Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/99 kur. 3-6
  • Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 2000

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 2000
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Vichwa vidogo
  • Maagizo
  • RATIBA
Huduma Yetu ya Ufalme—1999
km 10/99 kur. 3-6

Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 2000

Maagizo

Ifuatayo itakuwa ndiyo mipango wakati wa kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi mwaka wa 2000.

VYANZO VYA HABARI: Migawo itategemea Biblia, Mnara wa Mlinzi [w-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], na “Vichwa vya Biblia vya Mazungumzo” kama vipatikanavyo katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya [td-SW].

Shule yapaswa kuanza KWA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha. Hakuna haja ya kupitia yale yaliyo katika programu. Mwangalizi wa shule anapotoa utangulizi wa sehemu yake, atataja habari itakayozungumziwa. Endeleeni kama ifuatavyo:

MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa ushughulikiwe na mzee au mtumishi wa huduma, nao utategemea Mnara wa Mlinzi au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Unapotegemea Mnara wa Mlinzi, mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 15 bila pitio la mdomo; unapotegemea kitabu “Kila Andiko,” wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika kichapo hicho. Lengo halipaswi kuwa kuzungumza juu ya habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumziwa, ukikazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa chapasa kitumiwe.

Ndugu wanaogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa lazima au likiombwa na msemaji.

MAMBO MAKUU KUTOKANA NA USOMAJI WA BIBLIA: Dakika 6. Huu wapasa kushughulikiwa na mzee au mtumishi wa huduma atakayeitumia habari vya kufaa kuhusu mahitaji ya kwao. Si lazima kuwe na kichwa. Huu haupaswi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Pitio la ujumla la sekunde 30 hadi 60 la sura ambazo mgawo umetolewa laweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi watakaporuhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.

MGAWO NA. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa habari iliyo mgawo utakaotolewa na ndugu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika shule kuu na pia katika shule mbalimbali. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha kuruhusu wanafunzi watoe habari yenye maelezo mafupi katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia. Masimulizi ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyogawiwa yapasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa kusomwa haifuatani mfululizo, mwanafunzi aweza kutaja mstari ambao usomaji waendelea.

MGAWO NA. 3: Dakika 5. Dada atagawiwa mgawo huu. Habari za utoaji huu zitategemea “Vichwa vya Biblia vya Mazungumzo” kama vipatikanavyo katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Kikao chaweza kuwa utoaji wa ushahidi wa vivi hivi, ziara ya kurudia, funzo la Biblia nyumbani, na wenye kushiriki wanaweza wakawa ama wameketi ama wamesimama. Mwangalizi wa shule atapendezwa hasa na vile mwanafunzi anavyositawisha kichwa alichopewa na kumsaidia mwenye nyumba asababu kuhusu maandiko. Mwanafunzi mwenye kugawiwa sehemu hii apaswa awe anajua kusoma. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini msaidizi wa ziada aweza kutumiwa. Si kikao kinachopasa kupewa uangalifu mkuu, bali ni matumizi ya Biblia yenye matokeo.

MGAWO NA. 4: Dakika 5. Habari ya mgawo huu itategemea “Vichwa vya Biblia vya Mazungumzo” kama vipatikanavyo katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya, utagawiwa ndugu au dada. Unapogawiwa ndugu, huu wapaswa uwe hotuba. Kwa kawaida itafaa zaidi kwa huyo ndugu kutayarisha hotuba yake akifikiria wasikilizaji kwenye Jumba la Ufalme ili iwe yenye kuarifu na kunufaisha kikweli wale wanaoisikia hasa. Dada anapopewa sehemu hii, yapasa itolewe kama vile ilivyoonyeshwa kwa Mgawo Na. 3. Kwa kuongezea, wakati wowote kichwa cha Mgawo Na. 4 kifuatwapo na alama #, chapaswa kugawiwa ndugu.

*RATIBA YA KUONGEZEA YA USOMAJI WA BIBLIA: Hii imeongezwa katika mabano baada ya namba ya wimbo ya kila juma. Kwa kufuata ratiba hii, kusoma karibu kurasa kumi kila juma, Biblia yote nzima yaweza kusomwa kwa miaka mitatu. Sehemu katika programu ya shule au pitio la kuandika hazitegemei ratiba ya kuongezea ya usomaji.

TAARIFA: Kwa habari ya kuongezea na maagizo kuhusu shauri, wakati, mapitio ya kuandika, na utayarishaji wa migawo, tafadhali ona ukurasa wa 3 wa Huduma ya Ufalme Yetu ya Oktoba 1996.

RATIBA

Jan. 3 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 4-6

Wimbo Na. 9 [*Yeremia 49-52]

Na. 1: Thamini Baraka za Yehova (w98-SW 1/1 uku. 22-24)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 6:4-19

Na. 3: td-SW 14A Kwa Nini Mungu Hakubali Kuabudu Wazazi wa Kale?

Na. 4: td-SW 26D #Wakristo Wapaswa Kufunga Ndoa na Wakristo Tu

Jan. 10 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 7-10

Wimbo Na. 49 [*Maombolezo 1-5]

Na. 1: Mkweze Mungu wa Kweli (w98-SW 1/1 uku. 30-31)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 8:1-18

Na. 3: td-SW 14B Wanadamu Waweza Kuheshimiwa, Lakini ni Mungu Pekee wa Kuabudiwa

Na. 4: td-SW 26 E Wakristo wa Kweli Hawaoi Wake Wengi

Jan. 17 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 11-14

Wimbo Na. 132 [*Ezekieli 1-9]

Na. 1: Kwa Nini Kupanga Kimbele kwa Ajili ya Wapendwa Wetu? (w98-SW 1/15 uku. 19-22)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 11:1-12

Na. 3: td-SW 7A Har–Magedoni—Vita ya Kukomesha Uovu

Na. 4: td-SW 9A Maria Alikuwa Mama ya Yesu, Si “Mama ya Mungu”

Jan. 24 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 15-19

Wimbo Na. 162 [*Ezekieli 10-16]

Na. 1: Nguvu Yenye Kugeuza na Yenye Kuunganisha ya ile Kweli (w98-SW 1/15 uku. 29-31)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 19:11-21

Na. 3: td-SW 7B Sababu Inayofanya Har–Magedoni Iwe Tendo la Mungu la Upendo

Na. 4: td-SW 9B Biblia Huonyesha Kwamba Maria Hakuwa “Bikira Daima”

Jan. 31 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 20-23

Wimbo Na. 13 [*Ezekieli 17-21]

Na. 1: Maoni ya Kimaandiko juu ya Kusifu na Kurai (w98-SW 2/1 uku. 29-31)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 20:10-20

Na. 3: td-SW 33A Ubatizo—Takwa la Kikristo

Na. 4: td-SW 37A #Kile Ambacho Maandiko Husema juu ya Ukumbusho

Feb. 7 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 24-27

Wimbo Na. 222 [*Ezekieli 22-27]

Na. 1: Msingi wa Kutazamia Mema (w98-SW 2/1 uku. 4-6)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 25:5-16

Na. 3: td-SW 33B Ubatizo Hauoshei Mbali Dhambi

Na. 4: td-SW 37B Msherehekeo wa Misa Si wa Kimaandiko

Feb. 14 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 28-30

Wimbo Na. 180 [*Ezekieli 28-33]

Na. 1: Sitawisha Roho ya Shukrani (w98-SW 2/15 uku. 4-7)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 28:1-14

Na. 3: td-SW 1A Biblia Ni Neno la Mungu Lililopuliziwa

Na. 4: td-SW 22A #Lazima Wakristo Wote Wawe Wahudumu

Feb. 21 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu la Torati 31-34

Wimbo Na. 46 [*Ezekieli 34-39]

Na. 1: Kumbukumbu la Torati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 40-41 fu. 30-34)

Na. 2: Kumbukumbu la Torati 32:35-43

Na. 3: td-SW 1B Biblia—Mwongozo Wenye Kutumika kwa Siku Yetu

Na. 4: td-SW 22B #Sifa za Ustahili kwa Ajili ya Huduma

Feb. 28 Usomaji wa Biblia: Yoshua 1-5

Wimbo Na. 40 [*Ezekieli 40-45]

Na. 1: Utangulizi kwa Yoshua (si-SW uku. 42 fu. 1-5)

Na. 2: Yoshua 2:8-16

Na. 3: td-SW 1C Biblia—Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote

Na. 4: td-SW 39A Sababu ya Wakristo wa Kweli Kuchukiwa

Mac. 6 Usomaji wa Biblia: Yoshua 6-9

Wimbo Na. 164 [*Ezekieli 46–Danieli 2]

Na. 1: Wazazi—Walindeni Salama Watoto Wenu! (w98-SW 2/15 uku. 8-11)

Na. 2: Yoshua 7:1, 10-19

Na. 3: td-SW 2A Mitio ya Damu Mishipani Huvunja Utakatifu wa Damu

Na. 4: td-SW 39B Mke Hapaswi Kuruhusu Mume Amtenge na Mungu

Mac. 13 Usomaji wa Biblia: Yoshua 10-13

Wimbo Na. 138 [*Danieli 3-7]

Na. 1: Biblia Husema Nini Kuhusu Kipawa (w98-SW 2/15 uku. 23-27)

Na. 2: Yoshua 11:6-15

Na. 3: td-SW 2B Je, Uhai wa Mtu Uokolewe Hata Iweje?

Na. 4: td-SW 39C #Mume Hapaswi Kuruhusu Mke Amzuie Asitumikie Mungu

Mac. 20 Usomaji wa Biblia: Yoshua 14-17

Wimbo Na. 10 [*Danieli 8–Hosea 2]

Na. 1: Wanaume Waaminifu ‘Wenye Hisia Kama Zetu’ (w98-SW 3/1 uku. 26-29)

Na. 2: Yoshua 15:1-12

Na. 3: td-SW 32A Nyakati za Wasio Wayahudi Zilikoma Lini?

Na. 4: td-SW 29A Sala Ambazo Mungu Husikia

Mac. 27 Usomaji wa Biblia: Yoshua 18-20

Wimbo Na. 105 [*Hosea 3-14]

Na. 1: Kuzikumbuka Siku za Mwisho za Yesu Duniani (w98-SW 3/15 uku. 3-9)

Na. 2: Yoshua 18:1-10

Na. 3: td-SW 12A Kanisa la Kikristo ni Gani?

Na. 4: td-SW 29B Sababu Inayofanya Sala Fulani Zisifae

Apr. 3 Usomaji wa Biblia: Yoshua 21-24

Wimbo Na. 144 [*Yoeli 1–Amosi 7]

Na. 1: Yoshua—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 45-46 fu. 21-24)

Na. 2: Yoshua 21:43–22:8

Na. 3: td-SW 12B Je, Petro Ndiye “Tungamo-Mwamba”?

Na. 4: td-SW 11A #Binadamu Hakuamuliwa Kimbele Yatakayompata

Apr. 10 Usomaji wa Biblia: Waamuzi 1-4

Wimbo Na. 43 [*Amosi 8–Mika 5]

Na. 1: Utangulizi kwa Waamuzi (si-SW uku. 46-47 fu. 1-7)

Na. 2: Waamuzi 3:1-11

Na. 3: td-SW 41A Sayansi Iliyothibitishwa Hukubaliana na Simulizi la Uumbaji

Na. 4: td-SW 6A #Uhai wa Kibinadamu wa Yesu Ulikuwa “Fidia kwa Wote”

Apr. 17 Usomaji wa Biblia: Waamuzi 5-7

Wimbo Na. 193 [*Mika 6–Sefania 1]

Na. 1: Jifunze Kutokana na Maagizo ya Yesu kwa Wale 70 (w98-SW 3/1 uku. 30-31)

Na. 2: Waamuzi 5:24-31

Na. 3: td-SW 41B Je, Siku za Uumbaji Zilikuwa Kipindi cha Saa 24?

Na. 4: td-SW 6B #Sababu Kwa Nini Yesu Angeweza Kulipia Fidia

Apr. 24 Pitio la Kuandika. Kamilisha Kumbukumbu la Torati 4–Waamuzi 7

Wimbo Na. 91 [*Sefania 2–Zekaria 7]

Mei 1 Usomaji wa Biblia: Waamuzi 8-10

Wimbo Na. 38 [*Zekaria 8–Malaki 4]

Na. 1: Stahi Adhama ya Kibinafsi ya Wengine (w98-SW 4/1 uku. 28-31)

Na. 2: Waamuzi 9:7-21

Na. 3: td-SW 24A Je, Yesu Alikufa Msalabani?

Na. 4: td-SW 4A Jinsi ya Kuitambua Dini Moja ya Kweli

Mei 8 Usomaji wa Biblia: Waamuzi 11-14

Wimbo Na. 82 [*Mathayo 1-8]

Na. 1: Barnaba, Yule “Mwana wa Faraja” (w98-SW 4/15 uku. 20-23)

Na. 2: Waamuzi 13:2-10, 24

Na. 3: td-SW 24B Je, Wakristo Waabudu Msalaba?

Na. 4: td-SW 4B Je, Inafaa Kushutumu Mafundisho Yasiyo ya Kweli?

Mei 15 Usomaji wa Biblia: Waamuzi 15-18

Wimbo Na. 26 [*Mathayo 9-14]

Na. 1: Usalama Ulimwenguni Bila Majeshi (w98-SW 4/15 uku. 28-30)

Na. 2: Waamuzi 17:1-13

Na. 3: td-SW 13A Kifo Husababishwa na Nini?

Na. 4: td-SW 4C Wakati Ambapo Mungu Huruhusu Mtu Kubadili Dini

Mei 22 Usomaji wa Biblia: Waamuzi 19-21

Wimbo Na. 42 [*Mathayo 15-21]

Na. 1: Waamuzi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 50 fu. 26-28)

Na. 2: Waamuzi 19:11-21

Na. 3: td-SW 13B Je, Wafu Wanaweza Kukudhuru?

Na. 4: td-SW 4D Je, Mungu Huona “Wema Katika Dini Zote?”

Mei 29 Usomaji wa Biblia: Ruthu 1-4

Wimbo Na. 120 [*Mathayo 22-26]

Na. 1: Utangulizi kwa Ruthu na Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 51-53 fu. 1-3, 9-10)

Na. 2: Ruthu 3:1-13

Na. 3: td-SW 13C Je, Wanadamu Wanaweza Kuongea na Watu Wao wa Jamaa Waliokufa?

Na. 4: td-SW 35A Ni Nani Watakaofufuliwa Kutoka kwa Wafu?

Juni 5 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 1-3

Wimbo Na. 191 [*Mathayo 27–Marko 4]

Na. 1: Utangulizi kwa 1 Samweli (si-SW uku. 53-54 fu. 1-6)

Na. 2: 1 Samweli 1:9-20

Na. 3: td-SW 10A Je, Ibilisi ni Mtu Halisi?

Na. 4: td-SW35B Wafu Watafufuliwa Wapi?

Juni 12 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 4-7

Wimbo Na. 85 [*Marko 5-9]

Na. 1: Yehova Ni Nani? (w98-SW 5/1 uku. 5-7)

Na. 2: 1 Samweli 4:9-18

Na. 3: td-SW 10B Ibilisi—Mtawala Asiyeonekana wa Ulimwengu

Na. 4: td-SW 16A #Kurudi kwa Kristo Hakuonekani

Juni 19 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 8-11

Wimbo Na. 160 [*Marko 10-14]

Na. 1: Uaminifu-Maadili Wathawabishwa (w98-SW 5/1 uku. 30-31)

Na. 2: 1 Samweli 8:4-20

Na. 3: td-SW 10C Kile Ambacho Biblia Husema juu ya Malaika Walioasi

Na. 4: td-SW 16B #Kurudi kwa Kristo Hutambuliwa kwa Mambo ya Hakika Yenye Kuonekana

Juni 26 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 12-14

Wimbo Na. 172 [*Marko 15–Luka 3]

Na. 1: Je, Mali Zaweza Kukufanya Uwe Mwenye Furaha? (w98-SW 5/15 uku. 4-6)

Na. 2: 1 Samweli 14:1-14

Na. 3: td-SW 5A Dunia—Iliumbwa Iwe Paradiso

Na. 4: td-SW 28A Kushika Sabato Si Takwa kwa Wakristo

Jul. 3 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 15-17

Wimbo Na. 8 [*Luka 4-8]

Na. 1: Eunike na Loisi—Waelimishaji Walio Vielelezo Bora (w98-SW 5/15 uku. 7-9)

Na. 2: 1 Samweli 16:4-13

Na. 3: td-SW 5B Uhai Hautakoma Kamwe Duniani

Na. 4: td-SW28B #Wakristo Hawakupewa Sheria ya Sabato

Jul. 10 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 18-20

Wimbo Na. 156 [*Luka 9-12]

Na. 1: Fikia Moyo kwa Ufundi wa Ushawishi (w98-SW 5/15 uku. 21-23)

Na. 2: 1 Samweli 19:1-13

Na. 3: td-SW 18A Je, Unaweza Kuwatambua Manabii Wasio wa Kweli?

Na. 4: td-SW 28C #Wakati Ambapo Pumziko la Mungu la Sabato Linaanza na Kwisha

Jul. 17 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 21-24

Wimbo Na. 33 [*Luka 13-19]

Na. 1: Kuchukua Daraka Lako la Utunzaji wa Familia (w98-SW 6/1 uku. 20-23)

Na. 2: 1 Samweli 24:2-15

Na. 3: td-SW 15A Maponyo ya Kiroho Ni Muhimu Kadiri Gani?

Na. 4: td-SW 42A Wokovu ni Kutoka kwa Mungu Kupitia Kristo Pekee

Jul. 24 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 25-27

Wimbo Na. 60 [*Luka 20-24]

Na. 1: Haki ya Kweli—Lini na Jinsi Gani? (w98-SW 6/15 uku. 26-29)

Na. 2: 1 Samweli 25:23-33

Na. 3: td-SW 15B Ufalme wa Mungu—Njia ya Kuleta Maponyo ya Kimwili Yenye Kudumu

Na. 4: td-SW 42B “Ukiisha Okolewa, Umeokolewa Sikuzote” Si Wazo la Kimaandiko

Jul. 31 Usomaji wa Biblia: 1 Samweli 28-31

Wimbo Na. 170 [*Yohana 1-6]

Na. 1: 1 Samweli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 57-58 fu. 27-35)

Na. 2: 1 Samweli 31:1-13

Na. 3: td-SW 15C Imani ya Kuponya ya Kisasa Haitoki kwa Mungu

Na. 4: td-SW 42C “Wokovu wa Ulimwengu Wote Mzima” Si Wazo la Kimaandiko

Ago. 7 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 1-4

Wimbo Na. 22 [*Yohana 7-11]

Na. 1: Utangulizi kwa 2 Samweli (si-SW uku. 59 fu. 1-5)

Na. 2: 2 Samweli 2:1-11

Na. 3: td-SW 15D Je, Kusema kwa Lugha Ni Uthibitisho Hakika wa Kibali cha Mungu?

Na. 4: td-SW 3A Kinachomaanishwa na Dhambi

Ago. 14 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 5-8

Wimbo Na. 174 [*Yohana 12-18]

Na. 1: “Jikakamueni Wenyewe Kisulubu” (w98-SW 6/15 uku. 30-31)

Na. 2: 2 Samweli 7:4-16

Na. 3: td-SW 20A Ni Nani Waendao Mbinguni?

Na. 4: td-SW 3B Sababu ya Wanadamu Wote Kuteseka Kutokana na Dhambi ya Adamu

Ago. 21 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 9-12

Wimbo Na. 107 [*Yohana 19–Matendo 4]

Na. 1: Uwe Jirani Mwema (w98-SW 7/1 uku. 30-31)

Na. 2: 2 Samweli 11:2-15

Na. 3: td-SW 8A Helo Si Mahali pa Mateso ya Moto

Na. 4: td-SW 3C #Tunda Lililokatazwa Lilikuwa Nini?

Ago. 28 Pitio la Kuandika. Kamilisha Waamuzi 8–2 Samweli 12

Wimbo Na. 177 [*Matendo 5-10]

Sept. 4 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 13-15

Wimbo Na. 183 [*Matendo 11-16]

Na. 1: Waanzishie Watoto Wako Maisha Mazuri (w98-SW 7/15 uku. 4-6)

Na. 2: 2 Samweli 13:20-33

Na. 3: td-SW 8B Moto ni Mfano wa Angamizo

Na. 4: td-SW 3D #Dhambi Dhidi ya Roho Takatifu Ni Nini?

Sept. 11 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 16-18

Wimbo Na. 129 [*Matendo 17-22]

Na. 1: Maoni ya Mkristo Kuhusu Desturi za Mazishi (w98-SW 7/15 uku. 20-24)

Na. 2: 2 Samweli 16:5-14

Na. 3: td-SW 8C Simulizi la Tajiri na Lazaro Si Ithibati ya Mateso ya Milele

Na. 4: td-SW 25A #Nafsi ni Nini?

Sept. 18 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 19-21

Wimbo Na. 19 [*Matendo 23–Waroma 1]

Na. 1: Je, Waweza Kuamini Dhamiri Yako? (w98-SW 9/1 uku. 4-7)

Na. 2: 2 Samweli 20:1, 2, 14-22

Na. 3: td-SW 31A Maoni ya Mkristo Kuhusu Sikukuu

Na. 4: td-SW25B #Tofauti Kati ya Nafsi na Roho Ni Nini?

Sept. 25 Usomaji wa Biblia: 2 Samweli 22-24

Wimbo Na. 98 [*Waroma 2-9]

Na. 1: 2 Samweli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 63 fu. 28-31)

Na. 2: 2 Samweli 23:8-17

Na. 3: td-SW 23A Utumizi wa Mifano ni Suto kwa Mungu

Na. 4: td-SW 27A #Kinachomaanishwa na Roho Takatifu

Okt. 2 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 1-2

Wimbo Na. 36 [*Waroma 10–1 Wakorintho 3]

Na. 1: Utangulilizi kwa 1 Wafalme (si-SW uku. 64-65 fu. 1-5)

Na. 2: 1 Wafalme 2:1-11

Na. 3: td-SW 23B Matokeo ya Ibada ya Mifano

Na. 4: td-SW 27B #Kani ya Uhai ya Mwanadamu na Mnyama Huitwa Roho

Okt. 9 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 3-6

Wimbo Na. 106 [*1 Wakorintho 4-13]

Na. 1: Tanguliza Mambo Yanayopasa Kutangulizwa (w98-SW 9/1 uku. 19-21)

Na. 2: 1 Wafalme 4:21-34

Na. 3: td-SW 23C Yehova Pekee Ndiye Anayepasa Kuabudiwa

Na. 4: td-SW 21A #Mchanganyiko wa Imani Mbalimbali Si Njia ya Mungu

Okt. 16 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 7-8

Wimbo Na. 76 [*1 Wakorintho 14–2 Wakorintho 7]

Na. 1: Kutoa Ushahidi Mbele ya Waheshimiwa (w98-SW 9/1 uku. 30-31)

Na. 2: 1 Wafalme 7:1-14

Na. 3: td-SW 21B Je, Dini Zote ni Njema?

Na. 4: td-SW 43A Wakristo Wapaswa Kutumia Jina la Mungu la Kibinafsi

Okt. 23 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 9-11

Wimbo Na. 97 [*2 Wakorintho 8–Wagalatia 4]

Na. 1: Maoni ya Kikristo juu ya Mahari (w98-SW 9/15 uku. 24-27)

Na. 2: 1 Wafalme 11:1-13

Na. 3: td-SW 43B Kweli Kuhusu Kuwapo kwa Mungu

Na. 4: td-SW 43C #Kutambua Sifa za Mungu

Okt. 30 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 12-14

Wimbo Na. 113 [*Wagalatia 5–Wafilipi 2]

Na. 1: Je, Mungu Ni Halisi Kwako? (w98-SW 9/15 uku. 21-23)

Na. 2: 1 Wafalme 13:1-10

Na. 3: td-SW 43D Si Watu Wote Wanaomtumikia Mungu Yuleyule

Na. 4: td-SW 19A Je, Mashahidi wa Yehova ni Dini Mpya?

Nov. 6 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 15-17

Wimbo Na. 123 [*Wafilipi 3–1 Wathesalonike 5]

Na. 1: Zidi Kufanya Maendeleo ya Kiroho! (w98-SW 10/1 uku. 28-31)

Na. 2: 1 Wafalme 15:9-24

Na. 3: td-SW 44A Yesu Kristo—Mwana wa Mungu na Mfalme Aliyewekwa Rasmi

Na. 4: td-SW 44B Sababu Imani Katika Yesu ni ya Maana kwa Wokovu

Nov. 13 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 18-20

Wimbo Na. 159 [*2 Wathesalonike 1–2 Timotheo 3]

Na. 1: Tatua Matatizo kwa Amani (w98-SW 11/1 uku. 4-7)

Na. 2: 1 Wafalme 20:1, 13-22

Na. 3: td-SW 44C Je, Kuamini Yesu Tu Kwatosha Ili Kuokolewa?

Na. 4: td-SW 34A #Baraka Ambazo Ufalme wa Mungu Utaleta

Nov. 20 Usomaji wa Biblia: 1 Wafalme 21-22

Wimbo Na. 179 [*2 Timotheo 4–Waebrania 7]

Na. 1: 1 Wafalme—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 68-69 fu. 23-26)

Na. 2: 1 Wafalme 22:29-40

Na. 3: td-SW 34B Utawala wa Ufalme Waanza Wakati Ambapo Maadui wa Kristo Wangali Wanatenda

Na. 4: td-SW 34C Ufalme wa Mungu Hauji kwa Jitihada za Wanadamu

Nov. 27 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 1-3

Wimbo Na. 148 [*Waebrania 8–Yakobo 2]

Na. 1: Utangulizi kwa 2 Wafalme (si-SW uku. 69-70 fu. 1-4)

Na. 2: 2 Wafalme 2:15-25

Na. 3: td-SW 30A Kinachomaanishwa na “Mwisho wa Ulimwengu”

Na. 4: td-SW 30B #Uwe Macho Kiroho Kuelekea Ishara za Siku za Mwisho

Des. 4 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 4-6

Wimbo Na. 109 [*Yakobo 3–2 Petro 3]

Na. 1: Jihadhari na Usimoni (w98-SW 11/15 uku. 28)

Na. 2: 2 Wafalme 5:20-27

Na. 3: td-SW 36A Uhai Udumuo Milele Si Ndoto Tu

Na. 4: td-SW 36B Ni Nani Wanaoenda Mbinguni?

Des. 11 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 7-9

Wimbo Na. 117 [*1 Yohana 1–Ufunuo 1]

Na. 1: Kanuni za Biblia za Kufuata Unapokopesha au Kukopa (w98-SW 11/15 uku. 24-27)

Na. 2: 2 Wafalme 7:1, 2, 6, 7, 16-20

Na. 3: td-SW 36C Hakuna Mpaka kwa Idadi ya Wale Watakaopokea Uhai Udumuo Milele Duniani

Na. 4: td-SW 26A #Lazima Muungano wa Ndoa Uheshimike

Des. 18 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 10-12

Wimbo Na. 181 [*Ufunuo 2-12]

Na. 1: Masimulizi Halisi Kuhusu Kuzaliwa kwa Yesu (w98-SW 12/15 uku. 5-9)

Na. 2: 2 Wafalme 11:1-3, 9-16

Na. 3: td-SW 26B Lazima Wakristo Wastahi Kanuni ya Ukichwa

Na. 4: td-SW 26C Daraka la Wazazi kwa Watoto

Des. 25 Pitio la Kuandika. Kamilisha 2 Samweli 13–2 Wafalme 12

Wimbo Na. 217 [*Ufunuo 13-22]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki