Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/02 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2002
Huduma Yetu ya Ufalme—2002
km 4/02 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Januari 7 hadi Aprili 22, 2002. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu ya maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kwenye Mhubiri 2:2, Solomoni anasema kwamba kicheko na furaha zapaswa kuepukwa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 9/15 uku. 24 fu. 5.]

2. Kitabu cha Mhubiri si kitabu chenye kuvunja moyo, bali kimejaa hekima ya kimungu na kinaonyesha kwamba misiba inaletwa na shughuli zinazompuuza Mungu. [si-SW uku. 114 fu. 15]

3. Kwenye Isaya 1:7; nabii anataja ukiwa wa Yuda wakati wa utawala wa Ahazi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 17 fu. 16.]

4. ‘Kusimama mbele ya kiti cha ufalme na mbele ya Mwana-Kondoo,’ kama inavyotajwa katika Ufunuo 7:9, humaanisha kusimama mahali fulani mbinguni. [rs-SW uku. 195 fu. 2]

5. ‘Tukimheshimu Yehova’ kwa ukarimu na wakati wetu, na vipawa vyetu, nguvu zetu, na mali zetu, tutapokea baraka tele za kiroho kutoka kwake. (Mit. 3:9, 10) [w00-SW 1/15 uku. 25 fu. 1]

6. Katika siku zetu ‘tendo la ajabu na kazi ya ajabu’ iliyotabiriwa kwenye Isaya 28:21 hurejezea kuharibiwa kwa mataifa kwenye Har–Magedoni. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 295 fu. 16; uku. 301 fu. 28.]

7. Kama vile Mathayo 24:38, 39 inavyoonyesha, kula na kunywa, pamoja na matendo mengine ambayo watu hufanya, yalifanya watu wa siku za Noa wafagiliwe mbali na Gharika. [w00-SW 2/15 uku. 6 fu. 6]

8. Yehova hujibu sikuzote sala za watumishi wake wanyenyekevu ambao humtumikia bila ubinafsi. [w00-SW 3/1 uku. 4 fu. 3]

9. “Mataifa” wanaorejezewa kwenye Isaya 60:3 ni mataifa yote yakiwa mazima-mazima ambayo yamevutiwa na nuru ya Mungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w00-SW 1/1 uku. 12 fu. 4.]

10. Yehova ‘alimtakasa’ Yeremia kabla ya kuzaliwa kwa kuwa Aliamua kimbele jinsi maisha yake ya wakati ujao yatakavyokuwa. (Yer. 1:5) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 4/1 uku. 10 fu. 2.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Kwenye Mhubiri 11:1, NW, ni nini kinachomaanishwa na ‘kutupa mkate’? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 9/15 uku. 25 fu. 11.]

12. Kwenye Isaya 6:8, Yehova anatia ndani nani anaposema “yetu”? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 94-95 fu. 13.]

13. Katika utimizo wa Isaya 9:2, “nuru kuu” iling’aaje Galilaya? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 126 fu. 17.]

14. Siku hizi ni nini kinachoweza kulinganishwa na kuanguka kwa Babiloni katika mwaka wa 539 K.W.K. na hatimaye kuachwa kwake ukiwa kabisa? (Isa. 13:19, 20; 14:22, 23) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 188 fu. 30-31.]

15. “Mtumwa mwaminifu na mwenye busara” ametendaje kama “mlinzi” anayefafanuliwa kwenye Isaya 21:6? (Mt. 24:45) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 221-222 fu. 11.]

16. Ni shauri gani lenye hekima linalopatikana katika Mithali 31:10 analopewa kijana mwanamume anayetafuta mwenzi wa ndoa? [w00-SW 2/1 uku. 31 fu. 1]

17. Kwenye Isaya 43:9, miungu ya mataifa inapewa mwito gani wa ushindani? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 2/1 uku. 16 fu. 3.]

18. Miguu ya wale wanaotangaza habari njema za Ufalme wa Mungu ni “mizuri” kwa njia gani? (Isa. 52:7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 4/15 uku. 27 fu. 6.]

19. Ni lazima tufanye nini ili moyo wetu usitudanganye? (Yer. 17:9) [w00-SW 3/1 uku. 30 fu. 4]

20. Ni lazima wale ‘wanaotembea katika njia ya Yehova’ wafanye nini? (Yer. 7:23) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w99-SW 8/15 uku. 29 fu. 6.]

Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. “Moyo wake mwenye hekima uko upande wa kuume” katika maana ya kwamba “upande wa kuume” mara nyingi huonyesha _________________________ ; hivyo, hiyo yaonyesha kwamba _________________________ wake humchochea kufuatia mwenendo mwema unaofaa. (Mhu. 10:2; Mt. 25:33) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 9/15 uku. 25 fu. 9.]

22. Baadhi ya masomo yenye faida yanayofundishwa katika Wimbo Ulio Bora ni _________________________ , _________________________ , na _________________________ kwa kanuni za kimungu. [si-SW uku. 117 fu. 16]

23. Yule aharibuye majiji ya Yuda, anayefafanuliwa kwenye Isaya 33:1, ni taifa la _________________________ , ambalo lenyewe lilishindwa mwaka wa 632 K.W.K., na kuacha mateka mengi ambayo wakazi wa _________________________ , ‘wangeyakusanya kama mende.’ (Isa. 33:4, NW) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 343 fu. 4; uku. 345 fu. 6.]

24. Andiko la Isaya 54:1, (NW), likilinganishwa na Wagalatia 4:26, 27 huonyesha kwamba “mwanamke tasa” hufananisha “ _________________________ ”; na “mwanamke aliye na mume anayemmiliki,” lile _________________________ . [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 8/1 uku. 11 fu. 8.]

25. Tunapodhihakiwa na kukataliwa katika huduma yetu ya hadharani, twahitaji kukumbuka kwamba si _________________________ tunaopingwa, bali ni _________________________ , Chanzo cha ujumbe wetu. (2 Kor. 4:1, 7) [w00-SW 1/15 uku. 21 fu. 1]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Alipokuwa akiandika kuhusu ono la utukufu wa kimbingu wa Yesu, Paulo alijitaja kuwa yule “aliyezaliwa kabla ya wakati wake,” akimaanisha kwamba (alikuwa ametoka tu kuzaliwa kiroho; aliwekwa mapema kuwa mtume wa mataifa; ilikuwa kana kwamba amepewa heshima ya kuzaliwa, au kufufuliwa, kwenye uhai wa roho kabla ya wakati wake.) (1 Kor. 9:1; 15:8) [w00-SW 1/15 uku. 29 fu. 6]

27. Jina la cheo “Baba wa milele” larejezea nguvu na mamlaka ya Mfalme wa Kimesiya ya kuwapa wanadamu (nguvu za kiroho; uhai usioweza kuharibika mbinguni; tazamio la uhai wa milele duniani). (Isa. 9:6; Yn. 11:25, 26) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 131 fu. 26.]

28. Katika utimizo wa kisasa wa Isaya 66:7, “mtoto mwanamume” aliyezaliwa anawakilisha (Yesu Kristo, Ufalme wa Kimesiya; taifa jipya la kiroho lililozaliwa mwaka wa 1919). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 1/1 uku. 11 fu. 3.]

29. Kusoma kwa makini Mathayo 10:28 hutusaidia kuona kwamba Gehena yenye moto (ni mahali pa mateso; hufananisha uharibifu wa milele; humaanisha kutengwa na Mungu.) [rs-SW uku. 210 fu. 1]

30. Katika utimizo wa kisasa, ‘taifa lisilosikiliza sauti ya Yehova,’ linalotajwa kwenye Yeremia 7:28, larejezea (Babiloni Mkubwa; Jumuiya ya Wakristo; serikali ya saba ya ulimwengu). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 4/1 uku. 18 fu. 10.]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Mit. 24:16; Mhu. 3:11; Isa. 40:8; Rom. 10:15; 1 Pet. 4:6

31. Kila kazi ya Mungu inayopatana na kusudi lake itafunuliwa kwa wakati wake. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 9/15 uku. 24 fu. 8.]

32. Kuwahubiria waliokufa kiroho habari njema huwapa fursa ya kutubu. [rs-SW uku. 191 fu. 1]

33. Ijapokuwa vipingamizi katika maisha haviepukiki, mtu mwenye kumcha Mungu hakati tamaa katika kujitahidi kufanya lililo jema. [w00-SW 2/1 uku. 5 fu. 1]

34. Neno la Mungu, au kusudi lake lililotaarifiwa, haliwezi kubatilishwa wala kuzuiwa lisitimie. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona ip-1-SW uku. 401-402 fu. 10.]

35. Mitume wa Yesu walitumia sana unabii wa Isaya katika huduma yao. [si-SW uku. 123 fu. 37]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki