Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1998
Maagizo
Wakati wa 1998, ifuatayo itakuwa ndiyo mipango wakati wa kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu [jv-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele [kl-SW], Siri ya Kupata Furaha ya Familia [ fy-SW], na “Vichwa vya Biblia vya Mazungumzo” kama vipatikanavyo katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya [td-SW], vitakuwa msingi wa migawo.
Shule yapaswa kuanza KWA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha kisha kuendelea kama ifuatavyo:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma, nao utategemea habari katika Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Unapotegemea kitabu Wapiga-Mbiu, mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 15 bila pitio la mdomo; unapotegemea kitabu “Kila Andiko,” wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika kichapo hicho. Lengo lapaswa kuwa si kuzungumza juu ya habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumzwa, ukikazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa chapasa kitumiwe.
Ndugu wanaogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa ni lazima, au ikiwa msemaji ameomba shauri.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA USOMAJI WA BIBLIA: Dakika 6. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma atakayeitumia habari vya kufaa kuhusu mahitaji ya kwao. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Pitio la ujumla la sekunde 30 hadi 60 la sura ambazo zimegawiwa laweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani hiyo habari ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi watakaporuhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
MGAWO NA. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa habari iliyo mgawo utakaotolewa na ndugu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika shule kubwa na pia katika vikundi visaidizi vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha kuruhusu wanafunzi watoe habari yenye maelezo mafupi katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyogawiwa yapasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa isomwe haifuatani mfululizo, mwanafunzi aweza kutaja mstari mahali ambapo usomaji waendelea.
MGAWO NA. 3: Dakika 5. Dada atagawiwa mgawo huu. Habari za utoaji huu zitategemea kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele, Siri ya Kupata Furaha ya Familia au “Vichwa vya Biblia vya Mazungumzo” kama vipatikanavyo katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Mwanafunzi anayegawiwa sehemu hii apaswa awe anajua kusoma naye apaswa kujitahidi kupatanisha kichwa na habari ya mgawo iwe katika kikao chenye kutumika, hasa kile kinachohusisha utumishi wa shambani au ushahidi wa vivi hivi. Anapotoa habari hii, mwanafunzi aweza akawa ama ameketi ama amesimama. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini msaidizi wa ziada aweza kutumiwa. Si kikao kinachopasa kupewa uangalifu mkuu, bali ni matumizi ya habari yenye matokeo.
MGAWO NA. 4: Dakika 5. Mgawo huu unapotegemea habari katika “Vichwa vya Biblia vya Mazungumzo” kama vipatikanavyo katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya, utagawiwa ndugu au dada. Unapogawiwa ndugu, huu wapaswa uwe hotuba kwa wasikilizaji wote. Kwa kawaida itafaa zaidi kwa huyo ndugu kutayarisha hotuba yake akifikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Dada anapopewa sehemu hii, yapasa itolewe kama vile ilivyoonyeshwa kwa Mgawo Na. 3. Unapotegemea kitabu Furaha ya Familia, utagawiwa ndugu. Kwa kila mgawo kumewekwa kichwa katika ratiba.
*RATIBA YA KUONGEZEA YA USOMAJI WA BIBLIA: Hii imeongezwa katika mabano baada ya namba ya wimbo ya kila juma. Kwa kufuata ratiba hii, kusoma karibu kurasa kumi kila juma, Biblia yote nzima yaweza kusomwa kwa miaka mitatu. Sehemu katika programu ya shule au pitio la kuandika hazitegemei ratiba ya kuongezea ya usomaji wa Biblia.
TAARIFA: Kwa habari ya kuongezea na maagizo kuhusu shauri, wakati, mapitio ya kuandika, na utayarishaji wa migawo, tafadhali ona ukurasa wa 3 wa Huduma ya Ufalme Yetu ya Oktoba 1996.
RATIBA
Jan. 5 Usomaji wa Biblia: Matendo 7-8
Na. 1: Ndugu Waliojitoa Wachapa na Kujalidi Vitabu (jv-SW uku. 579 fu. 3–uku. 586 fu. 4)
Na. 2: Matendo 7:44-60
Na. 3: Sikuzote Tii Mamlaka Iliyo Kuu Kuliko Zote (kl-SW uku. 130-131 fu. 1-6)
Na. 4: td-SW 44B Kwa Nini Ni Lazima Tumwamini Yesu Kristo
Jan. 12 Usomaji wa Biblia: Matendo 9-10
Na. 1: Upanuzi Baada ya Vita ya Ulimwengu ya 2 (jv-SW uku. 588 fu. 1–uku. 596 fu. 1)
Na. 2: Matendo 9:1-16
Na. 3: Tii Mamlaka Zilizo Kubwa (kl-SW uku. 131-133 fu. 7-10)
Na. 4: td-SW 34A Mambo Ambayo Ufalme wa Mungu Utafanyia Wanadamu
Jan. 19 Usomaji wa Biblia: Matendo 11-13
Na. 1: Mifumo ya Kompyuta Yasaidia Kusongeza Mbele Habari Njema (jv-SW uku. 596 fu. 2–uku. 602 fu. 3)
Na. 2: Matendo 13:1-12
Na. 3: Tambua Mpango wa Mungu wa Mamlaka Katika Familia (kl-SW uku. 134-136 fu. 11-18)
Na. 4: td-SW 34C Ufalme wa Mungu Hauji Kupitia Jitihada za Mwanadamu
Jan. 26 Usomaji wa Biblia: Matendo 14-16
Na. 1: Wahubiri na Wagawanyaji wa Biblia Wenye Bidii (jv-SW uku. 603 fu. 1–uku. 607 fu. 4)
Na. 2: Matendo 16:1-15
Na. 3: Mamlaka Katika Kutaniko—Uandalizi Wenye Upendo Kutoka kwa Yehova (kl-SW uku. 137-139 fu. 19-25)
Na. 4: td-SW 30B Uwe Macho Kuelekea Ishara za Siku za Mwisho
Feb. 2 Usomaji wa Biblia: Matendo 17-19
Na. 1: Kutokeza Biblia New World Translation (jv-SW uku. 607 fu. 5–uku. 615 fu. 5)
Na. 2: Matendo 18:1-11
Na. 3: Jinsi Ambavyo Uaminifu-Mshikamanifu Huchangia Ndoa Yenye Furaha (kl-SW uku. 140-141 fu. 1-6)
Na. 4: td-SW 36B Si Kila Mtu Atakayeenda Mbinguni
Feb. 9 Usomaji wa Biblia: Matendo 20-21
Na. 1: Kutahini na Kupepeta Kuanzia Ndani (jv-SW uku. 618 fu. 1–uku. 623 fu. 3)
Na. 2: Matendo 21:1-14
Na. 3: Fungu Muhimu la Uwasiliano Katika Ndoa (kl-SW uku. 142-143 fu. 7-9)
Na. 4: td-SW 26A Muungano wa Ndoa Lazima Uheshimike
Feb. 16 Usomaji wa Biblia: Matendo 22-24
Na. 1: Badiliko Katika Usimamizi Latahini Sana (jv-SW uku. 623 fu. 4–uku. 629 fu. 2)
Na. 2: Matendo 22:1-16
Na. 3: Onyesha Heshima na Staha kwa Mwenzi Wako (kl-SW uku. 143-144 fu. 10-14)
Na. 4: td-SW 26C Daraka la Wazazi Wakristo kwa Watoto
Feb. 23 Usomaji wa Biblia: Matendo 25-26
Wimbo Na. 179 [*Mwanzo 50–Kutoka 1-7]
Na. 1: Marekebisho Katika Maoni ya Mafundisho na Matarajio (jv-SW uku. 629 fu. 3–uku. 633 fu. 4)
Na. 2: Matendo 25:1-12
Na. 3: Weka Kielelezo Kizuri na Uwaonyeshe Watoto Wako Upendo (kl-SW uku. 145-146 fu. 15-18)
Na. 4: td-SW 26E Wakristo wa Kweli Hawaoi Wake Wengi
Mac. 2 Usomaji wa Biblia: Matendo 27-28
Na. 1: Matendo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 204-205 fu. 32-40)
Na. 2: Matendo 27:33-44
Na. 3: Kile Ambacho Nidhamu Yenye Upendo na Mwelekezo Wenye Ustadi Waweza Kutimiza (kl-SW uku. 148-149 fu. 19-23)
Na. 4: td-SW 9B Biblia Huonyesha Kwamba Maria Hakuwa “Bikira Daima”
Mac. 9 Usomaji wa Biblia: Waroma 1-3
Na. 1: Utangulizi kwa Waroma (si-SW uku. 205-206 fu. 1-7)
Na. 2: Waroma 1:18-32
Na. 3: Sababu kwa Nini Twataka Kumkaribia Mungu (kl-SW uku. 150-151 fu. 1-5)
Na. 4: td-SW 37B Sherehe ya Misa Si ya Kimaandiko
Mac. 16 Usomaji wa Biblia: Waroma 4-6
Na. 1: Matarajio, Uhalisi, na Masuala Mengine (jv-SW uku. 635 fu. 1–uku. 641 fu. 3)
Na. 2: Waroma 4:1-15
Na. 3: Matakwa ya Kumkaribia Mungu (kl-SW uku. 152-153 fu. 6-9)
Na. 4: td-SW 22B Sifa za Ustahili kwa Ajili ya Huduma
Mac. 23 Usomaji wa Biblia: Waroma 7-9
Na. 1: “Nanyi Mtakuwa Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote” (jv-SW uku. 642 fu. 1–uku. 646 fu. 3)
Na. 2: Waroma 9:1-18
Na. 3: Ongea na Mungu Naye Akusikie (kl-SW uku. 153-155 fu. 10-14)
Na. 4: td-SW 39B Mke Hapaswi Kuruhusu Mume Wake Amtenge na Mungu
Mac. 30 Usomaji wa Biblia: Waroma 10-12
Na. 1: Unafiki wa Viongozi wa Kidini Wafunuliwa Wazi (jv-SW uku. 647 fu. 1–uku. 651 fu. 4)
Na. 2: Waroma 10:1-15
Na. 3: Dumu Katika Sala na Usikilize (kl-SW uku. 156-159 fu. 15-20)
Na. 4: td-SW 29A Sala Ambazo Mungu Husikia
Apr. 6 Usomaji wa Biblia: Waroma 13-16
Wimbo Na. 175 [*Kutoka 40–Mambo ya Walawi 1-7]
Na. 1: Waroma—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 209 fu. 20-25)
Na. 2: Waroma 13:1-10
Na. 3: Pata Usalama wa Kweli Miongoni mwa Watu wa Mungu (kl-SW uku. 160-161 fu. 1-4)
Na. 4: td-SW 11A Binadamu Hakuamuliwa Kimbele Yatakayompata
Apr. 13 Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 1-3
Wimbo Na. 173 [*Mambo ya Walawi 8-13]
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Wakorintho (si-SW uku. 210-211 fu. 1-7)
Na. 2: 1 Wakorintho 1:10-25
Na. 3: Jinsi Ambavyo Yehova Huandaa Chakula cha Kiroho (kl-SW uku. 162-163 fu. 5-8)
Na. 4: td-SW 6B Sababu kwa Nini Yesu Ndiye Angeweza Kulipia Fidia
Apr. 20 Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 4-6
Wimbo Na. 56 [*Mambo ya Walawi 14-19]
Na. 1: Uvutano wa Makasisi Waonekana Dhahiri (jv-SW uku. 652 fu. 1–uku. 658 fu. 4)
Na. 2: 1 Wakorintho 4:1-13
Na. 3: Kinachomaanishwa na Kujivika Upendo (kl-SW uku. 163-166 fu. 9-14)
Na. 4: td-SW 4B Je, Ni Makosa Kushutumu Mafundisho Yasiyo ya Kweli?
Apr. 27 Pitio la Kuandika. Kamilisha Matendo 7-28 Ro 1-16–1 Wakorintho 1-6
Wimbo Na. 91 [*Mambo ya Walawi 20-25]
Mei 4 Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 7-9
Wimbo Na. 29 [*Mambo ya Walawi 26-27–Hesabu 1-3]
Na. 1: Makasisi na Hitler Dhidi ya Watumishi wa Yehova (jv-SW uku. 659 fu. 1–uku. 665 fu. 1)
Na. 2: 1 Wakorintho 7:10-24
Na. 3: Kutaniko—Mahali pa Usalama (kl-SW uku. 167-169 fu. 15-20)
Na. 4: td-SW 4D Je, Mungu Aona Wema Katika Dini Zote?
Mei 11 Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 10-12
Na. 1: Upinzani wa Ulimwenguni Pote kwa Sababu ya Kumpa Yehova Ujitoaji Usiohusisha Wengine (jv-SW uku. 665 fu. 2–uku. 673 fu. 1)
Na. 2: 1 Wakorintho 11:1-16
Na. 3: Mwige Yesu—Umtumikie Mungu Milele (kl-SW uku. 170-171 fu. 1-6)
Na. 4: td-SW 35B Wafu Watafufuliwa Kwenda Wapi?
Mei 18 Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 13-14
Na. 1: Wachukiwa kwa Sababu “Wao Si Sehemu ya Ulimwengu” (jv-SW uku. 673 fu. 2–uku. 677 fu. 3)
Na. 2: 1 Wakorintho 14:1-12
Na. 3: Hatua Muhimu Zinazoongoza Kwenye Uhai (kl-SW uku. 173-175 fu. 7-9)
Na. 4: td-SW 16B Kurudi kwa Kristo Hutambuliwa kwa Mambo ya Hakika Yenye Kuonekana
Mei 25 Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 15-16
Na. 1: 1 Wakorintho—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 213-214 fu. 23-26)
Na. 2: 1 Wakorintho 16:1-13
Na. 3: Sababu kwa Nini Ubatizo Ni wa Lazima (kl-SW uku. 175-176 fu. 10-12)
Na. 4: td-SW 28B Sheria ya Sabato Haikupewa Wakristo
Juni 1 Usomaji wa Biblia: 2 Wakorintho 1-4
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Wakorintho (si-SW uku. 214 fu. 1-4)
Na. 2: 2 Wakorintho 4:1-12
Na. 3: Ubatizo—Hatua ya Maana Zaidi Katika Maisha Yako (kl-SW uku. 177 fu. 13-16)
Na. 4: td-SW 42A Mungu Hutoa Wokovu Kupitia Kristo Pekee
Juni 8 Usomaji wa Biblia: 2 Wakorintho 5-8
Na. 1: Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema (jv-SW uku. 678 fu. 1–uku. 683 fu. 4)
Na. 2: 2 Wakorintho 7:1-13
Na. 3: Kinachomaanishwa na Kuishi Kulingana na Wakfu na Ubatizo Wako (kl-SW uku. 178-180 fu. 17-22)
Na. 4: td-SW 42C “Wokovu wa Ulimwengu Wote Mzima” Sio wa Kimaandiko
Juni 15 Usomaji wa Biblia: 2 Wakorintho 9-13
Wimbo Na. 43 [*Hesabu 36–Kumbukumbu la Torati 1-4]
Na. 1: 2 Wakorintho—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 216-217 fu. 18-20)
Na. 2: 2 Wakorintho 10:1-12
Na. 3: Kujitayarisha Sasa kwa Ajili ya “Uhai Ulio Kwelikweli” (kl-SW uku. 181-182 fu. 1-5)
Na. 4: td-SW 3B Sababu kwa Nini Wanadamu Wote Huteseka Kutokana na Dhambi ya Adamu
Juni 22 Usomaji wa Biblia: Wagalatia 1-3
Wimbo Na. 127 [*Kumbukumbu la Torati 5-11]
Na. 1: Utangulizi kwa Wagalatia (si-SW uku. 217-218 fu. 1-6)
Na. 2: Wagalatia 1:1-12
Na. 3: Baada ya Har–Magedoni—Dunia Paradiso (kl-SW uku. 182-184 fu. 6-11)
Na. 4: td-SW 3D Dhambi Dhidi ya Roho Takatifu Ni Nini?
Juni 29 Usomaji wa Biblia: Wagalatia 4-6
Wimbo Na. 98 [*Kumbukumbu la Torati 12-19]
Na. 1: Wagalatia—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 219-220 fu. 14-18)
Na. 2: Wagalatia 6:1-18
Na. 3: Amani Kila Mahali na Ufufuo wa Wafu (kl-SW uku. 184-187 fu. 12-18)
Na. 4: td-SW 25B Nafsi na Roho Zatofautianaje?
Jul. 6 Usomaji wa Biblia: Waefeso 1-3
Wimbo Na. 71 [*Kumbukumbu la Torati 20-27]
Na. 1: Utangulizi kwa Waefeso (si-SW uku. 220-221 fu. 1-8)
Na. 2: Waefeso 1:1-14
Na. 3: Kitakachomaanishwa na Ukamilifu, na Jinsi Tutakavyoufurahia (kl-SW uku. 187-191 fu. 19-25)
Na. 4: td-SW 27B Kani ya Uhai ya Mwanadamu na Mnyama Huitwa Roho
Jul. 13 Usomaji wa Biblia: Waefeso 4-6
Wimbo Na. 214 [*Kumbukumbu la Torati 28-32]
Na. 1: Waefeso—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 223 fu. 16-19)
Na. 2: Waefeso 6:1-13
Na. 3: td-SW 27C Sababu kwa Nini Wakristo wa Kweli Huepuka Aina Zote za Uwasiliani-Roho
Na. 4: Familia Ina Tatizo (fy-SW uku. 1-9 fu. 1-14)
Jul. 20 Usomaji wa Biblia: Wafilipi 1-4
Wimbo Na. 123 [*Kumbukumbu la Torati 33-34–Yoshua 1-6]
Na. 1: Utangulizi kwa Wafilipi na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 223-224 fu. 1-7; uku. 225-226 fu. 12-14)
Na. 2: Wafilipi 1:1-14
Na. 3: Siri ya Kupata Furaha ya Familia (fy-SW uku. 10-12 fu. 15-23)
Na. 4: td-SW 40C Jinsi Mungu na Kristo Walivyo Mmoja
Jul. 27 Usomaji wa Biblia: Wakolosai 1-4
Na. 1: Utangulizi kwa Wakolosai na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 226-227 fu. 1-5; uku. 228 fu. 12-14)
Na. 2: Wakolosai 4:1-13
Na. 3: td-SW 40D Roho Takatifu Ni Kani ya Mungu ya Utendaji
Na. 4: Je, Uko Tayari kwa Ndoa? (fy-SW uku. 13-15 fu. 1-6)
Ago. 3 Usomaji wa Biblia: 1 Wathesalonike 1-5
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Wathesalonike na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 229 fu. 1-5; uku. 231 fu. 13-15)
Na. 2: 1 Wathesalonike 2:1-12
Na. 3: Sababu kwa Nini Yakupasa Ujijue Mwenyewe na Kuwa Mwenye Busara (fy-SW uku. 16-18 fu. 7-10)
Na. 4: td-SW 38C Nufaika na Rehema ya Mungu
Ago. 10 Usomaji wa Biblia: 2 Wathesalonike 1-3
Wimbo Na. 10 [*Yoshua 20-24–Waamuzi 1]
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Wathesalonike na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 232 fu. 1-4; uku. 233 fu. 10-11)
Na. 2: 2 Wathesalonike 1:1-12
Na. 3: td-SW 38D Ufalme wa Mungu Ndio Tumaini Pekee la Mwanadamu
Na. 4: Mambo ya Kutafuta Katika Mwenzi wa Ndoa (fy-SW uku. 18-22 fu. 11-15)
Ago. 17 Usomaji wa Biblia: 1 Timotheo 1-3
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Timotheo (si-SW uku. 234 fu. 1-6)
Na. 2: 1 Timotheo 1:3-16
Na. 3: Mambo ya Kufikiria Kabla ya Kufanya Uwajibikaji wa Kudumu (fy-SW uku. 22-23 fu. 16-19)
Na. 4: td-SW 17C Kudumu Ukiwa Huru na Hatia ya Damu ya Watu Wote
Ago. 24 Usomaji wa Biblia: 1 Timotheo 4-6
Na. 1: 1 Timotheo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 236-237 fu. 15-19)
Na. 2: 1 Timotheo 4:1-16
Na. 3: td-SW 14A Sababu kwa Nini Mungu Hukataa Ibada ya Wazazi wa Kale
Na. 4: Dumisha Utafutaji Wenu wa Uchumba Ukiwa Wenye Kuheshimika na Tazama Mbele ya Arusi (fy-SW uku. 24-26 fu. 20-23)
Ago. 31 Pitio la Kuandika. Kamilisha 1 Wakorintho 7-16; 2Co 1-13; Gal 1-6; Efe 1-6; Flp 1-4; Kol 1-4; 1Th 1-5; 2Th 1-3–1 Timotheo 1-6
Sept. 7 Usomaji wa Biblia: 2 Timotheo 1-4
Wimbo Na. 46 [*Waamuzi 20-21–Ruthu 1-4]
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Timotheo na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 237-238 fu. 1-4; uku. 238-239 fu. 10-12)
Na. 2: 2 Timotheo 3:1-13
Na. 3: Kanuni za Biblia Ambazo Zaweza Kukusaidia Ujitayarishe kwa Ndoa Yenye Mafanikio (fy-SW uku. 26 sanduku la pitio)
Na. 4: td-SW 7B Har–Magedoni Haivunji Upendo wa Mungu
Sept. 14 Usomaji wa Biblia: Tito 1-3–Filemoni 1-25
Wimbo Na. 155 [*1 Samweli 1-8]
Na. 1: Utangulizi kwa Tito na Filemoni na Kwa Nini Ni Vyenye Mafaa (si-SW uku. 239-241 fu. 1-4, 8-10; uku. 241-243 fu. 1-4, 7-10)
Na. 2: Tito 3:1-14
Na. 3: td-SW 33A Ubatizo Ni Takwa la Kikristo
Na. 4: Ufunguo wa Kwanza Uongozao Kwenye Ndoa Yenye Kudumu (fy-SW uku. 27-29 fu. 1-6)
Sept. 21 Usomaji wa Biblia: Waebrania 1-3
Wimbo Na. 149 [*1 Samweli 9-14]
Na. 1: Utangulizi kwa Waebrania (si-SW uku. 243-244 fu. 1-9)
Na. 2: Waebrania 3:1-15
Na. 3: Ufunguo wa Pili Uongozao Kwenye Ndoa Yenye Kudumu (fy-SW uku. 30-31 fu. 7-10)
Na. 4: td-SW 1B Biblia Ni Yenye Kutumika kwa Siku Yetu
Sept. 28 Usomaji wa Biblia: Waebrania 4-7
Wimbo Na. 3 [*1 Samweli 15-19]
Na. 1: Vita vya Kisheria vya Uhuru wa Ibada (jv-SW uku. 684 fu. 1–uku. 693 fu. 1)
Na. 2: Waebrania 6:1-12
Na. 3: td-SW 1C Biblia Ni Kitabu kwa Ajili ya Wanadamu Wote
Na. 4: Ukichwa wa Mwanamume Lazima Uwe Kama wa Kristo (fy-SW uku. 31-33 fu. 11-15)
Okt. 5 Usomaji wa Biblia: Waebrania 8-10
Wimbo Na. 209 [*1 Samweli 20-25]
Na. 1: Kumtumikia Yehova Bila Hofu na kwa Muungano Ujapokuwa Upinzani (jv-SW uku. 693 fu. 2–uku. 699 fu. 4))
Na. 2: Waebrania 8:1-12
Na. 3: Jinsi Mke Anavyopaswa Kumkamilisha Mume Wake (fy-SW uku. 34-35 fu. 16-19)
Na. 4: td-SW 32A Nyakati za Wasio Wayahudi Zilikoma 1914
Okt. 12 Usomaji wa Biblia: Waebrania 11-13
Wimbo Na. 108 [*1 Samweli 26-31–2 Samweli 1-2]
Na. 1: Waebrania—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 247 fu. 23-27)
Na. 2: Waebrania 11:1-10
Na. 3: td-SW 12A Kanisa la Kweli la Kristo
Na. 4: Kinachomaanishwa kwa Kweli na Uwasiliano Mzuri (fy-SW uku. 35-38 fu. 20-26)
Okt. 19 Usomaji wa Biblia: Yakobo 1-5
Wimbo Na. 144 [*2 Samweli 3-10]
Na. 1: Utangulizi kwa Yakobo na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 248-249 fu. 1-7; uku. 250 fu. 15-17)
Na. 2: Yakobo 5:1-12
Na. 3: Kanuni za Biblia Zinazoweza Kukusaidia Ufurahie Ndoa Idumuyo, Yenye Furaha (fy-SW uku. 38 sanduku la pitio)
Na. 4: td-SW 41B Je, Siku za Uumbaji Zilikuwa Siku Zenye Urefu wa Saa 24?
Okt. 26 Usomaji wa Biblia: 1 Petro 1-5
Wimbo Na. 54 [*2 Samweli 11-15]
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Petro na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 251-252 fu. 1-5; uku. 253 fu. 11-13)
Na. 2: 1 Petro 4:1-11
Na. 3: td-SW 24A Je, Yesu Alikufa Msalabani?
Na. 4: Ishi Kulingana na Mapato Yako (fy-SW uku. 39-41 fu. 1-6)
Nov. 2 Usomaji wa Biblia: 2 Petro 1-3
Wimbo Na. 177 [*2 Samweli 16-20]
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Petro na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 254 fu. 1-3; uku. 255 fu. 8-10)
Na. 2: 2 Petro 3:1-13
Na. 3: Kutunza Watu wa Nyumbani Ni Mradi wa Familia (fy-SW uku. 42-44 fu. 7-11)
Na. 4: td-SW 13B Ni Nini Iliyo Hali ya Wafu?
Nov. 9 Usomaji wa Biblia: 1 Yohana 1-5
Wimbo Na. 114 [*2 Samweli 21-24–1 Wafalme 1]
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Yohana na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 256-257 fu. 1-5; uku. 258 fu. 11-13)
Na. 2: 1 Yohana 5:1-12
Na. 3: td-SW 13C Kwa Nini Haiwezekani Kuongea na Wafu
Na. 4: Sababu kwa Nini Yehova Anataka Tuwe Safi (fy-SW uku. 45-49 fu. 12-20)
Nov. 16 Usomaji wa Biblia: 2 Yohana 1-13; 3Jo 1-14–Yuda 1-25
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Yohana, 3 Yohana, na Yuda na Kwa Nini Ni Vyenye Mafaa (si-SW uku. 259 fu. 1-3, 5; uku. 260-261 fu. 1-3, 5; uku. 261-263 fu. 1-4, 8-10)
Na. 2: 2 Yohana 1:1-13
Na. 3: Kile Ambacho Pongezi na Shukrani ya Moyo Mweupe Chaweza Kufanyia Familia (fy-SW uku. 49-50 fu. 21-22)
Na. 4: td-SW 10C Roho Waovu Ni Nani?
Nov. 23 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 1-3
Wimbo Na. 195 [*1 Wafalme 7-10]
Na. 1: Utangulizi kwa Ufunuo (si-SW uku. 263-264 fu. 1-6)
Na. 2: Ufunuo 3:1-11
Na. 3: td-SW 5A Kusudi la Mungu kwa Dunia Ni Nini?
Na. 4: Maoni ya Biblia Kuhusu Watoto na Daraka la Familia (fy-SW uku. 51-52 fu. 1-5)
Nov. 30 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 4-6
Wimbo Na. 203 [*1 Wafalme 11-15]
Na. 1: Dini Moja ya Kweli, Iliyochaguliwa na Mungu (jv-SW uku. 704 fu. 1–uku. 706 fu. 4)
Na. 2: Ufunuo 5:1-12
Na. 3: Kinachomaanishwa na Kutimiza Mahitaji ya Mtoto (fy-SW uku. 53-55 fu. 6-9)
Na. 4: td-SW 15A Kwa Nini Kuponya kwa Kiroho Ni kwa Maana Sana
Des. 7 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 7-9
Wimbo Na. 200 [*1 Wafalme 16-20]
Na. 1: Yehova Abariki Wale Ambao Hutumia Ile Kweli Maishani Mwao (jv-SW uku. 707 fu. 1–uku. 709 fu. 5)
Na. 2: Ufunuo 8:1-13
Na. 3: td-SW 15B Ufalme wa Mungu Utaleta Maponyo ya Kimwili Yenye Kudumu
Na. 4: Kaza Kweli Kikiki Katika Mtoto Wako (fy-SW uku. 55-57 fu. 10-15)
Des. 14 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 10-12
Wimbo Na. 137 [*1 Wafalme 21-22–2 Wafalme 1-3]
Na. 1: Alama Yenye Kutambulisha Wanafunzi wa Yesu wa Kweli (jv-SW uku. 710 fu. 1–uku. 712 fu. 3)
Na. 2: Ufunuo 10:1-11
Na. 3: Fundisha Mtoto Wako Njia za Yehova (fy-SW uku. 58-59 fu. 16-19)
Na. 4: td-SW 20A Ni 144,000 Tu Waendao Mbinguni
Des. 21 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 13-15
Na. 1: Watumishi Wote wa Kweli wa Mungu Lazima Wafulize Kulinda (jv-SW uku. 713 fu.1-uku. 716 fu. 4)
Na. 2: Ufunuo 13:1-15
Na. 3: td-SW 8A Helo Si Mahali pa Mateso ya Moto
Na. 4: Uhitaji Muhimu wa Nidhamu Katika Namna Zake Tofauti-Tofauti (fy-SW uku. 59-61 fu. 20-23)
Des. 28 Pitio la Kuandika. Kamilisha 2 Timotheo 1-4; Tit 1-3; Flm 1-25; Ebr 1-13; Yak 1-5; 1Pe 1-5; 2Pe 1-3; 1Yo 1-5; 2Yo 1-13; 3Yo 1-14; Juda 1-25–Ufunuo 15
Wimbo Na. 212 [*2 Wafalme 10-15]