Habari Za Kitheokrasi
◼ Nchi za Afrika Magharibi za Benin, Côte d’Ivoire, Ghana, Kamerun, Liberia, na Nigeria zote hizo zilifikia vilele vipya vya wahubiri katika Februari.
◼ Wakimbizi wengi wamekuwa wakirudi Liberia, na kuna njaa kubwa ya kweli katika nchi hiyo. Kilele chao cha Februari cha wahubiri 2,286 kiliripoti mafunzo ya Biblia nyumbani 6,277.
◼ Macao ilikuwa na ongezeko la asimilia 16 kuliko wastani wa mwaka jana, 135 wakiripoti katika Februari.
◼ Kutoka Pasifiki ya Kusini, Fiji, Visiwa vya Solomon, na Tahiti, nchi zote hizo ziliripoti vilele vipya vya wahubiri katika Februari.
◼ Kisiwa cha Madagaska kilifikia kilele kipya cha wahubiri 9,484, ambacho kilikuwa ongezeko la asilimia 14 kuliko wastani wa mwaka jana. Pia waliripoti mafunzo ya Biblia nyumbani zaidi ya 20,000 katika Februari.
◼ Uganda iliripoti kilele kipya cha wahubiri 2,128 mwezi wa Machi 1998.