Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/06 uku. 7
  • Sanduku la Swali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sanduku la Swali
  • Huduma ya Ufalme—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Kazi za Ufalme Zinavyogharimiwa
    Ufalme wa Mungu Unatawala!
  • Yote Hayo Hugharimiwaje?
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Yehova Huwapenda Watoaji Wachangamfu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Kazi Yetu ya Ulimwenguni Pote Inagharimiwaje?
    Ni Nani Wanaofanya Mapenzi ya Yehova Leo?
Pata Habari Zaidi
Huduma ya Ufalme—2006
km 12/06 uku. 7

Sanduku la Swali

◼ Je, ingefaa kuchangisha pesa kwa ajili ya kutaniko kwa kuuza bidhaa zilizotumika au kutumia njia nyingine ya kuchangisha?

Ni jambo la kawaida kwa mashirika ya kidini kuchangisha pesa kupitia mbinu mbalimbali kama vile, kuuza milo, bidhaa, au kuwa na sherehe fulani. Ingawa huenda wengine wakahisi kwamba inafaa kufanya hivyo, njia hizo zote ni mbinu za kuomba-omba. Mashahidi wa Yehova hawapokei msaada wa kifedha kwa njia hiyo.

Toleo la pili la Mnara wa Mlinzi la Agosti 1879, lilisema hivi kuhusu sababu ya kukataa kuiga tabia ya makanisa ya kuomba-omba pesa: “‘Tunaamini kwamba Zion’s Watch Tower’ linategemezwa na YEHOVA, na kwa sababu hiyo halitawahi kuwaomba-omba au kuwasihi wanadamu walitegemeze. Yule anayesema: ‘Dhahabu na fedha zote za milimani ni zangu,’ asipotuandalia pesa tunazohitaji, tutaelewa kwamba ni wakati wa kuacha kuchapa.”

Tunaendelea kufuata kanuni ya Kimaandiko: “Kila mmoja na afanye kama alivyoazimia moyoni mwake, si kwa kutopenda wala kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda mtoaji mchangamfu.” (2 Kor. 9:7) Masanduku ya mchango huwekwa katika Jumba la Ufalme ili yeyote anayetaka atoe mchango wa hiari. (2 Fal. 12:9) Hatuombi-ombi michango; wala haitolewi mtu akitazamia atapata kitu kwa sababu ya kufanya hivyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki