Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 2/08 uku. 9
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2008
Huduma Yetu ya Ufalme—2008
km 2/08 uku. 9

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatashughulikiwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Februari 25, 2008. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 30 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Januari 7 hadi Februari 25, 2008.

SIFA ZA USEMI

1. Tunahitaji kufanya nini ili kuwasaidia wasikilizaji wetu waelewe maana ya maandiko, na kwa nini tufanye hivyo? [be uku. 228 fu. 2-3]

2. Kwa nini ni muhimu tutoe hotuba inayoelimisha wasikilizaji wetu, na tunaweza kufanyaje hivyo? [be uku. 230 fu. 3-5, sanduku]

3. Kufanya utafiti kutatusaidiaje kufanya hotuba zetu ziwe zenye kuelimisha? [be uku. 231 fu. 1-3]

4. Tunaweza kutumiaje maandiko ambayo wasikilizaji wanayajua kwa njia inayoelimisha? [be uku. 231 fu. 4-5]

5. Kwa nini ni muhimu kusababu baada ya kusoma maandiko? [be uku. 232 fu. 3-4]

HOTUBA NA. 1

6. Ni nini kinachoonyesha kwamba mwandikaji wa kitabu cha Mathayo alikiandika hasa akiwafikiria Wayahudi? [si uku. 176 fu. 6-7]

7. Tunaweza kutayarishaje mioyo yetu kupokea maagizo ambayo Mungu anaandaa kupitia wasemaji jukwaani? (2 Nya. 20:33) [be uku. 13 fu. 4–uku. 14 fu. 5]

8. Wazazi wanaweza kuwazoezaje watoto wao kuwa wenye “hekima kwa ajili ya wokovu”? (2 Tim. 3:15) [be uku. 16 fu. 3-4]

9. Gospeli ya Mathayo inakaziaje utimizo wa unabii wa Biblia? [si uku. 181 fu. 32]

10. Ingawa Gospeli ya Mathayo inamwonyesha Yesu kuwa Mesiya na Mfalme aliyeahidiwa, Gospeli ya Marko inamfafanuaje? [si uku. 182 fu. 7-8]

USOMAJI WA BIBLIA WA KILA JUMA

11. Je, kuonyesha ghadhabu ni jambo zito kuliko kuendelea kuwa na ghadhabu? (Mt. 5:21, 22) [w08 1/15 “Neno la Yehova Liko Hai—Mambo Makuu Katika Kitabu cha Mathayo”]

12. Wakristo hudumishaje ‘jicho rahisi’? (Mt. 6: 22, 23) [w06 10/1 uku. 29]

13. Yesu alikuwa akikazia nini alipowauliza wanafunzi wake: “Je, mmeelewa maana ya mambo haya yote?” (Mt. 13:51, 52) [w08 1/15 “Neno la Yehova Liko Hai—Mambo Makuu Katika Kitabu cha Mathayo”]

14. Kwa nini Yesu mara nyingi aliwaagiza wale aliowaponya “wasifunue habari zake”? (Mt. 12:16) [w87 5/15 uku. 9; cl uku. 94]

15. Yesu alikuwa akimaanisha nini alipotaja “kipimo” ambacho mtu ‘anapimia’? (Marko 4:24, 25) [w80-SW 12/1 uku. 9 au w80-E 6/15 uku. 12; gt sura ya 43]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki