Ratiba Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 2002
Maagizo
Ifuatayo itakuwa mipango ya kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi mwaka wa 2002.
VYANZO VYA HABARI: Migawo itategemea Biblia, Mnara wa Mlinzi [w-SW], “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” [si-SW], na Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko [rs-SW].
Shule yapasa kuanza KWA WAKATI kwa wimbo, sala, na maneno machache ya kukaribisha. Hakuna haja ya kupitia yale yaliyo katika programu. Mwangalizi wa shule anapotoa utangulizi wa kila sehemu, atataja habari itakayozungumziwa. Endeleeni kama ifuatavyo:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa utolewe na mzee au mtumishi wa huduma, nao utategemea Mnara wa Mlinzi au “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Unapotegemea Mnara wa Mlinzi, mgawo huu wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 15 bila kuwauliza wasikilizaji maswali; unapotegemea kitabu “Kila Andiko,” wapasa kutolewa ukiwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12, ukitumia dakika 3 hadi 5 kuwauliza wasikilizaji maswali yaliyo katika kichapo hicho. Lengo halipasi kuwa kuzungumza juu ya habari hiyo tu bali pia kuonyesha jinsi habari inayozungumziwa inavyoweza kutumika, ukikazia mambo yatakayosaidia kutaniko. Kichwa kilichoonyeshwa chapasa kitumiwe.
Ndugu wanaogawiwa hotuba hii wapaswa kuwa waangalifu wasipite wakati uliowekwa. Shauri la faragha laweza kutolewa ikiwa lazima au likiombwa na msemaji.
MAMBO MAKUU YA USOMAJI WA BIBLIA: Dakika 6. Mgawo huu wapasa utolewe na mzee au mtumishi wa huduma atakayeitumia habari ifae mahitaji ya kwenu. Si lazima kuwe na kichwa. Huu haupasi kuwa muhtasari tu wa usomaji uliogawiwa. Pitio la ujumla la sekunde 30 hadi 60 la sura ambazo mgawo umetolewa laweza kutiwa ndani. Hata hivyo, lengo hasa ni kuwasaidia wasikilizaji wathamini ni kwa nini na ni jinsi gani habari hiyo ni yenye faida kwetu. Ndipo wanafunzi watakaporuhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
MGAWO NA. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia wa sehemu iliyoteuliwa utakaotolewa na ndugu, iwe mwanafunzi yuko katika shule kuu au katika shule nyingine. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha kuruhusu wanafunzi watoe utangulizi mfupi na maelezo ya kumalizia. Masimulizi ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho, na matumizi ya kanuni yaweza kutiwa ndani. Mistari yote yapasa isomwe bila kukatizwa. Wakati mistari inayopasa kusomwa haifuatani mfululizo, mwanafunzi aweza kutaja mstari unaofuata katika usomaji wake.
MGAWO NA. 3: Dakika 5. Dada atagawiwa mgawo huu. Habari za hotuba hii zitategemea kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Kikao chochote kinachofaa eneo lenu chaweza kutumiwa, na wenye kushiriki wanaweza kuketi au kusimama. Mwangalizi wa shule atapendezwa hasa na vile mwanafunzi anavyozungumzia kichwa alichopewa na kumsaidia mwenye nyumba asababu kwa kutumia maandiko. Mwanafunzi anayegawiwa sehemu hii apaswa awe anajua kusoma. Mwangalizi wa shule atapanga kuwe na msaidizi mmoja, lakini msaidizi wa ziada aweza kutumiwa. Matumizi ya Biblia yenye matokeo ndiyo yanayopasa kupewa uangalifu mkuu wala si kikao.
MGAWO NA. 4: Dakika 5. Habari ya mgawo huu itategemea kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko. Ndugu au dada anaweza kupewa Mgawo Na. 4. Ndugu anapopewa mgawo huu, wapasa uwe hotuba. Dada anapopewa mgawo huu, wapasa utolewe kama vile ilivyoonyeshwa katika Mgawo Na. 3.
RATIBA YA USOMAJI WA BIBLIA: Kila mtu katika kutaniko anatiwa moyo afuate ratiba ya usomaji wa Biblia kila juma, ambao unalingana na kusoma ukurasa mmoja kwa siku.
TAARIFA: Kwa habari ya ziada na maagizo kuhusu shauri, wakati, mapitio ya kuandika, na utayarishaji wa migawo, tafadhali ona ukurasa wa 3 wa Huduma Yetu ya Ufalme ya Oktoba 1996.
RATIBA
Jan. 7 Usomaji wa Biblia: Mhubiri 1-6
Wimbo Na. 59
Na. 1: Utangulizi wa Mhubiri (si-SW uku. 112-113 fu. 1-8)
Na. 2: Mhubiri 4:1-16
Na. 3: a‘Je, Wewe Huamini Maponyo?’ (rs-SW uku. 126 fu. 6–uku. 127 fu. 1)
Na. 4: Je, Sisi Sote Tulikuwa Katika Makao ya Kiroho Kabla ya Kuzaliwa Tukiwa Wanadamu? (rs-SW uku. 189 fu. 1–5)
Jan. 14 Usomaji wa Biblia: Mhubiri 7-12
Wimbo Na. 25
Na. 1: Mhubiri—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 114 fu. 15-19)
Na. 2: Mhubiri 8:1-17
Na. 3: Kama Adamu Hangefanya Dhambi, Je, Hatimaye Angeenda Mbinguni? (rs-SW uku. 189 fu. 6-uku. 190 fu. 1)
Na. 4: Je, Ni Lazima Mtu Aende Mbinguni Ili Awe na Wakati Ujao Wenye Furaha Kwelikweli? (rs-SW uku. 190 fu. 2-4)
Jan. 21 Usomaji wa Biblia: Wimbo Ulio Bora 1-8
Wimbo Na. 11
Na. 1: Utangulizi wa Wimbo Ulio Bora na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 115-117 fu. 1-4, 16-18)
Na. 2: Wimbo Ulio Bora 5:1-16
Na. 3: Andiko la 1 Petro 3:19, 20 Humaanisha Nini? (rs-SW uku. 190 fu. 5)
Na. 4: Andiko la 1 Petro 4:6 Humaanisha Nini? (rs-SW uku. 191 fu. 1)
Jan. 28 Usomaji wa Biblia: Isaya 1-6
Wimbo Na. 204
Na. 1: Utangulizi wa Isaya (si-SW uku. 118-119 fu. 1-8)
Na. 2: Isaya 2:1-17
Na. 3: Je, Wakristo Wote Wana Tumaini la Uhai wa Kimbingu? (rs-SW uku. 191 fu. 2-uku. 192 fu. 2)
Na. 4: “Agano Jipya” Husema Nini Kuhusu Uhai wa Milele Duniani? (rs-SW uku. 192 fu. 3–uku. 193 fu. 4)
Feb. 4 Usomaji wa Biblia: Isaya 7-11
Wimbo Na. 89
Na. 1: Twahitaji Tengenezo la Yehova (w00-SW 1/1 uku. 30-31)
Na. 2: Isaya 8:1-22
Na. 3: Biblia Inatolea Watu Wangapi Tumaini la Uhai wa Kimbingu? (rs-SW uku. 194 fu. 1-2)
Na. 4: Je, 144,000 Ni Wayahudi wa Asili Peke Yao? (rs-SW uku. 194 fu. 3–6)
Feb. 11 Usomaji wa Biblia: Isaya 12-19
Wimbo Na. 177
Na. 1: Wajionaje? (w00-SW 1/15 uku. 20-22)
Na. 2: Isaya 17:1-14
Na. 3: Maandiko Husema Nini Kuhusu Tumaini la “Umati Mkubwa”? (rs-SW uku. 195 fu. 1–3)
Na. 4: Wale Waendao Mbinguni Watafanya Nini Kule? (rs-SW uku. 195 fu. 4–uku. 196 fu. 2)
Feb. 18 Usomaji wa Biblia: Isaya 20-26
Wimbo Na. 225
Na. 1: Kuza Urafiki wa Karibu Pamoja na Yehova (w00-SW 1/15 uku. 23-26)
Na. 2: Isaya 22:1-19
Na. 3: Je, Biblia Yaonyesha Kwamba Nafsi Inaendelea Kuishi Baada ya Mwili Kufa? (rs-SW uku. 205 fu. 3–uku. 206 fu. 4)
Na. 4: Ni Watu wa Aina Gani Wanaoenda Kwenye Hell Inayosemwa na Biblia? (rs-SW uku. 206 fu. 5–uku. 207 fu. 2)
Feb. 25 Usomaji wa Biblia: Isaya 27-31
Wimbo Na. 192
Na. 1: Mnyanyasaji Aona Nuru Kubwa (w00-SW 1/15 uku. 27-29)
Na. 2: Isaya 29:1-14
Na. 3: Je, Yeyote Amewahi Kutoka Katika Hell Inayosemwa na Biblia? (rs-SW uku. 207 fu. 3-5)
Na. 4: Je, Kuna Adhabu ya Milele kwa Waovu? (rs-SW uku. 208 fu. 1-3)
Mac. 4 Usomaji wa Biblia: Isaya 32-37
Wimbo Na. 98
Na. 1: Kufanikiwa Kupitia Udumifu (w00-SW 2/1 uku. 4-6)
Na. 2: Isaya 33:1-16
Na. 3: Ni Nini Maana ya ‘Kuteswa Milele’ Kunakotajwa Katika Ufunuo? (rs-SW uku. 208 fu. 4–uku. 209 fu. 1)
Na. 4: Ni Nini ‘Gehena ya Moto’ Ambayo Yesu Alirejezea? (rs-SW uku. 209 fu. 2–uku. 210 fu. 1)
Mac. 11 Usomaji wa Biblia: Isaya 38-42
Wimbo Na. 132
Na. 1: Shauri la Mama Lenye Hekima (w00-SW 2/1 uku. 30-31)
Na. 2: Isaya 42:1-16
Na. 3: Adhabu ya Dhambi Ni Nini? (rs-SW uku. 210 fu. 2-5)
Na. 4: Je, Yesu Alifundisha Kwamba Waovu Huteswa Baada ya Kifo? (rs-SW uku. 211 fu. 1)
Mac. 18 Usomaji wa Biblia: Isaya 43-47
Wimbo Na. 160
Na. 1: Epuka Eneo la Hatari (w00-SW 2/15 uku. 4-7)
Na. 2: Isaya 44:6-20
Na. 3: Mfano wa Tajiri na Lazaro Wamaanisha Nini? (rs-SW uku. 211 fu. 2–uku. 212 fu. 1)
Na. 4: Je, Krismasi Ni Mwadhimisho Unaotegemea Biblia? (rs-SW uku. 290 fu. 1-4)
Mac. 25 Usomaji wa Biblia: Isaya 48-52
Wimbo Na. 161
Na. 1: Nguvu ya Sala (w00-SW 3/1 uku. 3-4)
Na. 2: Isaya 49:1-13
Na. 3: Wale Watu Wenye Hekima, au Mamajusi, Walioongozwa kwa Yesu na Nyota Walikuwa Akina Nani? (rs-SW uku. 291 fu. 1-3)
Na. 4: Twapaswa Kufikiria Nini Tunapochunguza Desturi za Krismasi? (rs-SW uku. 291 fu. 4–uku. 292 fu. 2)
Apr. 1 Usomaji wa Biblia: Isaya 53-59
Wimbo Na. 210
Na. 1: Kumtafuta Yehova kwa Moyo Ulio Tayari (w00-SW 3/1 uku. 29-31)
Na. 2: Isaya 54:1-17
Na. 3: Ni Kanuni Gani Zinazopasa Kutuongoza Kuhusiana na Sherehe? (rs-SW uku. 292 fu. 3–uku. 293 fu. 2)
Na. 4: Ni Mambo Gani Tunayopaswa Kujua Kuhusu Sherehe za Ista na Mwaka Mpya? (rs-SW uku. 293 fu. 3–uku. 294 fu. 3)
Apr. 8 Usomaji wa Biblia: Isaya 60-66
Wimbo Na. 111
Na. 1: Isaya—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 123 fu. 34-39)
Na. 2: Isaya 61:1-11
Na. 3: Ni Nini Iliyo Asili ya Sikukuu za Kukumbuka “Roho za Wafu”? (rs-SW uku. 294 fu. 4–uku. 295 fu. 3)
Na. 4: Twajua Nini Kuhusu Asili ya Siku ya Valentine, Siku ya Mama, na Sikukuu za Kitaifa? (rs-SW uku. 296 fu. 1-6)
Apr. 15 Usomaji wa Biblia: Yeremia 1-4
Wimbo Na. 70
Na. 1: Utangulizi wa Yeremia (si-SW uku. 124 fu. 1-5)
Na. 2: Yeremia 2:4-19
Na. 3: Biblia Husema Nini Juu ya Mifano Inayotumiwa Kuwa Vitu vya Ibada? (rs-SW uku. 196 fu. 3–uku. 197 fu. 2)
Na. 4: Je, Mifano Inaweza Kutumiwa Kuwa Misaada Tu Katika Ibada ya Mungu wa Kweli? (rs-SW uku. 197 fu. 3-7)
Apr. 22 Usomaji wa Biblia: Yeremia 5-8
Wimbo Na. 205
Na. 1: Sababu Inayofanya Wanadamu Wahitaji Msaidiaji (w00-SW 3/15 uku. 3-4)
Na. 2: Yeremia 7:1-20
Na. 3: Je, Tuheshimu “Watakatifu” Kama Waombezi Wetu kwa Mungu? (rs-SW uku. 197 fu. 8–uku. 198 fu. 5)
Na. 4: Mungu Anaonaje Mifano Ambayo Ni Vitu vya Ibada? (rs-SW uku. 198 fu. 6–uku. 199 fu. 3)
Apr. 29 Pitio la Kuandika. Usomaji wa Biblia: Yeremia 9-13
Wimbo Na. 46
Mei 6 Usomaji wa Biblia: Yeremia 14-18
Wimbo Na. 224
Na. 1: Jinsi Yesu Kristo Awezavyo Kutusaidia (w00-SW 3/15 uku. 5-9)
Na. 2: Yeremia 17:1-18
Na. 3: Inatupasa Tuoneje Mifano Yoyote Ambayo Huenda Zamani Tuliheshimu Sana? (rs-SW uku. 199 fu. 4–uku. 200 fu. 2)
Na. 4: Utumizi wa Mifano Katika Ibada Ungeweza Kuathirije Wakati Ujao Wetu Wenyewe? (rs-SW uku. 200 fu. 3-6)
Mei 13 Usomaji wa Biblia: Yeremia 19-23
Wimbo Na. 73
Na. 1: Kiasi—Sifa Inayokuza Amani (w00-SW 3/15 uku. 21-24)
Na. 2: Yeremia 19:1-15
Na. 3: Je, Kweli Watu Hupata Uhuru Wanapotupilia Kando Viwango vya Biblia? (rs-SW uku. 118 fu. 2–uku. 119 fu. 1)
Na. 4: Shauri la Biblia Ni Nini Kuhusu Kufuatia Vitu vya Kimwili na Kutumia Kileo Mno? (rs-SW uku. 119 fu. 2-3)
Mei 20 Usomaji wa Biblia: Yeremia 24-28
Wimbo Na. 140
Na. 1: Mtu Aliye Mfano Bora Ambaye Alikubali Kusahihishwa (w00-SW 3/15 uku. 25-28)
Na. 2: Yeremia 25:1-14
Na. 3: Thamini Uhusiano Wako Pamoja na Yehova, na Uepuke Mashirika Mabaya (rs-SW uku. 120 fu. 2)
Na. 4: Ni Nani Aliyechochea Wanadamu Wapuuze Amri za Mungu? (rs-SW uku. 120 fu. 3–uku. 121 fu. 1)
Mei 27 Usomaji wa Biblia: Yeremia 29-31
Wimbo Na. 42
Na. 1: Roho ya Mungu Hutendaje Kazi Leo? (w00-SW 4/1 uku. 8-11)
Na. 2: Yeremia 30:1-16
Na. 3: Ni Mielekeo Gani Tunayopaswa Kuepuka? (rs-SW uku. 121 fu. 2-8)
Na. 4: Mtu Huwa Chini ya Utawala wa Nani Wakati Kujitegemea Kunapomwongoza Aige Ulimwengu? (rs-SW uku. 122 fu. 1-2)
Juni 3 Usomaji wa Biblia: Yeremia 32-35
Wimbo Na. 85
Na. 1: Farijiwa na Nguvu za Yehova (w00-SW 4/15 uku. 4-7)
Na. 2: Yeremia 34:1-16
Na. 3: Ni Wapi Ambapo Jina la Mungu Hupatikana Katika Tafsiri Zinazotumiwa na Watu Wengi Leo? (rs-SW uku. 420 fu. 4–uku. 422 fu. 8)
Na. 4: Kwa Nini Tafsiri Nyingi za Biblia Hazitumii Jina la Kibinafsi la Mungu? (rs-SW uku. 422 fu. 9–uku. 423 fu. 4)
Juni 10 Usomaji wa Biblia: Yeremia 36-40
Wimbo Na. 159
Na. 1: Je, Unawaona Wenye Jeuri Kama Mungu Awaonavyo? (w00-SW 4/15 uku. 26-29)
Na. 2: Yeremia 37:1-17
Na. 3: Ni Namna Ipi ya Jina la Mungu Iliyo Sahihi, Yehova au Yahweh? (rs-SW uku. 424 fu. 1–uku. 426 fu. 6)
Na. 4: Je, Yehova Katika “Agano la Kale” Ni Yesu Kristo Katika “Agano Jipya”? (rs-SW uku. 426 fu. 7–uku. 427 fu. 2)
Juni 17 Usomaji wa Biblia: Yeremia 41-45
Wimbo Na. 26
Na. 1: “Linda Moyo Wako” (w00-SW 5/15 uku. 20-24)
Na. 2: Yeremia 41:1-15
Na. 3: Mtu Anaweza Kumpendaje Yehova Ikiwa Pia Anapaswa Kumwogopa? (rs-SW uku. 427 fu. 3-4)
Na. 4: Ni Itikadi Gani za Mashahidi wa Yehova Zinazowaweka Tofauti na Dini Nyingine? (rs-SW uku. 179 fu. 1–uku. 180 fu. 6)
Juni 24 Usomaji wa Biblia: Yeremia 46-49
Wimbo Na. 15
Na. 1: Maisha Makamilifu Si Ndoto Tu! (w00-SW 6/15 uku. 5-7)
Na. 2: Yeremia 49:1-13
Na. 3: Je, Mashahidi wa Yehova Ni Dini ya Kimarekani? (rs-SW uku. 180 fu. 7–uku. 181 fu. 5)
Na. 4: Je, Mashahidi wa Yehova Ni Farakano? (rs-SW uku. 181 fu. 6–uku. 183 fu. 2)
Jul. 1 Usomaji wa Biblia: Yeremia 50-52
Wimbo Na. 100
Na. 1: Yeremia—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 129 fu. 36-39)
Na. 2: Yeremia 50:1-16
Na. 3: Je, Mashahidi wa Yehova Wanaamini Kwamba Dini Yao Tu Ndiyo ya Kweli? (rs-SW uku. 183 fu. 3-4)
Na. 4: Dini ya Kweli Hufuata Biblia (rs-SW uku. 183 fu. 5)
Jul. 8 Usomaji wa Biblia: Maombolezo 1-2
Wimbo Na. 8
Na. 1: Utangulizi wa Maombolezo (si-SW uku. 130-131 fu. 1-7)
Na. 2: Maombolezo 1:1-14
Na. 3: Mashahidi wa Yehova Hutumia Njia Gani ya Kueleza Biblia? (rs-SW uku. 184 fu. 1–uku. 185 fu. 1)
Na. 4: Kwa Nini Kumekuwako Mabadiliko Katika Mafundisho ya Mashahidi wa Yehova? (rs-SW uku. 185 fu. 2)
Jul. 15 Usomaji wa Biblia: Maombolezo 3-5
Wimbo Na. 145
Na. 1: Maombolezo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 132 fu. 13-15)
Na. 2: Maombolezo 3:1-30
Na. 3: Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Wanahubiri Nyumba kwa Nyumba? (rs-SW uku. 185 fu. 3–uku. 186 fu. 2)
Na. 4: Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Wananyanyaswa? (rs-SW uku. 186 fu. 4–uku. 187 fu. 1)
Jul. 22 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 1-6
Wimbo Na. 94
Na. 1: Utangulizi wa Ezekieli (si-SW uku. 132-133 fu. 1-6)
Na. 2: Ezekieli 4:1-17
Na. 3: b‘Kwa Nini Nyinyi Watu Hamshiriki Kusaidia Kufanya Ulimwengu Uwe Mahali Bora pa Kuishi?’ (rs-SW uku. 187 fu. 2–uku. 188 fu. 1)
Na. 4: c‘Wakristo Wanapaswa Kuwa Mashahidi wa Yesu, Si wa Yehova’ (rs-SW uku. 188 fu. 2)
Jul. 29 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 7-12
Wimbo Na. 221
Na. 1: Nufaika na Vielelezo Vizuri (w00-SW 7/1 uku. 19-21)
Na. 2: Ezekieli 10:1-19
Na. 3: Je, Yesu Kristo Alikuwa Mtu Halisi? (rs-SW uku. 428 fu. 1-4)
Na. 4: Je, Yesu Kristo Alikuwa Mtu Mwema Tu? (rs-SW uku. 429 fu. 1)
Ago. 5 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 13-16
Wimbo Na. 106
Na. 1: Unaweza Kudumisha Usafi wa Kiadili Katika Ulimwengu Usio na Maadili (w00-SW 7/15 uku. 28-31)
Na. 2: Ezekieli 13:1-16
Na. 3: Je, Yesu Alikuwa Kiongozi Mwingine wa Kidini Tu? (rs-SW uku. 429 fu. 2)
Na. 4: Kwa Nini Wayahudi kwa Ujumla Hawakumkubali Yesu? (rs-SW uku. 430 fu. 1-2)
Ago. 12 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 17-20
Wimbo Na. 214
Na. 1: Kwa Nini Tuheshimu Mamlaka? (w00-SW 8/1 uku. 4-7)
Na. 2: Ezekieli 17:1-18
Na. 3: Je, Kweli Yesu Kristo Ni Mungu? (rs-SW uku. 430 fu. 3–uku. 431 fu. 1)
Na. 4: Je, Yohana 1:1 Huthibitisha Kwamba Yesu Ni Mungu? (rs-SW uku. 431 fu. 3-5)
Ago. 19 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 21-23
Wimbo Na. 86
Na. 1: Unafanyaje Kunapotokea Kutoelewana? (w00-SW 8/15 uku. 23-25)
Na. 2: Ezekieli 22:1-16
Na. 3: Je, Maneno ya Tomasi Katika Yohana 20:28 Yanathibitisha Kwamba Yesu Ni Mungu Kwelikweli? (rs-SW uku. 432 fu. 1-3)
Na. 4: Je, Mathayo 1:23 Huonyesha Kwamba Yesu Alipokuwa Duniani Alikuwa Mungu? (rs-SW uku. 432 fu. 4–uku. 433 fu. 2)
Ago. 26 Pitio la Kuandika. Usomaji wa Biblia: Ezekieli 24-28
Wimbo Na. 18
Sept. 2 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 29-32
Wimbo Na. 40
Na. 1: Kwa Nini Uwe Mwenye Kujitolea? (w00-SW 9/15 uku. 21-24)
Na. 2: Ezekieli 30:1-19
Na. 3: Andiko la Yohana 5:18 Humaanisha Nini? (rs-SW uku. 433 fu. 3-4)
Na. 4: Je, Uhakika wa Kwamba Yesu Anaabudiwa Huthibitisha Kwamba Yeye Ni Mungu? (rs-SW uku. 433 fu. 5–uku. 434 fu. 2)
Sept. 9 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 33-36
Wimbo Na. 49
Na. 1: Jinsi Uwezavyo Kumkaribia Mungu (w00-SW 10/15 uku. 4-7)
Na. 2: Ezekieli 33:1-16
Na. 3: Je, Miujiza Iliyofanywa na Yesu Yathibitisha Kwamba Yeye Ni Mungu? (rs-SW uku. 434 fu. 3-5)
Na. 4: Je, Kumwamini Yesu Kristo Ndilo Takwa Pekee la Kupata Wokovu? (rs-SW uku. 435 fu. 2)
Sept. 16 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 37-40
Wimbo Na. 34
Na. 1: Unakadiriaje Mafanikio? (w00-SW 11/1 uku. 18-21)
Na. 2: Ezekieli 39:1-16
Na. 3: Je, Yesu Alikuwako Mbinguni Kabla ya Kuwa Binadamu? (rs-SW uku. 435 fu. 3-4)
Na. 4: Je, Yesu Ana Mwili Wenye Mnofu Mbinguni? (rs-SW uku. 436 fu. 1-4)
Sept. 23 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 41-45
Wimbo Na. 50
Na. 1: Tumikia Mungu kwa Moyo wa Kupenda (w00-SW 11/15 uku. 21-23)
Na. 2: Ezekieli 42:1-20
Na. 3: Je, Yesu Kristo Ni Yuleyule Mikaeli Malaika Mkuu? (rs-SW uku. 436 fu. 5–uku. 437 fu. 2)
Na. 4: d‘Ninyi Hamwamini Yesu’ (rs-SW uku. 437 fu. 3–uku. 438 fu. 2)
Sept. 30 Usomaji wa Biblia: Ezekieli 46-48
Wimbo Na. 112
Na. 1: Ezekieli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 137 fu. 29-33)
Na. 2: Ezekieli 46:1-15
Na. 3: e‘Je, Wewe Unamkubali Yesu Kuwa Mwokozi Wako wa Kibinafsi?’ (rs-SW uku. 438 fu. 3-4)
Na. 4: f‘Mimi Nimemkubali Yesu Kuwa Mwokozi Wangu wa Kibinafsi’ (rs-SW uku. 438 fu. 5)
Okt. 7 Usomaji wa Biblia: Danieli 1-4
Wimbo Na. 10
Na. 1: Utangulizi wa Danieli (si-SW uku. 138-139 fu. 1-6)
Na. 2: Danieli 1:1-17
Na. 3: Je, Wayahudi wa Leo Ni Watu wa Mungu Wachaguliwa? (rs-SW uku. 411 fu. 1–uku. 412 fu. 3)
Na. 4: Je, Wayahudi Wote Watageuzwa Kwenye Imani Katika Kristo? (rs-SW uku. 412 fu. 4–uku. 413 fu. 1)
Okt. 14 Usomaji wa Biblia: Danieli 5-8
Wimbo Na. 191
Na. 1: Je, Ni Lazima Sikuzote Uamini Kile Ambacho Watu “Wenye Hekima” Husema? (w00-SW 12/1 uku. 29-31)
Na. 2: Danieli 5:1-16
Na. 3: Je, Ni Lazima Wayahudi Wamwamini Yesu Ili Waokolewe? (rs-SW uku. 413 fu. 2-3)
Na. 4: Je, Matukio Yanayoendelea Katika Israeli Leo Ni Utimizo wa Unabii wa Biblia? (rs-SW uku. 413 fu. 4–uku. 414 fu. 4)
Okt. 21 Usomaji wa Biblia: Danieli 9-12
Wimbo Na. 108
Na. 1: Danieli—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 141-142 fu. 19-23)
Na. 2: Danieli 10:1-21
Na. 3: Je, Unabii Juu ya Kurudishwa kwa Israeli Unatimizwa Leo? (rs-SW uku. 415 fu. 1-4)
Na. 4: Je, Ufalme wa Mungu Ni Serikali Halisi? (rs-SW uku. 325 fu. 4–uku. 326 fu. 1)
Okt. 28 Usomaji wa Biblia: Hosea 1-14
Wimbo Na. 23
Na. 1: Utangulizi wa Hosea na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 143-145 fu. 1-8, 14-17)
Na. 2: Hosea 4:1-19
Na. 3: Ni Nani Watawala wa Ufalme wa Mungu? (rs-SW uku. 326 fu. 2-4)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Utakuwa na Matokeo Gani Juu ya Serikali za Wanadamu? (rs-SW uku. 327 fu. 1-2)
Nov. 4 Usomaji wa Biblia: Yoeli 1-3
Wimbo Na. 166
Na. 1: Utangulizi wa Yoeli na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 146-148 fu. 1-5, 12-14)
Na. 2: Yoeli 1:1-20
Na. 3: Ufalme wa Mungu Utatakasa Jina la Yehova (rs-SW uku. 327 fu. 3-5)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Utaunganisha Uumbaji Wote Katika Ibada Safi (rs-SW uku. 328 fu. 1-2)
Nov. 11 Usomaji wa Biblia: Amosi 1-9
Wimbo Na. 80
Na. 1: Utangulizi wa Amosi na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 148-150 fu. 1-6, 13-17)
Na. 2: Amosi 1:1-15
Na. 3: Ufalme wa Mungu Utaondoa Vita na Ufisadi (rs-SW uku. 328 fu. 3–uku. 329 fu. 1)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Utaandaa Chakula kwa Wote na Kuondoa Magonjwa (rs-SW uku. 329 fu. 2-4)
Nov. 18 Usomaji wa Biblia: Obadia 1-21–Yona 1-4
Wimbo Na. 96
Na. 1: Utangulizi wa Obadia na Yona na kwa Nini Ni Vyenye Mafaa (si-SW uku. 151-153 fu. 1-5, 10-14; uku. 153-155 fu. 1-4, 9-12)
Na. 2: Obadia 1:1-16
Na. 3: Ufalme wa Mungu Utaandaa Nyumba, Kazi, na Usalama kwa Wote (rs-SW uku. 329 fu. 5–uku. 330 fu. 2)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Utafanya Kuwe na Uadilifu na Haki (rs-SW uku. 330 fu. 3-5)
Nov. 25 Usomaji wa Biblia: Mika 1-7
Wimbo Na. 138
Na. 1: Utangulizi wa Mika na kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 155-158 fu. 1-8, 16-19)
Na. 2: Mika 1:1-16
Na. 3: Ufalme wa Mungu Utafufua Wafu (rs-SW uku. 330 fu. 6–uku. 331 fu. 2)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Utafanya Kuwe na Ulimwengu Wenye Upendo na Upatano (rs-SW uku. 331 fu. 3-5)
Des. 2 Usomaji wa Biblia: Nahumu 1-3–Habakuki 1-3
Wimbo Na. 137
Na. 1: Utangulizi wa Nahumu na Habakuki na kwa Nini Ni Vyenye Mafaa (si-SW uku. 158-160 fu. 1-7, 11-12; uku. 161-163 fu. 1-5, 12-14)
Na. 2: Nahumu 3:1-19
Na. 3: Ufalme wa Mungu Utafanya Dunia Iwe Paradiso (rs-SW uku. 331 fu. 6–uku. 332 fu. 2)
Na. 4: Je, Ufalme wa Mungu Ulianza Kutawala Katika Karne ya Kwanza? (rs-SW uku. 332 fu. 3-5)
Des. 9 Usomaji wa Biblia: Sefania 1-3–Hagai 1-2
Wimbo Na. 146
Na. 1: Utangulizi wa Sefania na wa Hagai na kwa Nini Ni Vyenye Mafaa (si-SW uku. 163-166 fu. 1-6, 10-12; uku. 166-168 fu. 1-7, 13-16)
Na. 2: Sefania 2:1-15
Na. 3: Je, Kutawala kwa Ufalme wa Mungu Ni Lazima Kungojee Mgeuzo wa Ulimwengu? (rs-SW uku. 333 fu. 1-2)
Na. 4: g‘Ufalme wa Mungu Hautakuja Wakati wa Maisha Yangu’ (rs-SW uku. 333 fu. 4-5)
Des. 16 Usomaji wa Biblia: Zekaria 1-8
Wimbo Na. 1
Na. 1: Utangulizi wa Zekaria (si-SW uku. 168-169 fu. 1-7)
Na. 2: Zekaria 6:1-15
Na. 3: Ni Nini Kinachoonyesha Kwamba Tunaishi Katika Siku za Mwisho? (rs-SW uku. 297 fu. 1)
Na. 4: Ni kwa Njia Gani Vita na Upungufu wa Chakula Ni Sehemu ya ile “Ishara”? (rs-SW uku. 297 fu. 2–uku. 298 fu. 3)
Des. 23 Usomaji wa Biblia: Zekaria 9-14
Wimbo Na. 176
Na. 1: Zekaria—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 171-172 fu. 23-27)
Na. 2: Zekaria 9:1-17
Na. 3: Andiko la Luka 21:11 Limetimizwaje Tangu 1914? (rs-SW uku. 299 fu. 1-3)
Na. 4: Ongezeko la Kutotii Sheria Laonyesha Nini? (rs-SW uku. 299 fu. 4–uku. 300 fu. 1)
Des. 30 Pitio la Kuandika. Usomaji wa Biblia: Malaki 1-4
Wimbo Na. 118
[Maelezo ya Chini]
a Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.
b Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.
c Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.
d Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.
e Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.
f Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.
g Wakati ukiruhusu, mwanafunzi apaswa kujibu vipingamizi vya mwenye nyumba na mambo kama hayo na kadhalika, ili kufaana na mahitaji ya eneo lenu.