Habari Za Kitheokrasi
Majumba ya Ufalme: Programu ya pekee ya ujenzi wa Majumba ya Ufalme katika Rwanda imefanya maendeleo vizuri sana. Kati ya Majumba ya Ufalme 38 ambayo yamekubaliwa kujengwa, 17 yako karibu kumalizika.
Jumba la Ufalme la Nairobi Dandora liliwekwa wakfu hivi majuzi.
Baadhi ya Mambo Makuu Kutoka Ripoti ya Kila Mwaka: Nchi zote zilizo chini ya ofisi ya tawi ya Kenya zilikuwa na utendaji mzuri sana. Kila moja ya hizo nchi ilikuwa na ongezeko la asilimia 10 au zaidi katika idadi ya wahubiri: Kenya asilimia 11; Rwanda asilimia 32; Sudan asilimia 10; Tanzania asilimia 11; na Uganda asilimia 17. Kama uwezavyo kuona katika ripoti ya utumishi wa shambani ya Agosti, tulifunga mwaka wa utumishi wa 1997 kwa vilele vipya katika idadi ya wahubiri. Kulikuwa na maendeleo mazuri katika maangusho ya magazeti na utendaji wa painia-msaidizi. Hesabu ya jumla ya waliobatizwa katika nchi zote zilizo chini ya ofisi ya tawi ya Kenya ilikuwa 3,915. Ndiyo, twawapongeza nyinyi ndugu wapendwa kwa utendaji wenu mzuri wa shambani. Tutazamiapo kwa hamu matimizo ya mwaka wa utumishi wa 1998, na twendelee kumtolea Yehova utumishi mtakatifu kwa bidii.—Ufu. 7:15.
Hudhurio la Ukumbusho la 1997:
Kenya: 35,236
Rwanda: 20,121
Tanzania: 22,448
Uganda: 7,603