Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
1. Tunaweza kujifunza nini kutokana na amri iliyo katika andiko la Kutoka 23:19? [w06 4/1 uku. 31 fu. 1-5]
2. Urimu na Thumimu zilikuwa nini, na zilitumiwaje katika Israeli la kale? (Kut. 28:30) [w06 1/15 uku. 18; w01 9/1 uku. 27]
3. Yehova alizungumzaje na Musa “uso kwa uso”? (Kut. 33:11, 20) [w04 3/15 uku. 27]
4. Tunajifunza nini kutokana na jinsi Waisraeli walivyochanga kwa ukarimu mali na ustadi wao ili wajenge maskani? (Kut. 35:5, 10) [w99 11/1 uku. 31 fu. 1-2]
5. Kisitiri kinachotajwa katika andiko la Kutoka 40:28 kinawakilisha nini katika hekalu kubwa la kiroho la Mungu? [w00 1/15 uku. 15 fu. 7-8]
6. “Toleo la kuteketezwa” lililotolewa kwa kuteketeza sehemu zote kwenye madhabahu lilirejelea nini kuhusiana na dhabihu ya Yesu? (Law. 1:13) [w04 5/15 uku. 21 fu. 3]
7. Tunapaswa kuyaelewaje maneno “mafuta yote ni ya Yehova”? (Law. 3:16, 17) [w04 5/15 uku. 22 fu. 2]
8. Ni nini maana ya kumimina damu kwenye msingi wa madhabahu na kuitia juu ya vitu mbalimbali? (Law. 9:9) [w04 5/15 uku. 22 fu. 5]
9. Andiko la Mambo ya Walawi 12:8 linaonyesha nini kuhusu malezi ya Yesu, na tunajifunza nini kutokana na hilo? [w98 12/15 uku. 6 fu. 5]
10. Matumizi ya dhabihu ya fidia ya Yesu yaliwakilisha nini katika Siku ya Upatanisho ya kila mwaka? (Law. 16:11-16) [w98 2/15 uku. 12 fu. 2]