Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr16 Oktoba uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2016
  • Vichwa vidogo
  • OKTOBA 3-9
  • OKTOBA 31–NOVEMBA 6
Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2016
mwbr16 Oktoba uku. 1

Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

OKTOBA 3-9

KUTAFUTA HAZINA ZA KIROHO

it-2 180

Ujuzi

Chanzo cha Ujuzi. Yehova ndiye Chanzo cha ujuzi. Bila shaka uhai umetokana na Yehova na ili mtu apate ujuzi anapaswa kuwa hai. (Zb 36:9; Mdo 17:​25, 28) Isitoshe, Mungu aliumba kila kitu, hivyo ujuzi wa mwanadamu unategemea kujifunza kazi za mikono ya Mungu. (Ufu 4:11; Zb 19:​1, 2) Pia, Mungu alitumia roho yake kuwaongoza waandikaji wa Neno lake kwa hiyo wanadamu wanaweza kujifunza mapenzi na makusudi yake. (2Ti 3:​16, 17) Hivyo, chanzo cha ujuzi wote wa kweli ni Yehova na mtu anayetafuta ujuzi anapaswa kumwogopa Mungu. Na woga huo utamsaidia kuwa makini ili asifanye mambo yatakayomkasirisha Yehova. Woga huo ndio mwanzo wa ujuzi. (Met 1:7) Kumwogopa Mungu kunamfanya mtu atake kupata ujuzi sahihi, lakini watu wasiomwogopa Mungu, wanafikia mikataa isiyo sahihi kutokana na vitu walivyochunguza.

OKTOBA 31–NOVEMBA 6

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | METHALI 17-21

it-2 818 ¶4

Fimbo

Mamlaka ya wazazi. “Fimbo” inatumika kuwakilisha mamlaka ya wazazi kwa watoto wao. Kuna marejeo mengi kuhusu mamlaka ya wazazi kwenye kitabu cha Methali, na neno hilo linalejelea kila namna ya nidhamu inayotolewa, na pia linatia ndani fimbo halisi inayotumiwa kutoa adhabu. Wazazi ndio waliopewa daraka na Mungu la kutumia fimbo hiyo kuwadhibiti watoto wao. Mzazi akishindwa kutimiza daraka lake, atasababisha uharibifu na kifo kwa mtoto wake na atamwaibisha Mungu na kukosa kibali chake. (Met 10:1; 15:20; 17:25; 19:13) “Ujinga umefungwa pamoja na moyo wa mvulana; fimbo ya nidhamu ndiyo itakayouondolea mbali.” “Usimnyime mvulana nidhamu. Ukimpiga kwa fimbo, hatakufa. Inakupasa wewe mwenyewe umpige kwa fimbo, upate kuikomboa nafsi yake na Kaburi.” (Met 22:15; 23:​13, 14) Kwa kweli, “anayezuia fimbo yake anamchukia mwana wake, lakini anayempenda ni yule anayemwangalia kwa nidhamu.”​—Met 13:24; 19:18; 29:15; 1Sa 2:​27-36.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki