Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/04 uku. 7
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2004
  • Vichwa vidogo
  • SIFA ZA USEMI
Huduma Yetu ya Ufalme—2004
km 10/04 uku. 7

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatashughulikiwa kwa njia ya maswali na majibu katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanzia Oktoba 25, 2004. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 30 linalotegemea habari zilizozungumziwa kwenye hotuba zilizotolewa kuanzia juma la Septemba 6 hadi Oktoba 25, 2004. [Taarifa: Mahali ambapo vitabu vya marejeo havijatajwa baada ya swali, utahitaji kufanya utafiti wako mwenyewe ili kupata majibu.—Ona Shule ya Huduma, uku. 36-37.]

SIFA ZA USEMI

1. Tunawezaje kuwa wenye kutia moyo tunapotoa hotuba inayohusiana na sehemu fulani ya utendaji wetu wa Kikristo? [be uku. 203 fu. 3-4]

2. Kurudia ni nini, na kwa nini ni muhimu? [be uku. 206 fu. 1-4]

3. Tunawezaje kukazia kichwa kikuu cha hotuba zetu? [be uku. 210 fu. 1-5, sanduku]

4. Tunaweza kutambuaje mambo makuu katika hotuba tuliyopewa? [be uku. 212 fu. 1-4]

5. Kwa nini tunapaswa kuwa waangalifu tusiwe na mambo makuu mengi mno? [be uku. 213 fu. 2-4]

HOTUBA NA. 1

6. Ni maendeleo gani yaliyokuwako kabla ya Furiko ambayo huenda yalifanya iwe vigumu kwa watu kuamini kwamba ulimwengu uliowazunguka ungefikia kikomo? [w02 3/1 uku. 5-6]

7. Kwa nini watu wa siku za Yesu walimwita “Mwalimu” na wala si “Mponyaji”? (Luka 3:12; 7:40) [w02 5/1 uku. 4 fu. 3; uku. 6 fu. 6]

8. Andiko la Methali 11:24, 25 linakaziaje umuhimu wa kushiriki kikamili katika huduma ya shambani? [w02 7/15 uku. 30 fu. 3-5]

9. Ni suala gani kuhusu mema na mabaya lililozushwa na uasi uliotokea Edeni, na uasi huo umekuwa na matokeo gani? (Mwa. 3:1-6) [w02 10/1 uku. 5 fu. 6; uku. 6 fu. 2-3]

10. Tarehe ya kurejeshwa kwa ibada ya kweli katika Yerusalemu huamuliwaje? [si uku. 285 fu. 5]

USOMAJI WA BIBLIA WA KILA JUMA

11. Kwa kuwa Yehova alimwambia Balaamu aende pamoja na watu wa Balaki, kwa sababu gani Yeye alikasirika wakati nabii huyo alipoenda pamoja nao? (Hes. 22:20-22)

12. Je, mume wa mwanamke Mkristo anaweza kumfungua kutoka kwa nadhiri zake? (Hes. 30:6-8)

13. ‘Majiji ya makimbilio’ yanafananisha nini leo? (Hes. 35:6) [w95 11/15 uku. 17 fu. 8]

14. Je, amri inayopatikana katika Kumbukumbu la Torati 6:6-9 ya ‘kufunga sheria ya Mungu kama utepe kwenye mkono na kichwa,’ yapaswa kueleweka kihalisi?

15. Je, usemi “nguo yako ya kujitanda haikuchakaa” ulimaanisha kwamba Waisraeli walipewa mavazi mengine? (Kum. 8:4)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki