Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/11 uku. 1
  • Ushahidi Mkubwa Utatolewa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ushahidi Mkubwa Utatolewa
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Wakaribishe Kwa Uchangamfu!
    Huduma ya Ufalme—2013
  • Tunaweza Kuwasaidiaje Watakaohudhuria Ukumbusho?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2008
  • Karibisha Wageni
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Wafanye Wahisi Wamekaribishwa Kwenye Ukumbusho
    Huduma Yetu ya Ufalme—1994
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2011
km 4/11 uku. 1

Ushahidi Mkubwa Utatolewa

1. Zaidi ya hotuba, ni mambo gani mengine yanayoweza kuwavutia watu wanaohudhuria Ukumbusho? Eleza.

1 Lini? Katika jioni ya Ukumbusho. Tumejitahidi sana kuwaalika watu wahudhurie pamoja nasi. Si mambo ambayo wageni watasikia tu yatakayowavutia. Baada ya kuhudhuria Ukumbusho, mwanamke mmoja alitaja kwamba alivutiwa hasa na mambo aliyojionea, yaani, urafiki wa wote waliohudhuria, usafi, na uzuri wa jumba lililojengwa na linalotunzwa na watu wa kujitolea. Kwa hiyo, si msemaji tu, bali sisi sote tutachangia kutoa ushahidi kwenye tukio hili lililo muhimu kuliko matukio mengine yote katika mwaka.—Efe. 4:16.

2. Kila mmoja wetu anaweza kuwatolea wageni ushahidi jinsi gani?

2 Wasalimu Wageni kwa Urafiki: Wageni watatolewa ushahidi kwa tabasamu zetu na salamu zetu za uchangamfu. (Yoh. 13:35) Hata kama hutaweza kuzungumza na kila mtu, unaweza kujitambulisha kwa urafiki kwa watu wanaokaa karibu nawe. (Ebr. 13:1, 2) Uwe macho kuona kama kuna wageni wanaoonekana hawafahamu mtu yeyote. Yamkini walipata mwaliko tuliposambaza mialiko. Unaweza kuuliza, “Ni mara yenu ya kwanza kufika?” Waombe wakae karibu nawe, na uwe tayari kujibu maswali yoyote ambayo huenda wako nayo. Iwapo kutaniko lenu linahitaji kuondoka haraka ili kutaniko lingine liingie, huenda ukasema hivi: “Ningependa kusikia maoni yenu kuhusu hotuba. Ninaweza kuwasiliana nanyi kwa njia gani?”

3. Tunaweza kusema nini tunapowasalimu wahubiri wasiotenda?

3 Wasalimu Wasiotenda kwa Uchangamfu: Bila shaka wahubiri kadhaa wasiotenda watakuwapo, na pia watu ambao hawahudhurii mikutano mingine ila Ukumbusho. Wasalimu kwa uchangamfu, na uwaambie kwamba umefurahi sana kuwaona. (Rom. 15:7) Wazee wanaweza kuwatembelea muda mfupi baadaye ili kuwatia moyo wahudhurie mikutano. Ni matumaini yetu kwamba watu wengi watakaohudhuria watasukumwa kumsifu Mungu, si kwa sababu tu ya mambo ambayo watasikia, bali pia kwa sababu ya ‘matendo yetu mazuri ambayo wameshuhudia kwa macho.’—1 Pet. 2:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki