Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Februari 23, 2009. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Januari 5 hadi Februari 23, 2009.
1. Mungu angewezaje kutokeza nuru katika siku ya kwanza ikiwa alifanya mianga siku ya nne? (Mwa. 1:3, 16) [w04 1/1 uku. 28 fu. 5]
2. Kwa nini Noa alimlaani Kanaani? (Mwa. 9:20-25) [w04 1/1 uku. 31 fu. 2]
3. Agano la Abrahamu lilianza kufanya kazi wakati gani, na litaendelea kwa muda gani? (Mwa. 12:1-4) [w04 1/15 uku. 27 fu. 1; w01 8/15 uku. 17 fu. 13]
4. Ni nini kinachothibitisha kwamba Nimrodi na wale waliomfuata walishindwa ‘kujifanyia jina maarufu’? (Mwa. 11:4) [w98 3/15 uku. 25]
5. Kwa kuwa Loti anaitwa “mwadilifu” katika 2 Petro 2:7, huenda ni kwa nini aliwatoa binti zake kwa umati wa watu waliopotoka? (Mwa. 19:8) [w05 2/1 uku. 26 fu. 15-16; w04 1/15 uku. 27 fu. 3]
6. Kwa kuwa waume wanaomwogopa Mungu wanapaswa kuwatunza watu wa familia yao, kwa nini Abrahamu alimfukuza Hagari na Ishmaeli wakaenda nyikani? (Mwa. 21:10-21; 1 Tim. 5:8) [w88 2/15 uku. 31]
7. Tunajifunza masomo gani kutokana na jitihada ya Eliezeri ya kufanya mambo kwa njia ya Yehova alipomtafutia Isaka mke? (Mwa. 24:14, 15, 17-19, 26, 27) [w97 1/1 uku. 31 fu. 2]
8. Ndoto ya Yakobo ya malaika ‘wakipanda na kushuka juu ya ngazi’ ilimaanisha nini? (Mwa. 28:10-13) [w03 10/15 uku. 28 fu. 4; it-2 uku. 189]
9. Kwa nini Raheli alitaka sana dudai za mwana wa Lea? (Mwa. 30:14, 15) [w04 1/15 uku. 28 fu. 7]
10. Kwa nini Yakobo aliweka mfano mzuri katika kusuluhisha mizozo ya kibinafsi? (Mwa. 33:3, 4) [g83 04-SW uku. 10 fu. 4-6]