Barua Kutoka Kwa Ofisi ya Tawi
Wahubiri wa Ufalme Wapendwa:
Upanuzi mkubwa wa kiwanda cha Wallkill, Marekani, umekamilika na kinatumika sasa. Mashine mbili mpya za kuchapa, kila mashine ikiwa na uwezo wa kuchapa magazeti yapatayo 90,000 kwa saa tayari zimewekwa, na vilevile mashine mpya ambazo kwa dakika moja zinaweza kujalidi vitabu 120 hivi vya jalada gumu.
Katika nchi jirani, ujenzi wa ofisi mpya za tawi unaendelea na umefikia hatua zifuatazo: Ujenzi wa Ofisi ya Tawi ya Burundi unaendelea vizuri. Asilimia 90 ya kazi ya Ujenzi wa Jumba la Kusanyiko na Karakana imemalizika, na jengo la Makazi lenye ghorofa tatu linajengwa sasa. Mnamo Oktoba 2003 Ofisi ya Tawi ya Tanzania ilinunua uwanja wenye ukubwa wa ekari 7.5 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya tawi. Kutakuwa na Jengo la Usimamizi lenye ghorofa mbili na majengo matatu ya makazi yanayoweza kutoshea Wanabetheli 52. Jumba la Ufalme pia litajengwa kwenye uwanja huo. Nchini Uganda, ukuta wa kuzunguka uwanja ulianza kujengwa mwanzoni mwa mwezi wa Juni. Ujenzi wa ofisi ya tawi umepangiwa kuanza baadaye mwaka huu.
Kulikuwa na utendaji mwingi wakati wa majira ya Ukumbusho katika eneo la Afrika Mashariki. Kulikuwa na vilele vipya vya mapainia wasaidizi na idadi ya wale waliohudhuria mwadhimisho wa Mlo wa Jioni wa Bwana.
Pamoja nanyi, tunatazamia ‘kuwa na mengi ya kufanya katika kazi ya Bwana’ tunapoanza mwaka wa utumishi wa 2005.—1 Kor. 15:58.
Ndugu zenu,
Ofisi ya Tawi ya Burundi, Kenya, Tanzania, na Uganda