Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 2001
Maagizo
Ifuatayo itakuwa mipango wakati wa kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi mwaka wa 2001.
VYANZO VYA HABARI: Migawo itategemea Biblia, Mnara wa Mlinzi [w-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], na Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW].
Shule yapasa kuanza KWA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno machache ya kukaribisha. Hakuna haja ya kupitia yale yaliyo katika programu. Mwangalizi wa shule anapotoa utangulizi wa kila sehemu, atataja habari itakayozungumziwa. Endeleeni kama ifuatavyo:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa utolewe na mzee au mtumishi wa huduma, nao utategemea Mnara wa Mlinzi au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Unapotegemea Mnara wa Mlinzi, mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 15 bila pitio la mdomo; unapotegemea kitabu “Kila Andiko,” wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 kukiwa na pitio la mdomo la dakika 3 hadi 5, kwa kutumia maswali yaliyochapwa katika kichapo hicho. Lengo halipasi kuwa kuzungumza juu ya habari hiyo tu bali pia kuvuta fikira kwenye thamani inayotumika ya habari inayozungumziwa, ukikazia yale yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa chapasa kitumiwe.
Ndugu wanaogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa lazima au likiombwa na msemaji.
MAMBO MAKUU YA USOMAJI WA BIBLIA: Dakika 6. Mgawo huu wapasa utolewe na mzee au mtumishi wa huduma atakayeitumia habari ifae mahitaji ya kwao. Si lazima kuwe na kichwa. Huu haupasi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Pitio la ujumla la sekunde 30 hadi 60 la sura ambazo mgawo umetolewa laweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye thamani kwetu. Ndipo wanafunzi watakaporuhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
MGAWO NA. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa sehemu iliyoteuliwa utakaotolewa na ndugu, iwe mwanafunzi yuko katika shule kuu au katika shule nyingine. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha kuruhusu wanafunzi watoe habari yenye maelezo mafupi ya utangulizi na maelezo ya kumalizia. Masimulizi ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yaweza kutiwa ndani. Mistari yote ya usomaji yapasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, wakati mistari inayopasa kusomwa haifuatani mfululizo, mwanafunzi aweza kutaja mstari unaofuata katika usomaji wake.
MGAWO NA. 3: Dakika 5. Dada atagawiwa mgawo huu. Habari za utoaji huu zitategemea kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Kikao chaweza kuwa utoaji wa ushahidi wa vivi hivi, ziara ya kurudia, au funzo la Biblia nyumbani, na wenye kushiriki wanaweza wakawa ama wameketi au wamesimama. Mwangalizi wa shule atapendezwa hasa na vile mwanafunzi anavyositawisha kichwa alichopewa na kumsaidia mwenye nyumba asababu kwa kutumia maandiko. Mwanafunzi mwenye kugawiwa sehemu hii apaswa awe anajua kusoma. Msaidizi mmoja ataratibiwa na mwangalizi wa shule, lakini msaidizi wa ziada aweza kutumiwa. Si kikao kinachopasa kupewa uangalifu mkuu, bali ni matumizi ya Biblia yenye matokeo.
MGAWO NA. 4: Dakika 5. Habari ya mgawo huu itategemea kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Ndugu au dada anaweza kupewa Mgawo Na. 4. Ndugu anapopewa mgawo huo, wapasa uwe hotuba sikuzote. Dada anapopewa mgawo huo, wapasa utolewe kama vile ilivyoonyeshwa katika Mgawo Na. 3.
RATIBA YA USOMAJI WA BIBLIA: Kila mtu katika kutaniko anatiwa moyo afuate ratiba ya usomaji wa Biblia kila juma, ambao unalingana na kusoma ukurasa mmoja kwa siku.
TAARIFA: Kwa habari ya ziada na maagizo kuhusu shauri, wakati, mapitio ya kuandika, na utayarishaji wa migawo, tafadhali ona ukurasa wa 3 wa Huduma Yetu ya Ufalme ya Oktoba 1996.
RATIBA
Jan. 1 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 13-16
Na. 1: Tendo la Kusamehe Latokeza Wokovu (w99-SW 1/1 uku. 30-31)
Na. 2: 2 Wafalme 14:1-14
Na. 3: Utoaji-Mimba—Kwa Nini Unakatazwa? (rs-SW uku. 395 fu. 2-396 fu. 5)
Na. 4: Kumjibu Mtu Anayesema: ‘Nina Haki ya Kuamua Mambo Yanayohusu Mwili Wangu Mwenyewe’ (rs-SW uku. 396 fu. 6)
Jan. 8 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 17-20
Na. 1: Shauri Ambalo Ni Rahisi Kukubali (w99-SW 1/15 uku. 21-24)
Na. 2: 2 Wafalme 18:1-16
Na. 3: Adamu and Hawa—Je, Ni Watu Halisi wa Kihistoria? (rs-SW uku. 25-26 fu. 5)
Na. 4: Kumjibu Mtu Anayesema: ‘Dhambi ya Adamu Ilikuwa Mapenzi ya Mungu, Mpango wa Mungu’ (rs-SW uku. 27 fu. 1-2)
Jan. 15 Usomaji wa Biblia: 2 Wafalme 21-25
Na. 1: 2 Wafalme—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa? (si-SW uku. 74 fu. 33-36)
Na. 2: 2 Wafalme 21:1-16
Na. 3: Kwa Nini Kuabudu Wazazi wa Kale Waliokufa Ni Ubatili? (rs-SW uku. 110-111 fu. 10)
Na. 4: Kwa Nini Kuabudu Wazazi wa Kale Waliokufa Hakumpendezi Yehova Mungu? (rs-SW uku. 112 fu. 1-6)
Jan. 22 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 1-5
Na. 1: Utangulizi wa 1 Mambo ya Nyakati (si-SW uku. 75-76 fu. 1-7)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 1:1-27
Na. 3: Ni Nani Walio Wapinga-Kristo? (rs-SW uku. 212-213)
Na. 4: Kuwatambua Waasi-Imani (rs-SW uku. 317-319 fu. 4)
Jan. 29 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 6-10
Na. 1: Unyenyekevu wa Kweli Unavyoweza Kuonyeshwa (w99-SW 2/1 uku. 6-7)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 9:1-21
Na. 3: Twapaswa Kuwa na Mtazamo Gani Kuelekea Waasi-Imani? (rs-SW uku. 320 fu. 1-7)
Na. 4: Kristo Hakujenga Kanisa Juu ya Petro (rs-SW uku. 224-226 fu. 4)
Feb. 5 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 11-16
Na. 1: Uwe Chanzo cha Kitia-Moyo (w99-SW 2/15 uku. 26-29)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 11:1-19
Na. 3: Funguo Alizotumia Petro Zilikuwa Gani? (rs-SW uku. 226 fu. 5–uku. 229 fu. 3)
Na. 4: “Waandamizi wa Mitume” Si Wakristo wa Kweli (rs-SW uku. 229 fu. 4–uku. 231 fu. 7)
Feb. 12 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 17-23
Na. 1: Jifungeni Hali ya Akili ya Kujishusha Chini (w99-SW 3/1 uku. 30-31)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 18:1-17
Na. 3: Har–Magedoni Itapiganiwa Wapi? (rs-SW uku. 86-88 fu. 7)
Na. 4: Ni Nani na Ni Nini Kitakachoharibiwa Kwenye Har–Magedoni? (rs-SW uku. 88 fu. 8–uku. 89 fu. 5)
Feb. 19 Usomaji wa Biblia: 1 Mambo ya Nyakati 24-29
Na. 1: 1 Mambo ya Nyakati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa? (si-SW uku. 78-79 fu. 22-25)
Na. 2: 1 Mambo ya Nyakati 29:1-13
Na. 3: Ni Nani Atakayeokoka Har–Magedoni? (rs-SW uku. 89 fu. 6-uku. 90 fu. 3)
Na. 4: Har–Magedoni—Si Kuvunjwa kwa Upendo wa Mungu (rs-SW uku. 90 fu. 4-6)
Feb. 26 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 1-5
Na. 1: Utangulizi wa 2 Mambo ya Nyakati (si-SW uku. 79-80 fu. 1-6)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 1:1-17
Na. 3: Msimamo wa Kutokuwamo Kwenye Har–Magedoni Hauwezekani (rs-SW uku. 91 fu. 1-4)
Na. 4: Ni Nani Anayesababisha Uvutano Unaosukuma Mataifa Kwenye Hali ya Har–Magedoni? (rs-SW uku. 91 fu. 5–6)
Mac. 5 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 6-9
Na. 1: Usishindwe na Hangaiko (w99-SW 3/15 uku. 21-23)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 8:1-16
Na. 3: Kutambua Babuloni Unaotajwa Katika Ufunuo (rs-SW uku. 35 fu. 1-2)
Na. 4: Babuloni wa Kale Ulijulikana kwa Kitu Gani? (rs-SW uku. 36 fu. 1–uku. 37 fu. 5)
Mac. 12 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 10-15
Na.Wimbo Na. 59
Na. 1: Ni Nani Ambaye Huongoza Kufikiri Kwako? (w99-SW 4/1 uku. 20-22)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 10:1-16
Na. 3: Kwa Nini Dini Zinazodai Kuwa za Kikristo Ni Sehemu ya Babuloni Mkuu? (rs-SW uku. 38 fu. 1–uku. 39 fu. 1)
Na. 4: Kwa Nini Kuwe na Uharaka wa Kutoka Katika Babuloni Mkuu? (rs-SW uku. 39 fu. 2-7)
Mac. 19 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 16-20
Na.Wimbo Na. 69
Na. 1: Linda Moyo Wako Dhidi ya Roho ya Ibada ya Baali (w99-SW 4/1 uku. 28-31)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 16:1-14
Na. 3: Maana ya Ubatizo Ni Nini na kwa Nini Waamini Wabatizwe? (rs-SW uku. 321 fu. 1-4)
Na. 4: Ubatizo wa Kikristo—Si Kunyunyiziwa Maji, Si wa Vitoto Vichanga (rs-SW uku. 321 fu. 5–uku. 322 fu. 5)
Mac. 26 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 21-25
Na. 1: Usikose Kuwa Mwenye Shukrani (w99-SW 4/15 uku. 15-17)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 22:1-12
Na. 3: Ubatizo wa Maji Hautoi Msamaha wa Dhambi (rs-SW uku. 322 fu. 6–uku. 323 fu. 2)
Na. 4: Ni Nani Wanaobatizwa kwa Roho Takatifu? (rs-SW uku. 323 fu. 3–uku. 324 fu. 4)
Apr. 2 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 26-29
Na.Wimbo Na. 49
Na. 1: Je, Mungu Hufanya Mambo kwa Njia ‘Zilizopotoka’?
(w99-SW 5/1 uku. 28-29)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 28:1-15
Na. 3: Ubatizo wa Moto Si Sawa na Ubatizo wa Roho Takatifu
(rs-SW uku. 324 fu. 5–uku. 325 fu. 3)
Na. 4: Sababu za Kutufanya Tuichunguze Biblia (rs-SW uku. 40-41)
Apr. 9 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 30-33
Na.Wimbo Na. 1
Na. 1: Wanadamu Wanaweza Kumhimidije Yehova?
(w99-SW 5/15 uku. 21-24)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 33:1-13
Na. 3: Uthibitisho Kutoka Isaya na Yeremia Kwamba Biblia Iliongozwa na Mungu (rs-SW uku. 42–uku. 43 fu. 1)
Na. 4: Utimizo wa Unabii Mbalimbali wa Yesu Wathibitisha Biblia Iliongozwa na Mungu (rs-SW uku. 43 fu. 2–3)
Apr. 16 Usomaji wa Biblia: 2 Mambo ya Nyakati 34-36
Na. 1: 2 Mambo ya Nyakati—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa?
(si-SW uku. 84 fu. 34-36)
Na. 2: 2 Mambo ya Nyakati 36:1-16
Na. 3: Biblia Ni Timamu Kisayansi (rs-SW uku. 44 fu. 1–uku. 46 fu. 1)
Na. 4: aKujibu Vipingamizi Kuhusu Biblia
(rs-SW uku. 46 fu. 2–uku. 49)
Apr. 23 Usomaji wa Biblia: Ezra 1-6
Na.Wimbo Na. 90
Na. 1: Utangulizi wa Ezra na kwa Nini Ni Chenye Mafaa?
(si-SW uku. 85 fu. 1-7; uku. 87 fu. 14-18)
Na. 2: Ezra 4:1-16
Na. 3: Kwa Nini Wakristo Hawasherehekei Ukumbusho wa Siku ya Kuzaliwa? (rs-SW uku. 356-358 fu. 2)
Na. 4: Kwa Nini Wakristo Huepuka Damu? (rs-SW uku. 50-52 fu. 1)
Apr. 30 Pitio la Kuandika. Usomaji wa Biblia: Ezra 7-10
Mei 7 Usomaji wa Biblia: Nehemia 1-5
Na.Wimbo Na. 56
Na. 1: Utangulizi wa Nehemia (si-SW uku. 88 fu. 1-5)
Na. 2: Nehemia 1:1-11
Na. 3: Kwa Nini Wakristo Hukataa Kutiwa Damu Mishipani?
(rs-SW uku. 52 fu. 2–uku. 53)
Na. 4: bKujibu Madai Yanayotolewa Kuhusu Kutiwa Damu Mishipani (rs-SW uku. 54 fu. 1–uku. 56 fu. 1)
Mei 14 Usomaji wa Biblia: Nehemia 6-9
Na. 1: Kutaniko la Kikristo Ni Chanzo cha Msaada Wenye Kutia Nguvu (w99-SW 5/15 uku. 25-28)
Na. 2: Nehemia 9:1-15
Na. 3: Ni Nini Maana ya Kuzaliwa Mara ya Pili?
(rs-SW uku. 150-151 fu. 6)
Na. 4: Wokovu Hautegemei ‘Kuzaliwa Mara ya Pili’
(rs-SW uku. 151 fu. 7–uku. 153 fu. 1)
Mei 21 Usomaji wa Biblia: Nehemia 10-13
Na.Wimbo Na. 46
Na. 1: Nehemia—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa?
(si-SW uku. 90-91 fu. 16-19)
Na. 2: Nehemia 12:27-43
Na. 3: cKujibu Maoni ya Watu Kuhusu Kuzaliwa Mara ya Pili
(rs-SW uku. 153 fu. 3–uku. 154 fu. 1)
Na. 4: Kuungama Mbele ya Makasisi—Kwa Nini Hakupatani na Maandiko? (rs-SW uku. 365-366 fu. 3)
Mei 28 Usomaji wa Biblia: Esta 1-4
Na.Wimbo Na. 38
Na. 1: Utangulizi wa Esta (si-SW uku. 91-92 fu. 1-6)
Na. 2: Esta 1:1-15
Na. 3: Kuungama Dhambi Iliyofanywa Dhidi ya Mungu na Mwanadamu (rs-SW uku. 367 fu. 4-uku. 368 fu 3)
Na. 4: Kwa Nini Dhambi Nzito Zimepasa Kuungamwa kwa Wazee? (rs-SW uku. 368 fu. 4–8)
Juni 4 Usomaji wa Biblia: Esta 5-10
Na.Wimbo Na. 37
Na. 1: Esta—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa? (si-SW uku. 94 fu. 16-18)
Na. 2: Esta 5:1-14
Na. 3: Kwa Nini Ni Jambo la Akili Kuamini Uumbaji?
(rs-SW uku. 397-399 fu. 1)
Na. 4: Kuelewa Masimulizi ya Biblia Juu ya Uumbaji
(rs-SW uku. 399 fu. 2–uku. 401 fu. 2)
Juni 11 Usomaji wa Biblia: Ayubu 1-7
Na.Wimbo Na. 84
Na. 1: Utangulizi wa Ayubu (si-SW uku. 95-96 fu. 1-6)
Na. 2: Ayubu 1:6-22
Na. 3: Kwa Nini Kuheshimu Msalaba Hakupatani na Maandiko?
(rs-SW uku. 217 fu. 1–7)
Na. 4: Kwa Nini Wanadamu Hufa? (rs-SW uku. 100-101 fu. 5)
Juni 18 Usomaji wa Biblia: Ayubu 8-14
Na. 1: Sauli—Chombo-Kichaguliwa kwa Bwana
(w99-SW 5/15 uku. 29-31)
Na. 2: Ayubu 8:1-22
Na. 3: Wafu Wako Wapi na Wako Katika Hali Gani?
(rs-SW uku. 101 fu. 6–uku. 103 fu. 3)
Na. 4: Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Hawashiriki Desturi za Kimapokeo za Maombolezo?
(rs-SW uku. 104 fu. 1–uku. 105 fu. 1)
Juni 25 Usomaji wa Biblia: Ayubu 15-21
Na.Wimbo Na. 81
Na. 1: Mungu Si wa Polepole kwa Habari ya Ahadi Yake
(w99-SW 6/1 uku. 4-7)
Na. 2: Ayubu 17:1-16
Na. 3: dKujibu Watu Wenye Maoni Yasiyofaa Kuhusu Kifo
(rs-SW uku. 105 fu. 2–4)
Na. 4: Ndoto: Zilizoongozwa na Zisizoongozwa na Mungu
(rs-SW uku. 247-248 fu. 5)
Jul. 2 Usomaji wa Biblia: Ayubu 22-29
Na. 1: Je, Yakupasa Kupanua Maoni Yako? (w99-SW 6/15 uku. 10-13)
Na. 2: Ayubu 27:1-23
Na. 3: Dawa za Kulevya—Zinapokatazwa kwa Wakristo
(rs-SW uku. 56-58 fu. 2)
Na. 4: Kwa Nini Wakristo Huepuka Marijuana au Bangi?
(rs-SW uku. 58 fu. 3–uku. 59 fu. 2)
Jul. 9 Usomaji wa Biblia: Ayubu 30-35
Na. 1: Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia
(w99-SW 7/15 uku. 4-8)
Na. 2: Ayubu 31:1-22
Na. 3: Kwa Nini Wakristo Huepuka Tumbaku?
(rs-SW uku. 60 fu. 1–uku. 61 fu. 4)
Na. 4: Twaweza Kushindaje Mazoea Mabaya? (rs-SW uku. 62 fu. 1–4)
Jul. 16 Usomaji wa Biblia: Ayubu 36-42
Na. 1: Ayubu—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa? (si-SW uku. 100 fu. 39-43)
Na. 2: Ayubu 36:1-22
Na. 3: Mataifa Hayatazuia Kusudi la Mungu Kuhusu Dunia
(rs-SW uku. 78-79 fu. 3)
Na. 4: Je, Yehova Ataiharibu Dunia kwa Moto?
(rs-SW uku. 79 fu. 4–uku. 80 fu. 1)
Jul. 23 Usomaji wa Biblia: Zaburi 1-10
Na.Wimbo Na. 5
Na. 1: Utangulizi wa Zaburi—Sehemu ya 1 (si-SW uku. 101 fu. 1-5)
Na. 2: Zaburi 3:1–4:8
Na. 3: Washiriki wa Yerusalemu Mpya Hawatarudi Duniani Baada ya Waovu Kuharibiwa (rs-SW uku. 81 fu. 2–3)
Na. 4: Je, Kusudi la Mungu la Awali kwa Dunia Limebadilika? (rs-SW uku. 82 fu. 1–uku. 83 fu. 1)
Jul. 30 Usomaji wa Biblia: Zaburi 11-18
Na.Wimbo Na. 48
Na. 1: Utangulizi wa Zaburi—Sehemu ya 2 (si-SW uku. 102 fu. 6-11)
Na. 2: Zaburi 11:1–13:6
Na. 3: Twaweza Kuwatiaje Moyo Walio Wagonjwa?
(rs-SW uku. 106-107 fu. 2)
Na. 4: Jinsi Tunavyoweza Kuwatia Moyo Waliofiwa
(rs-SW uku. 107 fu. 3-7)
Ago. 6 Usomaji wa Biblia: Zaburi 19-26
Na. 1: Mawasiliano Yenye Kujenga—Ufunguo wa Kuwa na Ndoa Nzuri (w99-SW 7/15 uku. 21-23)
Na. 2: Zaburi 20:1–21:13
Na. 3: Kitia-Moyo kwa Wale Wanaonyanyaswa kwa Ajili ya Kufanya Mapenzi ya Mungu (rs-SW uku. 107 fu. 8–uku. 108 fu. 5)
Na. 4: Unaweza Kutiaje Moyo Wale Waliovunjika Moyo kwa Sababu ya Ukosefu wa Haki? (rs-SW uku. 108 fu. 6–uku. 109 fu. 2)
Ago. 13 Usomaji wa Biblia: Zaburi 27-34
Na. 1: Filipo—Mweneza-Evanjeli Mwenye Bidii
(w99-SW 7/15 uku. 24-25)
Na. 2: Zaburi 28:1–29:11
Na. 3: Kuna Kitia-Moyo Gani kwa Ajili ya Wale Wanaokazwa na Matatizo ya Kiuchumi? (rs-SW uku. 109 fu. 3-7)
Na. 4: Kitia-Moyo kwa Wale Waliovunjika Moyo kwa Sababu ya Kufanya Makosa (rs-SW uku. 109 fu. 8–uku. 110 fu. 3)
Ago. 20 Usomaji wa Biblia: Zaburi 35-39
Na.Wimbo Na. 18
Na. 1: Msongo wa Marika—Je, Waweza Kutumiwa kwa Manufaa Yako? (w99-SW 8/1 uku. 22-25)
Na. 2: Zaburi 38:1-22
Na. 3: Mageuzi—Tatizo la Kisayansi (rs-SW uku. 159-161 fu. 1)
Na. 4: Mageuzi, Rekodi ya Visukuku, na Kusababu
(rs-SW uku. 161 fu. 2–uku. 163 fu. 6)
Ago. 27 Pitio la Kuandika. Usomaji wa Biblia: Zaburi 40-47
Sept. 3 Usomaji wa Biblia: Zaburi 48-55
Na. 1: Zuia Hasira Isikukwaze (w99-SW 8/15 uku. 8-9)
Na. 2: Zaburi 49:1-20
Na. 3: eKujibu Madai Yanayotolewa na Wanamageuzi (rs-SW uku. 164–uku. 166 fu. 2)
Na. 4: Kwa Nini Watu Wengi Wanakosa Imani? (rs-SW uku. 91-92 fu. 5)
Sept. 10 Usomaji wa Biblia: Zaburi 56-65
Na. 1: Je, Ibilisi Hutufanya Tuwe Wagonjwa? (w99-SW 9/1 uku. 4-7)
Na. 2: Zaburi 59:1-17
Na. 3: Mtu Aweza Kupataje Imani? (rs-SW uku. 93 fu. 1–4)
Na. 4: Imani Katika Taraja la Mfumo Mpya Wenye Uadilifu Yathibitishwa kwa Matendo
(rs-SW uku. 93 fu. 6–uku. 94 fu. 4)
Sept. 17 Usomaji wa Biblia: Zaburi 66-71
Na. 1: Chagua “Fungu Jema” (w99-SW 9/1 uku. 30-31)
Na. 2: Zaburi 69:1-19
Na. 3: Manabii Bandia Wanaweza Kutambuliwaje?
(rs-SW uku. 166-168 fu. 2)
Na. 4: Manabii wa Kweli Hawakuelewa Sikuzote Jinsi na Lini Mambo Yaliyotabiriwa Yangetukia (rs-SW uku. 168 fu. 3-8)
Sept. 24 Usomaji wa Biblia: Zaburi 72-77
Na. 1: Kwa Nini Utimize Ahadi Zako? (w99-SW 9/15 uku. 8-11)
Na. 2: Zaburi 73:1-24
Na. 3: Matamko ya Nabii wa Kweli Yanaendeleza Ibada ya Kweli
(rs-SW uku. 169 fu. 1-2)
Na. 4: Manabii wa Kweli Hutambuliwa kwa Matunda Wanayotokeza (rs-SW uku. 169 fu. 3–uku. 171 fu. 1)
Okt. 1 Usomaji wa Biblia: Zaburi 78-81
Na. 1: Pata Hekima na Ukubali Nidhamu (w99-SW 9/15 uku. 12-15)
Na. 2: Zaburi 78:1-22
Na. 3: Kujibu Wale Ambao Hutuita Manabii Bandia
(rs-SW uku. 171 fu. 2-4)
Na. 4: Mungu Haamulii Kimbele Kila Mtu Wakati wa Kufa
(rs-SW uku. 27-uku. 28 fu. 2)
Okt. 8 Usomaji wa Biblia: Zaburi 82-89
Na. 1: Timotheo—“Mtoto Halisi Katika Imani”
(w99-SW 9/15 uku. 29-31)
Na. 2: Zaburi 88:1-18
Na. 3: Si Kila Jambo Linalotukia Ni Mapenzi ya Mungu
(rs-SW uku. 28 fu. 3–uku. 29 fu. 7)
Na. 4: Mungu Hajui Kimbele na Kuweka Kimbele Kila Jambo
(rs-SW uku. 30 fu. 1-3)
Okt. 15 Usomaji wa Biblia: Zaburi 90-98
Na. 1: Tumeimarishwa Kukataa Kutenda Kosa
(w99-SW 10/1 uku. 28-31)
Na. 2: Zaburi 90:1-17
Na. 3: Uwezo wa Mungu wa Kujua na Kuweka Kimbele Matukio (rs-SW uku. 30 fu. 4-uku. 31 fu. 3)
Na. 4: Kwa Nini Mungu Hakutumia Uwezo Wake wa Kujua
Kimbele Mambo kwa Habari ya Adamu?
(rs-SW uku. 31 fu. 4-uku. 32 fu. 1)
Okt. 22 Usomaji wa Biblia: Zaburi 99-105
Na. 1: Kujifunza Njia Ipitayo Zote ya Upendo (w99-SW 10/15 uku. 8-11)
Na. 2: Zaburi 103:1-22
Na. 3: Mungu Hakuamuru Kimbele Mambo Ambayo Yangewapata Yakobo, Esau, au Yuda (rs-SW uku. 32 fu. 2–uku. 33 fu. 1)
Na. 4: Kutaniko la Kikristo Liliamuriwa Kimbele kwa Njia Gani? (rs-SW uku. 33 fu. 2–3)
Okt. 29 Usomaji wa Biblia: Zaburi 106-109
Na. 1: “Bwana Huwapa Watu Hekima” (w99-SW 11/15 uku. 24-27)
Na. 2: Zaburi 107:1-19
Na. 3: Ni Nini Maoni ya Maandiko Kuhusu Unajimu?
(rs-SW uku. 34 fu. 1–5)
Na. 4: Ni Nini Baadhi ya Sababu Timamu za Kuitikadi Kwamba Kuna Mungu? (rs-SW uku. 218-219 fu. 3)
Nov. 5 Usomaji wa Biblia: Zaburi 110-118
Na.Wimbo Na. 14
Na. 1: Apokalipsi—Je, Tuiogope au Tuitumainie?
(w99-SW 12/1 uku. 5-8)
Na. 2: Zaburi 112:1–113:9
Na. 3: Uovu na Mateso Havithibitishi Kutokuwako kwa Mungu (rs-SW uku. 219 fu. 4–6)
Na. 4: Mungu Ni Mtu Halisi Awezaye Kuwa na Hisia-Moyo
(rs-SW uku. 220 fu. 1–7)
Nov. 12 Usomaji wa Biblia: Zaburi 119
Na.Wimbo Na. 35
Na. 1: Usiache Uwezo Wako Uwe Udhaifu Wako
(w99-SW 12/1 uku. 26-29)
Na. 2: Zaburi 119:1-24
Na. 3: Mungu Hakuwa na Mwanzo (rs-SW uku. 220
fu. 8-uku. 221 fu. 3)
Na. 4: Kutumia Jina la Mungu Ni Muhimu Ili Kupata Wokovu
(rs-SW uku. 222 fu. 1-4)
Nov. 19 Usomaji wa Biblia: Zaburi 120-137
Na. 1: Zaburi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa?—Sehemu ya 1
(si-SW uku. 104-105 fu. 23-27)
Na. 2: Zaburi 120:1–122:9
Na. 3: Je, Dini Zote Ni Nzuri? (rs-SW uku. 222 fu. 5-8)
Na. 4: Yesu Ni “Mungu” wa Aina Gani? (rs-SW uku. 222 fu. 9-10)
Nov. 26 Usomaji wa Biblia: Zaburi 138-150
Na. 1: Zaburi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa?—Sehemu ya 2
(si-SW uku. 105-106 fu. 28-32)
Na. 2: Zaburi 139:1-24
Na. 3: fKujibu Vipingamizi Kuhusu Kuitikadi Mungu
(rs-SW uku. 223 fu. 1–uku. 224 fu. 2)
Na. 4: Kwa Nini Binadamu Wameshindwa Kusimamisha Serikali Yenye Haki? (rs-SW uku. 279-280 fu. 6)
Des. 3 Usomaji wa Biblia: Mithali 1-7
Na. 1: Utangulizi wa Mithali—Sehemu ya 1 (si-SW uku. 106-107 fu. 1-5)
Na. 2: Mithali 4:1-27
Na. 3: Kwa Nini Jitihada za Wanadamu za Kuleta Kitulizo Haziwezi Kufanikiwa? (rs-SW uku. 281 fu. 1–6)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Ndio Jawabu Pekee kwa Mahitaji Halisi ya Wanadamu (rs-SW uku. 282 fu. 1–5)
Des. 10 Usomaji wa Biblia: Mithali 8-13
Na. 1: Utangulizi wa Mithali—Sehemu ya 2 (si-SW uku. 107-108 fu. 6-11)
Na. 2: Mithali 13:1-25
Na. 3: Unabii wa Biblia Umethibitika Kuwa Wenye Kutegemeka Kabisa (rs-SW uku. 283 fu. 1-4)
Na. 4: Maponyo ya Kimwujiza Leo Hayafanywi na Roho ya Mungu (rs-SW uku. 122-123 fu. 3)
Des. 17 Usomaji wa Biblia: Mithali 14-19
Na. 1: Mithali—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa?—Sehemu ya 1
(si-SW uku. 109-110 fu. 19-28)
Na. 2: Mithali 16:1-25
Na. 3: Tofauti Kati ya Maponyo ya Yesu na Mitume Wake na Yale ya Leo (rs-SW uku. 123 fu. 4–uku. 124 fu. 2)
Na. 4: Jinsi Wakristo wa Kweli Wanavyotambuliwa Leo
(rs-SW uku. 124 fu. 3–uku. 125 fu. 1)
Des. 24 Usomaji wa Biblia: Mithali 20-25
Na. 1: Mithali—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa?—Sehemu ya 2
(si-SW uku. 110-111 fu. 29-38)
Na. 2: Mithali 20:1-30
Na. 3: Kwa Nini Vipawa vya Kuponya Vilipewa Wakristo wa Karne ya Kwanza? (rs-SW uku. 125 fu. 2–uku. 126 fu. 2)
Na. 4: Kuna Tumaini Gani kwa Uponyaji wa Kweli wa Wanadamu Wote? (rs-SW uku. 126 fu. 3-5)
Des. 31 Pitio la Kuandika. Usomaji wa Biblia: Mithali 26-31
[Maelezo ya Chini]
a Wakati ukiruhusu, zungumzieni majibu kwa madai, vipingamizi, na kadhalika ambavyo vitafaa kabisa eneo lenu.
b Wakati ukiruhusu, zungumzieni majibu kwa madai, vipingamizi, na kadhalika ambavyo vitafaa kabisa eneo lenu.
c Wakati ukiruhusu, zungumzieni majibu kwa madai, vipingamizi, na kadhalika ambavyo vitafaa kabisa eneo lenu.
d Wakati ukiruhusu, zungumzieni majibu kwa madai, vipingamizi, na kadhalika ambavyo vitafaa kabisa eneo lenu.
e Wakati ukiruhusu, zungumzieni majibu kwa madai, vipingamizi, na kadhalika ambavyo vitafaa kabisa eneo lenu.
f Wakati ukiruhusu, zungumzieni majibu kwa madai, vipingamizi, na kadhalika ambavyo vitafaa kabisa eneo lenu.