Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Februari 23, 2015.
Majiji ya makimbilio katika Israeli la kale yalitofautianaje na maficho ya wahalifu ya wapagani? (Yos. 20:2, 3) [Jan. 5, w10 11/1 uku. 15 fu. 4-6]
Kwa nini Yoshua alisema kwa uhakika kabisa maneno yaliyo kwenye andiko la Yoshua 23:14, na kwa nini tunaweza kuamini kabisa ahadi za Yehova? [Jan. 12, w07 11/1 uku. 26 fu. 19]
Kwa nini kabila la Yuda linatajwa kuwa la kwanza kumiliki nchi ambayo linapewa? (Amu. 1:2, 4) [Jan. 19, w05 1/15 uku. 24 fu. 5]
Kwa nini Baraka alisisitiza kwamba nabii wa kike Debora aende pamoja naye kwenye uwanja wa vita? (Amu. 4:8) [Jan. 19, w05 1/15 uku. 25 fu. 4]
Jina la madhabahu ambayo Gideoni aliijenga lilimaanisha nini, na tunajifunza nini? (Amu. 6:23, 24) [Jan. 26, w14 2/15 uku. 22-23 fu. 9]
Tunajifunza nini kutokana na jinsi Gideoni alivyowajibu Waefraimu wagomvi? (Amu. 8:1-3) [Feb. 2, w05 7/15 uku. 16 fu. 4]
Je, Yeftha alikuwa akifikiria dhabihu ya kibinadamu alipoweka nadhiri yake? (Amu. 11:30, 31) [Feb. 9, w05 1/15 uku. 26 fu. 1]
Kulingana na Waamuzi 11:35-37, ni nini kilichomwezesha binti ya Yeftha kutimiza nadhiri ya baba yake? [Feb. 9, w11 12/15 uku. 20-21 fu. 15-16]
Wakati ambapo hakukuwa na mfalme katika Israeli na ‘kila mtu alipokuwa akifanya yaliyo sawa machoni pake mwenyewe,’ je, hilo lilichochea machafuko? Eleza. (Amu. 17:6) [Feb. 16, w05 1/15 uku. 27 fu. 6]
Tunajifunza nini kuhusu kuendelea kusali kutokana na simulizi la Waisraeli kushindwa mara mbili na kabila la Benyamini lililoasi? (Amu. 20:14-25) [Feb. 23, w11 9/15 uku. 32 fu. 1-4]