Young People Ask—How Can I Make Real Friends?
Yehova aliwaumba wanadamu washirikiane na kufanya urafiki. (Met. 17:17; 18:1, 24) Ili sote tunufaike na mahusiano hayo, ni lazima tuchague marafiki wetu kwa uangalifu. (Met. 13:20) Baada ya kutazama video Young People Ask—How Can I Make Real Friends?, je, unaweza kujibu maswali yafuatayo?
Utangulizi (Introduction):
(1) Rafiki wa kweli ni yupi?
Vipingamizi vya Kupata Marafiki (Roadblocks to Friendship):
(2) Tunaweza kushindaje hisia za kupuuzwa? (Flp. 2:4) (3) Kwa nini tunapaswa kuwa tayari kuboresha utu wetu, na ni nani anayeweza kutusaidia kufanya hivyo? (2 Kor. 13:11) (4) Tunaweza kupataje fursa za kupata marafiki wengi zaidi?—2 Kor. 6:13.
Urafiki Pamoja na Mungu (Friendship With God):
(5) Tunaweza kukuzaje uhusiano wa karibu pamoja na Yehova, na kwa nini jitihada hizo si za bure? (Zab. 34:8) (6) Tunapomfanya Yehova kuwa rafiki yetu mkubwa, ni urafiki gani wenye manufaa pamoja na wengine tunaoweza kupata?
Marafiki Wabaya (The Wrong Kind of Friends):
(7) Ni nani walio mashirika mabaya? (1 Kor. 15:33) (8) Marafiki wabaya wanawezaje kumwangamiza mtu kiroho?
Drama ya Kisasa (A Modern-Day Drama):
(9) Simulizi la Biblia kuhusu Dina linatufundisha nini? (Mwa. 34:1, 2, 7, 19) (10) Tara aliuteteaje urafiki wake pamoja na vijana walimwengu? (11) Huko shuleni, marafiki wa Tara walimweka kwenye hatari gani? (12) Kwa nini wazazi wa Tara walishindwa kutambua hatari aliyokuwa akikabili, lakini walipotambua tatizo hilo walimsaidiaje kujenga tena uhusiano wake pamoja na Yehova? (13) Dada mmoja painia alithibitikaje kuwa rafiki wa kweli wa Tara? (14) Hatimaye Tara alibadilisha maoni yake kuhusu nini?
Umalizio (Conclusion):
(15) Umejifunza mambo gani kutokana na video hii? (16) Unaweza kuitumiaje video hii kuwasaidia wengine?
Sote na tuchague marafiki watakaotusaidia kudumisha urafiki bora kuliko wote—urafiki pamoja na Mungu!—Zab. 15:1, 4; Isa. 41:8.