Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 1/02 uku. 8
  • Mambo ya Kusema Kuhusu Magazeti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mambo ya Kusema Kuhusu Magazeti
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2002
Huduma Yetu ya Ufalme—2002
km 1/02 uku. 8

Mambo ya Kusema Kuhusu Magazeti

Mnara wa Mlinzi Jan. 1

“Je, wewe hujiuliza ni kwa nini watu wengine huwa na maisha mazuri hali wengine hupambana na hali ili kupata riziki? Biblia inatoa jibu. [Soma Ayubu 34:19.] Gazeti hili linazungumzia jinsi ambavyo Mungu anakusudia kukomesha ubaguzi wa kijamii.”

Amkeni! Jan. 8

“Sisi sote tumesikia kuhusu ule msiba uliotikisa ulimwengu. Tangu wakati huo, watu wamehitaji faraja na msaada mwingi. Makala hii yaeleza kile ambacho Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakifanya ili kusaidia waokokaji wa msiba huo, wafanyakazi wa dharura, na wale waliofiwa.”

Mnara wa Mlinzi Jan. 15

“Watu wengi hutumia sanamu katika ibada yao. Je, wafikiri vitu hivyo vina nguvu za kuokoa? [Ngoja jibu.] Tafadhali ona yale ambayo Mungu wa kweli atatufanyia. [Soma Ufunuo 21:3, 4.] Ni Mungu wa kweli tu atakayeweza kufanya hivyo. Gazeti hili laonyesha yeye ni nani na jinsi tunavyoweza kunufaika kwa kumtumaini yeye.”

Amkeni! Jan. 22

“Huenda tukakosa kuthamini sana makao yetu. Lakini mamilioni ya wakimbizi ulimwenguni pote hurandaranda bila tumaini, nao hawapati usalama wanaotafuta. Gazeti Amkeni! lachunguza sababu ya kuwapo kwa tatizo hilo na pia ahadi ya Biblia kwamba siku moja kila mtu atakuwa na makao ya kudumu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki