Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp20 Na. 3 uku. 6
  • Jinsi Muumba Anavyofunua Ahadi Zake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jinsi Muumba Anavyofunua Ahadi Zake
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • NENO LA MUNGU LINAPATIKANA DUNIANI POTE
  • Biblia Ni Nini?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • ‘Waliongozwa na Roho Takatifu’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Biblia Ni Ujumbe Kutoka kwa Mungu
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
  • Biblia—Je, Kweli ‘Imeongozwa na Roho ya Mungu’?
    Amkeni!—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
wp20 Na. 3 uku. 6
Bosi akimpa mfanyakazi maagizo atakayoandika kwenye barua.

Kama bosi anavyomtumia mfanyakazi kuandika barua kwa niaba yake, ndivyo Mungu alivyowatumia wanadamu waaminifu kuandika Maandiko Matakatifu

Jinsi Muumba Anavyofunua Ahadi Zake

Zamani, Muumba wetu aliwasiliana na wanadamu kupitia malaika na manabii. Kwa kuongezea, aliamua ujumbe wake na ahadi alizotoa ziandikwe. Mungu anaahidi kwamba tutakuwa na furaha wakati ujao.Tunaweza kupata wapi ujumbe kutoka kwa Mungu?

Ujumbe wa Mungu unapatikana katika Maandiko Matakatifu. (2 Timotheo 3:16) Mungu aliwatumia manabii kuandika ujumbe wake. Jinsi gani? Mungu aliweka mawazo yake ndani ya akili za waandikaji, nao wakaandika mawazo hayo. (2 Petro 1:21) Kwa mfano, ikiwa bosi atamwomba mfanyakazi aandike barua kwa niaba yake, bila shaka ujumbe wa barua hiyo ni wa bosi na si wa mfanyakazi huyo. Vivyo hivyo, ingawa Mungu aliwatumia wanadamu kuandika ujumbe wake, yeye ndiye Mtungaji wa Maandiko Matakatifu.

NENO LA MUNGU LINAPATIKANA DUNIANI POTE

Ujumbe kutoka kwa Mungu ni muhimu sana, naye anataka watu wote wausome na kuuelewa. Leo, “habari njema ya milele” inapatikana kwa “kila taifa na kabila na lugha.” (Ufunuo 14:6) Maandiko Matakatifu yanapatikana yakiwa na vitabu vyote au vitabu vichache katika lugha zaidi ya 3,000. Hakuna kitabu kingine duniani kinachopatikana katika lugha nyingi kadiri hiyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki