5-6]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Kuna uthibitisho wa kwamba Mathayo aliandika Gospeli yake katika (Kiebrania; Kiaramu; Kigiriki) na baadaye akaitafsiri katika (Kiebrania; Kiaramu; Kigiriki). [si-SW uku. 176 fu. 6]

27. Walio wengi wa (mabaki; 144,000) wako mbinguni, na (mabaki; 144,000), ambao wangali duniani, hufanyiza (Baraza Linaloongoza; jamii ya mtumwa mwaminifu mwenye akili). [uw-SW uku. 80 fu. 7]

28. Mhubiri 9:11 hutusaidia kung’amua kwamba mara nyingi watu huumia na kuteseka kwa sababu ya (Ibilisi; watu waovu; tukio, kuwa mahali fulani kwa wakati mbaya). [rs-SW uku. 133 fu. 1]

29. Ubatizo “kwa jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu,” ulianza katika (29 W.K.; 33 W.K.; 36 W.K.) (Mt. 28:19, NW) [uw-SW uku. 98 fu. 9]

30. Yesu akaja kuwa Mesiya wakati wa (kuzaliwa kwake; kubatizwa; kufufuliwa), ambako kulikuwa mwaka (2 K.W.K.; 29 W.K.; 33 W.K.) [kl-SW uku. 65 fu. 12]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Zek. 4:6; Mt. 4:8-10; Mt. 16:19; Flp. 1:9-11; Ebr. 13:5, 6

31. Tunapaswa kutumia maisha yetu katika njia inayoonyesha kwamba twaelewa kikweli mambo yaliyo ya maana zaidi. [uw-SW uku. 91 fu. 9]

32. Wafuasi wa kweli wa Yesu hukataa kujiingiza katika mambo ya kisiasa ya ulimwengu huu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 5/1 uku. 12 fu. 9.]

33. Ujuzi kuhusu Ufalme wa Mungu ungefungulia Wayahudi, Wasamaria, na Wasio Wayahudi njia ya kwenda mbinguni. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 3/15 uku. 5.]

34. Upinzani wa ulimwenguni pote kuelekea kazi yetu ya kuhubiri umeshindwa, si kwa jitihada za kibinadamu, bali kwa mwelekezo na ulinzi wa Yehova. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 8/15 uku. 17 fu. 4.]

35. Kujapokuwa bei zilizo juu na ongezeko la ukosefu wa kazi ya kuajiriwa, Yehova atahakikisha kwamba tuna yale tunayohitaji hasa. [uw-SW uku. 89 fu. 6]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki