Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Mei 4 hadi Agosti 24, 1998. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Kulingana na rekodi ya Biblia, Paulo alitembelea Korintho mara tatu. [si-SW uku. 214 fu. 3]
2. Hatua za kuelekea ubatizo wa Kikristo huanza kwa kutwaa ndani ya moyo wetu ujuzi sahihi juu ya Yehova Mungu na Yesu Kristo. [kl-SW uku. 173 fu. 7]
3. Bidii ya kupita kiasi ya kuendeleza masilahi ya Ufalme haitetei ukosefu wa busara, hisia-mwenzi, na wororo tunaposhughulika na wengine. (1 Kor. 13:2, 3) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 10/15 uku. 31 fu. 5.]
4. Twaweza kuchuma uhai kwa kumtumikia Yehova Mungu. [kl-SW uku. 182 fu. 4]
5. Andiko la Wagalatia 5:26 hukataza Wakristo wa kweli mashindano yote ya michezo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona g95-SW 12/8 uku. 15 fu. 8.]
6. Paulo aliposema kwenye 2 Wakorintho 10:4 kwamba, “silaha za shughuli yetu ya vita si za kimwili,” alikuwa akikazia kwamba Wakristo hawapaswi kamwe kugeukia ujanja, lugha ya majivuno, au silaha za kimwili, ili walinde kutaniko dhidi ya mafundisho yasiyo ya kweli. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona rs-SW uku. 140 fu. 1.]
7. Barua waliyoandikiwa Wafilipi iliandikwa na Paulo miezi michache tu baada ya kuanzisha kutaniko katika Filipi, nayo ilichochewa na mfululizo wa matatizo yaliyokuwa yametokea miongoni mwao. [si-SW uku. 224 fu. 3]
8. Yesu “alitangazwa kuwa mwadilifu katika roho,” kama inavyotajwa kwenye 1 Timotheo 3:16, kwa kuthawabishwa awe na uhai wa roho alipofufuliwa; hilo lilimfanya Mungu ajulishe kwamba Yesu alikuwa mwadilifu kabisa na mwenye kustahiki migawo zaidi iliyotukuka. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 1/15 uku. 13 fu. 12.]
9. “Kule kuachiliwa” kunakotajwa kwenye Wafilipi 1:23 kwa wazi ni tazamio la Paulo la kuwa pamoja na Kristo mara baada ya kifo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 30 fu. 4.]
10. Paulo aliandika 1 Timotheo wakati wa kipindi cha kati ya kuachiliwa kwake kutoka kifungo chake cha kwanza gerezani katika Roma na kufungwa kwake gerezani kwa mwisho huko. [si-SW uku. 234 fu. 2]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Ni katika njia gani baadhi ya watu katika Korintho walikuwa wakishiriki kula mifano “isivyostahili” walipokuja pamoja ili kusherehekea Ukumbusho wa kifo cha Kristo? (1 Kor. 11:27) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 2/15 uku. 19 fu. 17.]
12. Ni kuwapo kwa nani kulikotisha hali njema ya kutaniko la Korintho, kukimchochea Paulo kuandikia Korintho barua yake ya pili? [si-SW uku. 214 fu. 2]
13. Yehova atalipiaje chochote kile ambacho huenda tukadhabihu kwa ajili ya ibada yake? [kl-SW uku. 169 fu. 20]
14. Ni nini ambacho kimetimizwa kwa kukata rufani kwenye mahakama zilizo kuu zaidi juu ya mambo yanayohusu ibada yetu ya kweli? [jv-SW uku. 683 fu. 4]
15. Katika matumizi yake ya Neno la Mungu, Paulo aliandaaje kielelezo maridadi kwa wahudumu Wakristo leo? [si-SW uku. 217 fu. 19]
16. Mtume Paulo alimaanisha nini aliposema kwamba Sheria “iliongezwa kufanya mikiuko-sheria iwe dhahiri”? (Gal. 3:19) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona uw-SW uku. 147 fu. 3-4.]
17. Kwenye Wafilipi 1:3-7, Paulo awapongeza akina ndugu kwa sababu zipi, nasi twaweza kunufaikaje kutokana na kielelezo chake? [si-SW uku. 225 fu. 12]
18. Kwa nini wahudumu wote Wakristo wapaswa kufuata shauri kwenye Wakolosai 4:6? [si-SW uku. 228 fu. 13]
19. Mtume Paulo alimaanisha nini aliposema kwamba alitamani wanawake “wajirembe wenyewe . . . na kiasi”? (1 Tim. 2:9) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona g91-SW 10/8 uku. 13 fu. 2.]
20. Kwa nini Wakristo wapaswa kutii onyo la Paulo lililo kwenye 1 Timotheo 6:4 kuhusu “mashindano juu ya maneno”? [si-SW uku. 236 fu. 15]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Mwaka wa _________________________ , mwafaka kati ya _________________________ na Nazi ya Ujerumani ulitiwa sahihi, Hitler alianzisha kampeni ya kuwaangamiza _________________________ katika Ujerumani. [jv-SW uku. 659 fu. 1]
22. Barua ya Paulo ya kwanza kwa Wakorintho ni yenye mafaa sana katika kukuza kuelewa kwetu _________________________ , ambamo yatoa mengi ya manukuu yayo. [si-SW uku. 213 fu. 23]
23. Katika barua yake kwa Wagalatia, Paulo athibitisha kwamba mtu hutetewa kuwa mwenye haki kwa kuwa na _________________________ katika Kristo Yesu, wala si kwa kazi za _________________________ , na kwamba kwa sababu hiyo haihitajiwi Wakristo _________________________ . [si-SW uku. 218 fu. 6]
24. Katika barua yake ya kwanza kwa Wathesalonike, katika pindi nne Paulo ataja _________________________ kwa Yesu Kristo, kama inavyoonekana, ni kwa sababu kutaniko lilipendezwa na fundisho hilo. [si-SW uku. 231 fu. 15]
25. Barua ya pili kwa Wathesalonike iliandikwa na _________________________ alipokuwa _________________________ katika mwaka wa _________________________ . [si-SW uku. 232 fu. 4]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Katika kuzungumzia juu ya haki yake ya kupata riziki kutokana na huduma yake, Paulo arejezea (Talmud; Mishnah; Sheria ya Musa), ambayo husema kwamba wanyama wenye kufanya kazi hawapaswi kufumbwa kinywa ili kuwazuia wasile na kwamba (Walawi; Wanethini; familia ya kikuhani ya Aroni) katika utumishi wa hekalu walipokea fungu lao kutoka kwa madhabahu. [si-SW uku. 213 fu. 24]
27. Barua ya Paulo kwa Wagalatia hutoa fasiri ya Isaya 54:1-6, ikimtambulisha mwanamke wa Yehova kuwa (Yerusalemu wa kidunia; Yerusalemu wa juu; Yerusalemu Mpya). (Gal. 4:21-26) [si-SW uku. 220 fu. 16]
28. Kwenye Waefeso 1:10, “uhudumiaji” hurejezea (Ufalme wa Kimesiya; Baraza Linaloongoza; njia ya Mungu ya kusimamia mambo yake ya nyumba). [si-SW uku. 221 fu. 8]
29. (Wageuzao watu wafuate dini ya Kiyahudi; jamii ya makasisi wa Jumuiya ya Wakristo; Babiloni Mkubwa) yaweza kutambuliwa kwa yule “mtu wa uasi-sheria” anayetajwa kwenye 2 Wathesalonike 2:3. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 1/15 uku. 18 fu. 11.]
30. Ukiwa na shaka kuhusu mtu unayetafuta uchumba naye, jambo la hekima kufanya ni (kuruhusu hisia za kimahaba zishinde shaka zako; kukatiza uhusiano; kufunga macho yako kuelekea kasoro nzito ukitumaini kwamba mambo yatakuwa nafuu baada ya ndoa). [fy-SW uku. 23 fu. 19]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
1 Kor. 10:11, 12; 2 Kor. 4:7; 2 Kor. 8:14; Flp. 4:6, 7; 2 The. 1:8, 9, 12
31. Wakati mtu awekapo huduma ya Kikristo kwanza katika maisha yake, yeye huupata uwezo ambao Mungu hutoa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 3/1 uku. 29 fu. 5.]
32. Twapaswa kutii onyo lililotolewa kuwa kielelezo cha Waisraeli wakiwa chini ya uongozi wa Musa na kuepuka kujitegemea wenyewe. [si-SW uku. 213 fu. 23]
33. Zawadi za ukarimu kutoka kwa Wakristo wenye mali ya kimwili zaweza kusaidia wale wenye uhitaji wa vitu vya kimwili, ilhali bidii ya wale wenye shida yaweza kuleta shangwe na kitia-moyo kwa wapaji. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 12/15 uku. 21 fu. 20.]
34. Lazima tusikate tamaa kuhubiri habari njema, kwa sababu kulingana na Biblia, watu wote walio hai leo ambao waendelea kuishi hadi mwisho wa mfumo huu mwovu wa mambo na ambao wanahukumiwa kuwa adui za ibada ya kweli watapata uharibifu wa milele. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 5/1 uku. 19 fu. 4.]
35. Yehova hupa shwari na utulivu miongoni mwa hali zenye majaribu sana. [Usomaji wa Biblia kila juma; w88-SW 11/1 uku. 30 fu. 19-20.]